Kiranja wa jamii
JF-Expert Member
- Jan 2, 2023
- 441
- 1,065
Anaandika Askofu Bagonza
Tulizoea kusema UJINGA NI MZIGO lakini kwa sasa UJINGA NI MTAJI wa makundi mbalimbali:
1. Viongozi wa Dini: Wanahitaji wajinga wengi ili wawauzie wokovu, utajiri hewa, uponyaji nk.
2. Wanasiasa: Wanahitaji wajinga wengi ili wawadanganye bila kukamatwa na wawajaze ahadi hewa.
3. Waganga wa kienyeji: Wanahitaji wajinga wengi wa kuwaletea kuku huku hao wajinga wakilishwa vinyesi na mikojo.
4. Walimu: Wanajitaji wajinga wengi ili wafanye mazoezi ya kufuta ujinga kwa kuuongeza.
5. Watumishi wa serikali wasio waaminifu: Wanahitaji wajinga wengi ili wawatoze rushwa na kuwauzia haki zao.
6. Wahisani na Wafadhili: Wanahitaji wajinga wengi ili wapate pa kupeleka misaada inayodumaza na kuwasaidia kumiliki uchumi wa wajinga.
7. Serikali: Inahitaji wajinga wengi ili waiogope. Kwa kawaida serikali huwaogopa wananchi wanaojielewa.
8. Matapeli wa Mitandaoni: wanahitaji wajinga wengi ili waweze kutajirika bila kufanya kazi.
9. Wafanya biashara: Wanahitaji wajinga wengi ili wanaoamini kuwa kuna duka la bei nafuu.
10. Umaskini na Maradhi: Wanahitajika wajinga wengi ili hawa ndugu waendelea kustawi.
Vita ya kupambana na ujinga haijaanza. Ikianza mniamshe. Hakuna kundi lisilo na mjinga. Ukichunguza kundi usimuone mjinga, tambua wewe ndiye mjinga.
NB: Mimi mniamshe siku mkimuona kiongozi yoyote anapambana watu wake waache ujinga kwenye nchi hii