Inside10
JF-Expert Member
- May 20, 2011
- 29,909
- 32,414
Askofu Bagonza ameandika hayo kupitia ukurasa wake wa Facebook;
Mwaka 2019 tulitangaziwa kuna uchaguzi. Likawa shindano la kujaza fomu. CCM wakashinda. Wapinzani wakarudi darasani kujifunza kujaza fomu.
Mwaka huu tukatangaziwa, safari hii ni UCHAGUZI KWELI. Tukainuka kuhamasisha watu wajiandikishe. Wakaandikwa hata watakaofikisha miaka 18 miaka 5 ijayo. Idadi ya waliojiandikisha ikazidi ya wapiga kura. Tanzania tuna miujiza kweli.
Ghafla, uchaguzi “ukahairishwa” tukarudi tena kwenye mashindano ya kujaza fomu. CCM wameshinda tena. Wapeni maua yao. Lakini:
1. Nduguyo akikukosea muonye mkiwa wawili. Akikataa, chukua shahidi ukaonye tena. Akikataa liambie kanisa. Akikatalia kanisa, achana naye. Mwone kama mmataifa na mtoza ushuru (Mathayo 18:16-18). CCT, TEC na Bakwata wamesema tayari. Hata wasioomba wanaomba!
2. Wanyambo wana hekima isemayo; “Ukimwonya nduguyo ili afunike uchi wake akakataa, jiunge na wanaomcheka”. Nipo nacheka utadhani mazuri!
3. Tumemaliza ibada Musoma. Tumempata Mkurya mmoja akawa Askofu. Kofia ilitaka kugoma kuingia kichwani tukatamani tutafute ya jeshi. Yesu “aliyemteka” Mkurya akatii, kuna siku atawateka wanaokaidi maonyo ya kanisa lake kuhusu taifa.
4. Mgeni rasmi Prof John Kabudi, katupiga darasa ibadani. Ilani nzima ya chama chake imefunika mpaka wengine tukaondoka bila kula mchele. Katujulisha habari za BWAWA la umeme. Ahsante Prof LAKINI..
5. Watanzania hawa wanatamani Bwawa kubwa la kuzalisha Demokrasia. Bwawa hilo litalinda Bwawa la Umeme. Bila demokrasia wanaohujumu SGR watahamia kwenye umeme.
6. Najiuliza: Waweza kuwa na taifa huru lisilo na watu huru? Na je waweza kuwa na watu huru katika taifa lisilo huru? Niliwahi jibu swali nikiwa darasa la sita, lisemalo “Afrika ni Bara Tajiri lenye watu maskini: Jadili kwa kutoa mifano. Majibu yangu yalisababisha nifukuzwe shule mwaka mzima. Apumzike kwa amani Mwalimu aliyenifukuza.
7. Nimalize tafakuri yangu kwa kutoa pole kwa wahanga wa Kariakoo. Nitoe pole kwa familia Mama Kibiki. Waliomuua “wameishakufa” hata kama wanatembea. Nitoe pole kwa wote walioenda kwenye uchaguzi wakaambulia mashindano ya kujaza fomu. Nitoe pole kwa wote wanaolazimika kucheka wakati moyoni wanatamani kulia.
Nawaomba radhi wote niliowahamasisha kwenda kujiandikisha ili wapige kura. Nilidanganywa nami nikawadanganya. Sitarudia tena.
Mungu wetu ana kazi kweli kweli. Mwizi wa Kura anamuomba afanikiwe kuiba. Mlinzi wa kura naye anakanyaga mafuta ili alinde kura zisiibiwe. Lakini HADHIAKIWI.
Naipenda nchi yangu hata kama kuna wanaonilazimisha niichukie. Hata mkiniteka, SIICHUKII NCHI YANGU.