GE2025 Askofu Bagonza: Tuache kutekana wala kukamatana kwa tofauti za maoni, Maoni siyo kura turidhiane kwanza

GE2025 Askofu Bagonza: Tuache kutekana wala kukamatana kwa tofauti za maoni, Maoni siyo kura turidhiane kwanza

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Kupitia ukurasa wake wa Mtandao wa Facebook Askofu Bagonza ameandika haya:


UCHAGUZI SI “Tumbo la Kuhara”: TURIDHIANE KWANZA.
Sikati tamaa kuleta wito wa MARIDHIANO katika Taifa letu kabla ya uchaguzi mkuu mwezi ujao. Uchaguzi Mkuu siyo “tumbo la kuhara” kutufanya tuharakishe bila kujali madhara ya kuharakisha kwetu. Kwa nini naamini katika maridhiano:

1. Mwaka 2020 tulipiga kura watu wengi na vyama vyote. Matokeo ya uchaguzi ule yanajutiwa mpaka leo. Hata waliochaguliwa wanauita ule kuwa ulikuwa UCHAFUZI.

2. Ikiwa wengi walishiriki 2020 na bado matokeo yake yakahojiwa na kulaaniwa, itakuwaje sasa wakati dalili zinaonyesha hamasa ndogo ya kupiga kura? Tushtuke. Ni hekima

3. Wakuu wa serikali na chama tawala wako kwenye kumbukumbu wakisema ule haukuwa uchaguzi na kuahidi hali ile isitokee tena. Sasa wagombea wameenguliwa, vyama vimefungiwa, kampeni ziko mahakamani kuliko viwanjani nk. Je Tutegemee matokeo tofauti na 2020?

4. Ukiacha nyongeza ya neno HURU kwenye tume inayosimamia uchaguzi, yaliyolalamikiwa mwaka 2020 bado yapo na tume ni ile ile. Hukumu ya Mpina (11/9/2025) imethibitisha kuwa uhuru wa Tume haupo maana inaweza kuingiliwa hata na ofisi ya Msajili. Je hili halitoshi kutufanya tukutane ili kuridhiana?

5. Sina hakika kama wadau wakuu wa demokrasia hapa nchini HAWAJANUNA! Yaani Vyama halisi vya upinzani, Asasi za kiraia (civil society), mashirika ya dini (TEC, CCT, BAKWATA, PCTC nk). Kama hawajanuna watabasamu basi tuwaone. Mnuno huo unaashiria hatari mbele

6. Taifa limegawanyika. Hawa wanasema tuchague; wale wanapiga kampeini tusichague. Bora tungekuwa tunabishania tumchague nani tu? Taifa moja, chaguzi mbili kwa wakati mmoja?! Tunahitaji hekima na UONGOZI. Na uongozi ni kujikana na kutanguliza taifa, siyo nafsi wala chama

7. Uhuru wa kukusanyika, kujieleza na kuchagua umefunikwa na hofu kuu. Uhuru wa kuabudu umepatwa na kwikwi mbaya. Ibada zinaingiliwa, nyumba za kuabudiwa zinaingiliwa kuliko maliwatoni😭. Hata kukusanyika kuombea mvua kinahitajika kibali. Huu ni msiba kwa Tanzania ya Kambarage. Msibani, hata shughuli za kuoa husimama mpaka tuzike. TURIDHIANE

8. Rais wetu amesisitiza “tusidharau miiba kwa kuwa misumari imelala”. Miiba yenyewe inampigia kampeini lakini haiamini sawasawa. MARIDHIANO ya kweli yanaitaka hata misumari isimame maana ni sehemu ya nyumba yetu tunayoijenga. Mdharau Mwiba, mguu huota tende. Je mpuuza msumari uliolala? TURIDHIANE

9. Katikati ya mchakato wa uchaguzi, watu bado wanakamatwa, wanatekwa, na waliotekwa zamani hawajulikani wako wapi. Kama hii si hujuma kwa mgombea wa serikali, basi waachiwe ili wapige kura ya shukrani kwa kuachiwa huru. Wanaovuruga amani wakamatwe wazi wazi ili kuzuia “uzushi” wa fulani katekwa. Kuna tofauti ndogo sana kati ya kutekwa na kukamatwa kinyume na utaratibu. Tuache kutekana wala kukamatana kwa tofauti za maoni. Maoni siyo kura. TURIDHIANE

10. “Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko”. Wagombea wote hakuna anayeahidi mabadiliko ya msingi katika taifa letu. Wana orodha ya vitu si masuala (Hardware Vs Software). Tuna matatizo makubwa katika kila sekta isipokuwa miundombinu na majengo. Asiyeona haja ya mabadiliko katika taifa letu, ana mpango wa kulihama. TURIDHIANE kuhusu vipa umbele vyetu

Dawa ya kupuuza inatibu sasa; si baada ya uchaguzi. Legitimacy ina nguvu kuliko bunduki. TURIDHIANE maana hatuna tumbo la kuhara

1757837045972.png


1757837167407.png
 
Back
Top Bottom