Askofu Bagonza: Tuliyajua, Hatukuyajua lakini hilo zaidi ya tatizo

Askofu Bagonza: Tuliyajua, Hatukuyajua lakini hilo zaidi ya tatizo

Inabidi iundwe Tume ya Maridhiano kama walivyofanya South Africa baada ya Utawala wa Kibaguzi kukomeshwa 1994, Tume ilikuwa chini ya Desmund Tutu, tusitumie utaratibu wa Kagame wa kuwapeleka Magakamani wale Wahalifu kwny Mahakama za Gachwachwa.

'Zamani Tajiri alikuwa anaweza kufanya lolote lakin Sasa hivi anaweza 'Kufanywa' lolote'- Kauli ngumu sana hii maana hata Madikteta kina Kagema hawana huu ujasiri wa kutamka haya hadharan

Kwa Niaba ya Wastaafu wa UV CCM Taifa tunawaomba radhi waliopata madhila ya kudhulumiwa Mali na nafsi zao na za Wapendwa wao
Hahaha umepatwa na nini? Alwtan Pohamba si ulisema una pharmacy Mwananyamala watakao vunjwa miguu na mikono utawauzia unga wa POP?
 
a) Tuache wazi milango ya uchunguzi kwa wateule wengine wanaotajwatajwa na kutuhumiwa kutenda uhalifu dhidi ya Katiba na sheria za nchi.
Na kwa kuwa uhalifu huu haukuanza na utawala wa Magufuli, nashauri uchunguzi uanzie huko kwenye awamu zilizotangulia ili mradi pawepo ushahidi unaojitosheleza.

Watu tumeumizwa sana.
 
TULIYAJUA, HATUKUYAJUA, HILI NI ZAIDI YA TATIZO.

Kesi iko mahakamani, sitaki kusema yaliyomo ya kesi hiyo. Najipa haki ya kusema jambo zima kwa ujumla wake.

Siku Rais Samia alipochukua ofisi nilipendekeza Mwongozo wa Kuongoza Kipindi cha Mpito wa awamu mbili, yaani kutoka ya 5 kwenda ya 6. Nimeupitia tena, sioni cha kubadili. Naweza kupuuzwa lakini madhara ya kunipuuza hayaepukiki.

Nilisema, Wateule wote wenye HULKA ya kukanyaga sheria na katiba kwa kisingizio cha uzalendo wapumzishwe. Nikongeza, hawa wateule ni "hatari kwa Rais kuliko walivyo hatari kwa nchi".

Unapokuwa na Mteule anayemiliki "jeshi" lake, "silaha zake", "benki yake" " dini yake isiyosajiliwa popote" nk. Na Mteule huyo ana uwezo wa kumkaribia Rais wetu, Makamu wake, Waziri Mkuu wetu, Spika wetu, Jaji Mkuu wetu, maabara zetu nk - huwezi kujua atafanya nini kuwadhuru ili afiche uhalifu wake.

Tuhuma zilizotajwa, ziwe zilitokea au hazikutokea, Taifa letu lina mgogoro mkubwa mikononi mwake. Kama yalitokea na hatukujua, ni tatizo. Kama hayakutokea lakini yanazushwa kumuonea Mteule, nalo ni tatizo. Kwa nini?

1. Mfumo wetu unaolilinda Taifa letu (system) ulifeli sana. Kama haukufeli bali uliona ukaandika taarifa kwa wakubwa na hawakuchukua hatua, bado ni tatizo la mfumo, si la wakubwa. Mfumo ujifunze kutumikia taifa na siyo kutumikia Viongozi na watawala. Baba wa Taifa alifikiri kwa makini kuuita "Mfumo wa Taifa", si Mfumo wa Rais au Viongozi.

2. Sabaya asingeweza kutenda haya au kufikiriwa kutenda haya bila msaada au kimya cha mfumo. Mnyororo wa kuwezesha uhalifu huu ni mrefu na kwa uchache unajumuisha Watendaji wa mfumo, Polisi, chama tawala, Media, TCRA, PCCB, RC na timu yake, wabunge wa maeneo, makanisa, misikiti, mfumo wa afya, na serikali za mitaa. Twaweza kumshughulikia Sabaya lakini tujue mnyororo huu una virus au vidonda vya hatari.

3. Haiwezekani kuwa Sabaya ni Mteule pekee aliyefanya haya nchi nzima. Wapo wengine, tena wengi. Nami nimewashuhudia kwa macho yangu. Nina mengi. Kumshughulikia Sabaya bila kukagua ripoti za mfumo ambazo hazikusomwa au zilisomwa zikapuuzwa , itakuwa ni kutibu dalili na kuacha ugonjwa.

4. Si madhambi yote ya wateule yanafaa kwenda mahakamani. Mengine tutumie kanuni ya Baba wa Taifa kuhusu Mke wa Kaizari. Wateule wote ama waishi ng'ambo ya tuhuma au waonekane kuishi ng'ambo ya tuhuma.

