Askofu Bagonza: Itungwe sheria maalum kujinaisha (Criminalize) vitendo vya kusifia viongozi wa Umma!

Askofu Bagonza: Itungwe sheria maalum kujinaisha (Criminalize) vitendo vya kusifia viongozi wa Umma!

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,790
Reaction score
288,165
INAFIKIRISHA! INASUTA! TUSUTIKE

Nilipochaguliwa kuwa Askofu baada ya wanaofaa kukosekana, marafiki zangu waliandaa tafrija ya kuniaga huko Chicago, Marekani. Mmoja wa watani wangu akatoa hotuba na kusema "Benson, wewe sasa ni Askofu. Tangu sasa una uhakika wa mambo matatu:

1. Daima utakula chakula kizuri
2. Daima utavaa vizuri
3. Daima hutaambiwa ukweli.

Ni miaka 19 tangu niambiwe na yote nimeyaona. Ufafanuzi wa niliyoyaona nitaufanya siku nyingine. Kimsingi Viongozi katika jamii tunaishi kwa kujidanganya, kudanganya na kudanganya.
Leo Nina hili:

Comrade Anthony Diallo amesema maneno mazito. Ametimiza ahadi ya mwana TANU/CCM isemayo "Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko". Ukweli uliochelewa ni bora kuliko uwongo uliowahi.

Nitoe ushauri ufuatao:

1. Viongozi na watawala wetu kama hawawezi kuzuia kusifiwasifiwa basi angalau wanune wakisifiwa.

2. Waliokwishamaliza muda wa uongozi wasijengewe masanamu au kutangazwa ni watakatifu mpaka muda maalum upite.

3. Ikithibitika kuwa kiongozi wa umma ngazi yeyote amewahi kuwa na tatizo la afya akili, maamuzi yake yote yatenguliwe.

4. Walioathirika au kunufaika na maamuzi ya kiongozi mwenye tatizo la afya ya akili wajulikane na kusaidiwa.

5. Itungwe sheria maalum kujinaisha (Criminalize) vitendo vya kusifia viongozi wa umma hadharani au kupendekeza ukiukwaji wa Katiba. Kuwasifia iwe sawa na kuwakashifu. Anayetaka kumsifia au kumkashifu kiongozi amwandikie barua binafsi. Kusifia hadharani ni rushwa.

6. Iwe marufuku wananchi kuwapigia makofi viongozi au kuwachezea ngoma, badala yake Viongozi wawapigie makofi wananchi na kuwachezea ngoma. Waliomba kutumwa, makofi ni ya nini?

Haya yote yanasisitiza msimamo wangu wa TUSUBIRI KUPONGEZA WALA KULAUMU.

Tangu enzi ya Mwalimu mpaka Samia, wanajitokeza watu wa kushinikiza kuvunja katiba ili Viongozi waongezewe muda wa kutawala. Wakiishakufa ndipo tunaanza kuambiwa mambo mazito yaliyokuwa yanaendelea nyuma ya pazia.

INAFIKIRISHA, INASUTA, TUSUTIKE.

8D358FBC-29B2-482C-9C41-74CC30F6DE6D.jpeg
 
Hivi visasi vya mwanafunzi wa nursing Bugando ambaye shule ilimshinda kabla ya kuhanja Maganzo! Tunamkumbuka
 
Walishangaa kwa sababu ulisema hadharani na kweli ungeweza kukamatwa, lakini waliikubali kauli yako. Yule dhalimu alimteka na kumuua Ben Saanane kwa kutaka elimu yake ifanyiwe uhakiki.

Niliwahi kulopoka nikiwa kwenye Basi kuwa Mwendazake ni mlemavu wa akili Abiria walinishangaa sana na walidhani ntakamatwa aiseh!!!
 
Back
Top Bottom