Katika andiko lake lenye kichwa cha habari, “Mashindano ya Kujaza Fomu: CCM Mshindi. Mpeni Maua Yake,”
Anasema, kama ni kushindana kujaza fomu nyingi za uchaguzi CCM wameshinda kabla ya kuchaguliwa.
“Mwaka 2019 tulitangaziwa kuna uchaguzi. Likawa shindano la kujaza fomu. CCM wakashinda. Wapinzani wakarudi darasani kujifunza kujaza fomu.”
Anasema; Mwaka huu tumetangaziwa tena lakini idadi ya waliojiandikisha imeonekana kuwa kubwa kuliko idadi halisi ya wapiga kura,
“Wakaandikishwa hata watakaofikisha miaka 18 miaka 5 ijayo. Idadi ya waliojiandikisha ikazidi ya wapiga kura. Tanzania tuna miujiza kweli.”
“Ukimwonya nduguyo ili afunike uchi wake akakataa, jiunge na wanaomcheka”. Sasa nacheka.
“Nimalize tafakuri yangu kwa kuwaomba radhi wote niliowahamasisha kwenda kujiandikisha ili wapige kura, nilidanganywa nami nikawadanganya, sitarudia tena".
"Mungu wetu ana kazi kweli kweli. Mwizi wa Kura anaomba Mungu afanikiwe kuiba, lakini Mungu hadhihakiwi. Ninaipenda nchi yangu hata kama kuna wanaonilazimisha niichukie. Hata mkiniteka, siichukii nchi yangu” Dkt. Benson Bagonza.