5. Ili kubaini madhara ya wateule kama Sabaya, kubaini kasoro za mfumo, kuponya Taifa, kuepusha yasitokee tena na kumtendea haki Mama Tanzania, nashauri yafuatayo:

a) Tuache wazi milango ya uchunguzi kwa wateule wengine wanaotajwatajwa na kutuhumiwa kutenda uhalifu dhidi ya Katiba na sheria za nchi.

b) Hata wasiotajwa lakini wangependa kuchunguzwa ili watamkwe kuwa safi, waruhusiwe kujitokeza na kuchunguzwa.

c) Wanaotajwa, wakitoa ushirikiano kwa chombo cha uchunguzi wasamehewe lakini wajiuzuru au kuvuliwa nyadhifa zao. Hata wakikutwa hawana hatia wajiuzuru kwa kuruhusu kutuhumiwa mambo mazito.

d) Watakaokutwa na hatia (si mahakamani bali mbele ya chombo cha uchunguzi) wasiruhusiwe kuwa katika utumishi wa umma au ofisi ya kuchaguliwa kwa kipindi maalum.

e) Viongozi wa kuchaguliwa, kuteuliwa, kuajiriwa na Viongozi wa imani waliojua au kushuhudia yaliyotendwa na wateule kama Sabaya lakini wakakaa kimya waone sababu ya kuwajibika kwa ama kujiuzuru, kuomba radhi, au kustaafu.

f) Waliotiwa hasara za mali au afya wafidiwe. Sehemu ya fidia itokane na mali za waliotenda makosa hayo.

g) Tuhitimishe mchakato huo kwa kuwa na siku ya kitaifa ya MWANZO MPYA. Siku hiyo wahanga washikane mikono na watesi wao.

NB: Maoni yangu yamejaa vionjo vya Imani yangu. Imani yangu si ya Taifa. Yasipuuzwe kwa udhaifu wa kuingiza Imani. Tuna tatizo kubwa na dawa yake si kulipuuza. Ukimwacha nyoka wakati unalima shamba, utamkuta wakati wa mavuno.

Ameandika : Kalikawe Lwakalinda BagonzaView attachment 1809165View attachment 1809166
Uwepo wa katiba mpya utapunguza uozo uliopo.
 
Kwa hiyo serikali iliyopo Samia mmempigia kura ,mpaka awatoe maafisa wa serikali waliochaguliwa na serikali iliyoshinda uchaguz?Kwa hiyo Bagonza ulishiriki katika dhambi ya kumuua Magufuli,ili mpange serikali mnayoitaka?
Magufuli amekufa kwa ujinga na upumbavu wake wa kudharau covid, alistahili kifo kile hakika!
 
Kwa hiyo serikali iliyopo Samia mmempigia kura ,mpaka awatoe maafisa wa serikali waliochaguliwa na serikali iliyoshinda uchaguz?Kwa hiyo Bagonza ulishiriki katika dhambi ya kumuua Magufuli,ili mpange serikali mnayoitaka?
Ni ama hujui au hukwenda kupiga kura kwenye uchaguzi wa 2020, wakati ule unapiga kura kwenye ile karatasi ya kura kulikuwa na picha ya Mafuguli na Picha ya samia pia, kwa hiyo wakati unachagua Magufuli ulikuwa pia unamchagua Samia, kwa maana hiyo Rais Samia aliyepo Madarakani sasa alipigiwa pia kura wakati huo! When you pray for rain you indirectly pray for mud!
 
Ni miaka 20 sasa imepita tangu uamuzi wa kuchoma kaya 135 uliotolewa na aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Serengeti Thomas Ole Sabaya , kuchomwa moto kwa kaya hizo kulitokea siku nne baada ya amri kutoka kwa mkuu wa wilaya kuwataka kuondoka eneo hilo kwa madai kuwa wananchi hao wanaishi katika eneo la Pori ala akiba la Ikorongo.

MAAMUZI YA MAHAKA BAADA YA TUKIO LA KUCHOMA NYUMBA HIZO.
Katika hukumu ya shauri namba 22/2005 lililofunguliwa na kaya hizo mbele ya Mahakama Kuu Kitengo cha ardhi kupitia msaada wa kituo cha Haki za Binadamu ,iliamuliwa kuwa kata hizo ziliondolewa kinyume na sheria na kuamuru warudishwe katika maeneo yao , akirejea Ibara ya 24 ya Katiba ya Jamhuri wa Muungano Tanzania , Jaji Mziray aliamuru kuwa kuondolewa kaya hizo katika maeneo yao ni kinyume na haki za binadamu.

KAULI YA SERIKALI.
Akielezea juu ya jambo hilo Naibu waziri wa Ardhi , Nyumba na Maendeleo ya Makazi alisema serikali iko tayari kutekeleza maagizo yote ya Mahakama na tayari imerekebisha hati ya makazi ya eneo hilo lenye ukubwa wa hekta 5000 ambayo ilikuwa inamilikiwa na kampuni bila binafsi kinyume na utaratibu.

Swali nalojiuliza huyu Thomas Ole Sabaya ana undugu na huyo Lengai Ole Sabaya?.....
Kama si ndugu, basi majina ya Ole Sabaya ni mabaya, myafute kama mmeshayaita ndugu au watoto wenu
 
Back
Top Bottom