PreGE2025 Askofu Bagonza: Nimepokea taarifa kuwa 'Wasiojulikana' watakuja kunimaliza

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Ee Mwenyezi Mungu tunakuomba uiponye Tanzania yetu. Wasaidie viongozi wetu wapate akili, ufahamu na hekima ya kuongoza Wananchi vema.
 
Ameandika Baba Askofu Rev.Dr.Banson Bagonza (PhD), Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe
_______
Leo 8/5/2025, Papa wa 267 (Papa Leo XIV) amechaguliwa. Ni Mwana Chicago mwenzangu; Mwana CTU mwenzangu (CTU ni chuo kikuu cha Theolojia cha Kanisa Katoliki ambapo Bagonza kasoma hapo pia). Na ni Mwana Augustino mwenzangu (Msisahau Martin Luther alikuwa Padre wa O.S.A). Kwahiyo imekua siku njema kwangu.

Lakini pia imekua siku ngumu kwa sababu nimepokea taarifa kuwa “WASIOJULIKANA” watakuja kunimaliza. Hivyo nimeambiwa niishi kwa tahadhari. Sishangai maana ukimfuga mbwa ukamwachia aonje damu za watu, huwezi kumdhibiti tena na hawezi kuacha mwenyewe.

1. Kama kweli wanakuja; WAMEKOSEA. Wanaichafua serikali na taifa kwa jumla.

2. Kama hawaji, pia WAMEKOSEA. Bado Wanaichafua serikali na taifa kwa kuwaza kuja.

Kama wakija, nawaomba wasiharibu milango ya nyumba yangu na kuwafanya wanangu nitakaowaacha yatima waanze kufikiria kuitengeneza upya. Waniite nitatoka nijikabidhi.

Kama hawaji; namshauri mfuga mbwa awafungie mbwa wake ndani. Si kwa ajili yangu bali kwa ajili ya usalama wa mfunga mbwa mwenyewe na usalama wa kijiji chetu.

Huu ni mwaka wa uchaguzi. Hekima ni kutengeneza marafiki wapya kuliko maadui wapya. Usimuue mtu aliye tayari kufa. Hayo ni matumizi mabaya ya mauaji.

Awamu ya tano walikuja. Si lazima waje awamu ya sita hata kama awamu ya sita ni muendelezo wa awamu ya tano.

Iwe awamu ile au hii, hawa wasiojulikana ni waharibifu wa awamu zote mbili. Serikali makini (kama kweli haiwajui) ijitenge nao.

Wanaweza kufanya (kwangu) kwa sababu wameishafanya pasipotegemewa (TEC). Wakifanya wasijipongeze, wasipongezwe, na adhabu yao iwe ni kufanya MILELE.

Kama wakifanya; mwili utaoza, watu watalia, wengine watashangilia lakini watazaliwa wengine zaidi yangu.

Mungu analipenda taifa hili kuliko mimi ninavyolipenda. Hachelewi wala hawahi. Atasimama kulitetea.

Naishi katika jimbo la Waziri wa Mambo ya Ndani. Nina uhakika hajawatuma. Nawashauri wasitumie rungu kuua mbu aliyekaa kwenye kende za mfalme. Wala jiwe kumtungua kunguru aliyekaa kwenye kichwa cha Malkia.

Nawapenda Watanzania. Wakija kunichukua, tusipoonana tena, basi tutaonana kwa Baba kwa wale mlio na imani 🙏🏽
 
huyu muungwana asingekua mtu wa uzinzi kwa wake za watu waamini wake na mpachika mimba mahiri na kutekeleza watoto mitaani huko karagwe angekua mtu wa maana na wa kuaminika sana, but kwa alivyo naona nonsense tupu 🐒
 
Acha ujinga hata basi kula posho.Sisi tunaye mfahamu tokea USA we una unafahamu wapi zaidi ya kulamba kupumuliwa nyuma na CCM
 
huyu muungwana asingekua mtu wa uzinzi kwa wake za watu waamini wake na mpachika mimba mahiri na kutekeleza watoto mitaani huko karagwe angekua mtu wa maana na wa kuaminika sana, but kwa alivyo naona nonsense tupu 🐒
Pumbaf
 
Mfadhili wa ziara ya chadema Kagera, sijui huwa anawapanga wahasibu wa kanisa baada ya kuchota mamilioni na kuyaingiza katika siasa
 
huyu muungwana asingekua mtu wa uzinzi kwa wake za watu waamini wake na mpachika mimba mahiri na kutekeleza watoto mitaani huko karagwe angekua mtu wa maana na wa kuaminika sana, but kwa alivyo naona nonsense tupu 🐒
Yeye na kitima ndio mambo yao
 
Bogonza kumbe anachana mistarii!
 
Mama Yao na chawa kazidi sana utekaji.huenda aliyemuua magu ni yeye maana muuaji akianza kuua hawezi kuacha hiyo kazi ndiyo maana Kila siku utekaji
 
huyu muungwana asingekua mtu wa uzinzi kwa wake za watu waamini wake na mpachika mimba mahiri na kutekeleza watoto mitaani huko karagwe angekua mtu wa maana na wa kuaminika sana, but kwa alivyo naona nonsense tupu 🐒
Hii kazi mnayofanya kama mnafanya bure mtakuwa wajinga sana

Mmepewa kazi ngumu sana
 
Nimeogopa sana
 
huyu muungwana asingekua mtu wa uzinzi kwa wake za watu waamini wake na mpachika mimba mahiri na kutekeleza watoto mitaani huko karagwe angekua mtu wa maana na wa kuaminika sana, but kwa alivyo naona nonsense tupu 🐒
Hapo umemshambulia ki binafsi tuu,ila mawazo yake ni mchango mkubwa kwa Taifa letu.Huyu baba mi tunu....Tamaa hata wewe unazo
 
Hapo umemshambulia ki binafsi tuu,ila mawazo yake ni mchango mkubwa kwa Taifa letu.Huyu baba mi tunu....Tamaa hata wewe unazo
Hoja ndo huwa hawajibu --- yani mfano yunasema yote aliyomchafua sawa- haya jibu hoja yake , atakimbia tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…