PreGE2025 Askofu Bagonza: Nimepokea taarifa kuwa 'Wasiojulikana' watakuja kunimaliza

PreGE2025 Askofu Bagonza: Nimepokea taarifa kuwa 'Wasiojulikana' watakuja kunimaliza

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Aya ya kwanza ya askofu imekaa kimkwara zaidi
 
Nimepita kwenye vijiwe vya bodaboda kadhaa nikakaa kusikiliza maongeza yao nikagundua Nchi hii watu wameamka sana.
 
Bado ana kiu ya damu..... anataka wote wawe kama huyu.
chawa.jpg
 
From X/Twitter page yake👇🏻

".....#TANZANIA:
Anaandika Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Karagwe, Dk Benson Bagonza

KAMA NI KWELI; WAMEKOSEA: KAMA SI KWELI; WAMEKOSEA

Leo 8/5/2025, siku Papa wa 267 (Papa Leo Xiv) amechaguliwa. Ni Mwana Chicago mwenzangu; Mwana Catholic Theological Union (CTU) mwenzangu, na Mwana Augustino mwenzangu (Msisahau Luther alikuwa Augustianian), imekuwa siku njema na ngumu kwangu.

Ngumu kwa kuwa nimekuwa napokea taarifa na tahadhari kuwa“WASIOJULIKANA” watakuja kunimaliza. Sishangai maana ukimfuga mbwa ukamwachia aonje damu za watu, huwezi kumdhibiti tena na hawezi kuacha mwenyewe.

1. Kama ni kweli wanakuja; WAMEKOSEA. Wanaichafua serikali na taifa kwa jumla.

2. Kama si kweli, pia WAMEKOSEA. Wanaichafua serikali na taifa letu pendwa hata kwa kuwaza hayo.

3. Kama wakija, nawaomba wasiharibu milango ya nyumba yangu kuwafanya yatima kuitengeneza upya. Waniite nitatoka nijikabidhi.

4. Kama hawapo na kwa hiyo hawaji; nashauri kama nilivyomshauri mfuga mbwa kuwa awafungie mbwa wake ndani. Si kwa ajili yangu bali kwa ajili ya mfunga mbwa na kijiji chetu.

5. Huu ni mwaka wa uchaguzi. Hekima ni kutengeneza marafiki wapya kuliko maadui wapya. Usimuue anayetaka kufa. Ni matumizi mabaya ya mauaji.

6. Niwakumbushe machache:

i) Katika awamu ya tano walikuja. Si lazima waje awamu ya sita hata kama awamu ya sita ni muendelezo wa awamu ya tano!

ii) Iwe awamu ile au hii, hawa wasiojulikana ni waharibifu wa awamu zote mbili. Serikali makini, na hii ni makini, kama haiwajui, ijitenge nao siyo kutujulisha kuwa wapo.

iii) Wanaweza kufanya kwa sababu wameishafanya pasipotegenewa. Wakifanya, wasijipongeze, wasipongezwe, na adhabu yao iwe ni kufanya MILELE.

iv) Kama wakifanya; mwili utaoza, watu watalia na wengine watashangilia, LAKINI, ukweli hautazikwa, upumbavu wangu hautazikwa na watazaliwa wapumbavu wengine zaidi yangu.

v) Mungu analipenda taifa hili kuliko ninavyolipenda. Hachelewi wala hawahi. Atasimama kulitetea.

7. Naishi katika jimbo la Waziri wa Mambo ya Ndani. Nina uhakika hakuwatuma. Nawashauri wasitumie rungu kuua mbu aliyekaa makende ya mfalme, Watamuumiza. Watumie hekima, mbu ataondoka. Wasimtungue kwa jiwe la manati kunguru mchafu aliyekaa juu ya kichwa cha malkia. Wakikosea kidogo, jiwe litamjeruhi malkia.
ITOSHE SIKU KWA UOVU WAKE.

Nawapenda Watanzania. Tusipoonana tena, tutakutana kwa Baba wale mlio na imani...."


================================================
Mimi binafsi najiuliza swali hili kila siku, lakini nimeshindwa kupata jibu lake

#Serikali ya CCM chini ya Bi Samia Suluhu Hassan a.k.a Chura Kiziwi imepatwa na kichaa gani ambapo sasa kila anayeikosoa, anatafutwa ili auwawe? Wanaficha mambo gani ambayo hawataki watu wajue kiasi cha kujihami kwa staili hii...?

##Hivi jeshi letu la Polisi na vyombo vingine vya usalama kama TISS mnatupa ujumbe gani wananchi? Kwamba, mmeshindwa kabisa kukutia nguvuni kikundi hiki cha kigaidi kinachoendesha utekaji raia na kuua?

