Ule wakati wa malipo kwa wale viongozi wa serikali waliokuwa juu ya sheria kipindi cha nyuma sasa dhahiri umefika.
Waliokuwa juu ya sheria si Sabaya peke yake bali ni wengi ila inabidi washughulikiwe mmoja baada ya mwingine kadri taarifa zinapopatikana na heshima ya awamu ya tano itaridhiwa tu baada ya kundi hili ovu kutengwa.
Walikuwepo wakuu wa mikoa na wilaya ambao walitumia nafasi zao za kazi za uongozi wa umma vibaya. Hawa walijipendekeza kwa hayati Rais Magufuli huku wakifanya mambo maovu.
Waliwanyima Watanzania wengine haki zao za kibinadamu na kujifanya wao ni raia wa hali ya juu (first class citizens).
Waliwaweka Watanzania wenzao korokoroni bila uhalali wowote na wakati mwingine walivuruga biashara za Watanzania wanaohangaika huku wakichukua mlungula kutoka kwa wafanyabiashara wenzao wakware.
Kama unayo taarifa au kumbukumbu yoyote ya viongozi waovu waliotenda vitendo hivyo tupia hapo chini ya Makonda mengine yamekwishasemwa kwenye mikeka huku JF na mengine yatajitokeza humu humu sasa tunaanza na mfalme mmoja aliyekuwa mkoa wa Manyara.
Mkoa wa Manyara ni moja ya mikoa kitovu cha rasilimali za madini pamoja na wanyamapori ya madini yamekwishasemwa sana hapa tupo kwenye rasiliamali ya wanyamapori.
Aliyekuwa mkuu wa mkoa huo Alexander Mnyeti ambaye kwa sasa hivi ni mmoja wa mabilionea vijana yeye alitumia nafasi yake kujitajirisha kwa kufunga jicho moja na kushirikiana na majangili.
Alishirikiana na majangili ya kiarabu kuvuruga maliasili hiyo ni baada ya kuondoka tu na kuja mkuu wa mkoa aliyehamishwa JOSEPH MKIRIKITI ndio tukaona hatua madhubuti ya kuwakabili majangili zimechukuliwa.
Majangili haya yamekuwa yakitumia ukwasi wa fedha kutoa hongo kwa maafisa wa serikali wa ngazi za juu na chini.
Hivi karibuni jangili mmoja aliyekubuhu aitwaye GERALD alitiwa hatiani na kupewa kifungo cha miaka 30 jela na bado kesi nyingine zinamkabili mahakamani.
Kipindi cha nyuma jangili huyu angepangua kesi zote kwa kutumia ukwasi wa waarabu ambao wanamtumia kwenye shughuli zao.
Hatahivyo, kesi aliyepigwa miaka 30 ikipelelezwa kiukweli hao wakware waarabu watabainika hivyo Mh Rais Samia Suluhu Hassan jihadhari na makundi ya waarabu wanaokuja serikalini kujidai wanataka kuleta mitaji kama watu wema na fanya uchunguzi wako mwenyewe utagundua nyuma ya pazia hakuna kilimo wala utalii ni ujangili tu na ushahidi upo wazi.
Huyu Mnyeti anadaiwa kujiingiza kwenye migogoro ya makampuni ya uwindaji kesi ziko mahakamani na alitumia madaraka yake vibaya kuzuia wenye biashara kufanya biashara zao bila kufuata taratibu za kiutawala.
Aliagiza wafanyabiashara kutiwa rumande bila uhalali wowote na haiwezekani haya yote yafanyike bila maslahi binafsi ya upande wake.
Hakuna ajabu yoyote ya yeye kuwa bilionea kijana kwani alipokuwa akifanya vitendo vya kukiuka sheria bila shaka alipata faida ushahidi wa vitendo vya ujangili vilivyokuwa vikifanyika wakati wa utawala wake na upo bayana waliokuwa wakifanya vitendo hivi walipata nguvu ya kujitapa kwamba wako na mkubwa sasa tunataka kujua ubilionea ameutoa wapi?
Tatizo moja tulilonalo ni kwamba vyombo mbalimbali vya umma vilikuwa vikiwalinda aina hii kina Ole Sabaya, Mnyeti na kadhalika walijieleza kama watoto wa hayati Magufuli na walikuwa untouchables.
Kwenye suala la Sabaya tulisubiri hadi mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan alipomsimakisha kazi na kuagiza uchunguzi ufanyike.
Ni wakati sasa vyombo vya dola vinavyohusika na haki za wananchi na utawala bora kuwashughulikia ipasavyo wote waliofanya maovu kipindi kilichopita na tunampomgeza Rais Samia kuchukua maaamuzi sahihi kuhusu Ole Sabaya.
Tunamshauri Rais Samia awamulike wote ambao kwa njia moja ama nyingine wanawalinda wale viongozi waliofanya maovu kipindi cha nyuma bila shaka na wao kwenye utawala unaokuja wa kufuata haki watapewa nafasi ya kujitetea.
Kama unayo taarifa yoyote ya wakware tupia hapa chini ni baada ya ukweli na uwazi tu ndio tutajenga taifa lenye kuheshimiana kati ya viongozi na wananchi.
Mheshimiwa Rais amechukua hatua nzuri waliokuwa wanapeleka mabega juu siku za nyuma na kujipatia utajiri washughulikiwe bila huruma yoyote maana nia zao zilikuwa kuwafanya watanzania wenzao maskini wakati wao wakijitajirisha kudadadeki.
Mwisho.