##Kama ninyi sio washiriki, na mmeshindwa kulinda usalama wa wananchi na mali zao, basi hamstahili kuwepo kwenye nafasi zenu hizo kuanzia Rais Samia Suluhu Hassan na wengine wote...!
 
huyu muungwana asingekua mtu wa uzinzi kwa wake za watu waamini wake na mpachika mimba mahiri na kutekeleza watoto mitaani huko karagwe angekua mtu wa maana na wa kuaminika sana, but kwa alivyo naona nonsense tupu 🐒
Mmmh, mtawamaliza maaskofu wote?
Mtaweza? Nataka nione.
 
Nimepita kwenye vijiwe vya bodaboda kadhaa nikakaa kusikiliza maongeza yao nikagundua Nchi hii watu wameamka sana.
Hamna kitu mkuu bado sanaaaa.Labda kwenye simba na yanga ndo wameamka!
 
Ameandika Baba Askofu Rev.Dr.Banson Bagonza (PhD), Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe

KAMA NI KWELI; WAMEKOSEA: KAMA SI KWELI; WAMEKOSEA

Leo 8/5/2025, siku Papa wa 267 (Papa Leo Xiv) amechaguliwa. Ni Mwana Chicago mwenzangu; Mwana Catholic Theological Union (CTU) mwenzangu, na Mwana Augustino mwenzangu (Msisahau Luther alikuwa Augustianian), imekuwa siku njema na ngumu kwangu.

Ngumu kwa kuwa nimekuwa napokea taarifa na tahadhari kuwa “WASIOJULIKANA” watakuja kunimaliza. Sishangai maana ukimfuga mbwa ukamwachia aonje damu za watu, huwezi kumdhibiti tena na hawezi kuacha mwenyewe.

1. Kama ni kweli wanakuja; WAMEKOSEA. Wanaichafua serikali na taifa kwa jumla.

2. Kama si kweli, pia WAMEKOSEA. Wanaichafua serikali na taifa letu pendwa hata kwa kuwaza hayo.

3. Kama wakija, nawaomba wasiharibu milango ya nyumba yangu kuwafanya yatima kuitengeneza upya. Waniite nitatoka nijikabidhi.

4. Kama hawapo na kwa hiyo hawaji; nashauri kama nilivyomshauri mfuga mbwa kuwa awafungie mbwa wake ndani. Si kwa ajili yangu bali kwa ajili ya mfunga mbwa na kijiji chetu.

5. Huu ni mwaka wa uchaguzi. Hekima ni kutengeneza marafiki wapya kuliko maadui wapya. Usimuue anayetaka kufa. Ni matumizi mabaya ya mauaji.

6. Niwakumbushe machache:

i) Katika awamu ya tano walikuja. Si lazima waje awamu ya sita hata kama awamu ya sita ni muendelezo wa awamu ya tano!

ii) Iwe awamu ile au hii, hawa wasiojulikana ni waharibifu wa awamu zote mbili. Serikali makini, na hii ni makini, kama haiwajui, ijitenge nao siyo kutujulisha kuwa wapo.

iii) Wanaweza kufanya kwa sababu wameishafanya pasipotegenewa. Wakifanya, wasijipongeze, wasipongezwe, na adhabu yao iwe ni kufanya MILELE.

iv) Kama wakifanya; mwili utaoza, watu watalia na wengine watashangilia, LAKINI, ukweli hautazikwa, upumbavu wangu hautazikwa na watazaliwa wapumbavu wengine zaidi yangu.

v) Mungu analipenda taifa hili kuliko ninavyolipenda. Hachelewi wala hawahi. Atasimama kulitetea.

7. Naishi katika jimbo la Waziri wa Mambo ya Ndani. Nina uhakika hakuwatuma. Nawashauri wasitumie rungu kuua mbu aliyekaa makende ya mfalme. Watamuumiza. Watumie hekima, mbu ataondoka. Wasimtungue kwa jiwe la manati kunguru mchafu aliyekaa juu ya kichwa cha malkia. Wakikosea kidogo, jiwe litamjeruhi malkia. ITOSHE SIKU KWA UOVU WAKE.

Nawapenda Watanzania. Tusipoonana tena, tutakutana kwa Baba wale mlio na imani.

View attachment 3328998
Ujumbe murua kwa wauaji.
 
huyu muungwana asingekua mtu wa uzinzi kwa wake za watu waamini wake na mpachika mimba mahiri na kutekeleza watoto mitaani huko karagwe angekua mtu wa maana na wa kuaminika sana, but kwa alivyo naona nonsense tupu 🐒
Alikupiga Mimba akakukimbia ?
 
Back
Top Bottom