Askofu Bagonza: Ujinga ni mtaji

Askofu Bagonza: Ujinga ni mtaji

Kiranja wa jamii

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2023
Posts
441
Reaction score
1,065
Anaandika Askofu Bagonza

Tulizoea kusema UJINGA NI MZIGO lakini kwa sasa UJINGA NI MTAJI wa makundi mbalimbali:

1. Viongozi wa Dini: Wanahitaji wajinga wengi ili wawauzie wokovu, utajiri hewa, uponyaji nk.

2. Wanasiasa: Wanahitaji wajinga wengi ili wawadanganye bila kukamatwa na wawajaze ahadi hewa.

3. Waganga wa kienyeji: Wanahitaji wajinga wengi wa kuwaletea kuku huku hao wajinga wakilishwa vinyesi na mikojo.

4. Walimu: Wanajitaji wajinga wengi ili wafanye mazoezi ya kufuta ujinga kwa kuuongeza.

5. Watumishi wa serikali wasio waaminifu: Wanahitaji wajinga wengi ili wawatoze rushwa na kuwauzia haki zao.

6. Wahisani na Wafadhili: Wanahitaji wajinga wengi ili wapate pa kupeleka misaada inayodumaza na kuwasaidia kumiliki uchumi wa wajinga.

7. Serikali: Inahitaji wajinga wengi ili waiogope. Kwa kawaida serikali huwaogopa wananchi wanaojielewa.

8. Matapeli wa Mitandaoni: wanahitaji wajinga wengi ili waweze kutajirika bila kufanya kazi.

9. Wafanya biashara: Wanahitaji wajinga wengi ili wanaoamini kuwa kuna duka la bei nafuu.

10. Umaskini na Maradhi: Wanahitajika wajinga wengi ili hawa ndugu waendelea kustawi.

Vita ya kupambana na ujinga haijaanza. Ikianza mniamshe. Hakuna kundi lisilo na mjinga. Ukichunguza kundi usimuone mjinga, tambua wewe ndiye mjinga.

NB: Mimi mniamshe siku mkimuona kiongozi yoyote anapambana watu wake waache ujinga kwenye nchi hii
 
Askofu Bagonza: "Ujinga ni Mtaji"? Alama ya kuuliza nimeiongeza.

Binafsi siamini kuwa ni "Ujinga". Hivi mtu anaweza akaachana na ujinga kwa kipindi fulani, halafu baadae akauokota tena ujinga ambao alikwisha achana nao?

CCM haitumii "ujinga" wa waTanzania, bali ilicho kifanya ni "KUWAFANYA WATANZANIA KUWA MATEKA.
Wewe fikiria hata sehemu ambazo huwezi kutegemea kuwepo wajinga; kwa mfano ndani ya kundi kama TLS (Tanganyika Law Society)' lakini kundi hili nalo limetekwa. Shuhudia wanavyo lazimishwa kuwapata viongozi wao kwa kuondolewa wasiotakiwa na CCM.

Hata huko ndani ya dini, CCM imejiingiza na kuwapata mateka. Viongozi wengi huko huwezi kuwaita kuwa ni wajinga, lakini wanatekwa kwa njia mbalimbali, wengine hata kupewa rushwa (milioni kumi zawaidi ya siku ya kuzaliwa kiongozi wa dini. Huku ni kutekwa, kama kiongozi huyo akikubali, siyo amegeuka na kuwa mjinga.

Mateka atajinasua vipi kutoka katika hali yake ya umateka?
Hili ndilo linalopaswa kujadiliwa kwa kina, hasa wakati huu tunapoelekezwa tuendelee kuukubali umateka wetu kwa kuwarudisha CCM kuendelea na utekaji wao.

tukishindwa kujinasua safari hii kwa amani, italazimu tuukate huu mnyororo wa umateka wetu kwa kumwaga damu ya waTanzania. Huko ndiko inakotupeleka CCM.
 
Kundi ambalo liongoza kwa kuwa na wajinga wengi ni bunge, lifuwatiwa na wakuu wa kuteuliwa.,
 
Askofu Bagonza: "Ujinga ni Mtaji"?
Alama ya kuuliza nimeiongeza.

Binafsi siamini kuwa ni "Ujinga". Hivi mtu anaweza akaachana na ujinga kwa kipindi fulani, halafu baadae akauokota tena ujinga ambao alikwisha achana nao?

CCM haitumii "ujinga" wa waTanzania, bali ilicho kifanya ni "KUWAFANYA WATANZANIA KUWA MATEKA.
Wewe fikiria hata sehemu ambazo huwezi kutegemea kuwepo wajinga; kwa mfano ndani ya kundi kama TLS (Tanganyika Law Society)' lakini kundi hili nalo limetekwa. Shuhudia wanavyo lazimishwa kuwapata viongozi wao kwa kuondolewa wasiotakiwa na CCM.

Hata huko ndani ya dini, CCM imejiingiza na kuwapata mateka. Viongozi wengi huko huwezi kuwaita kuwa ni wajinga, lakini wanatekwa kwa njia mbalimbali, wengine hata kupewa rushwa (milioni kumi zawaidi ya siku ya kuzaliwa kiongozi wa dini. Huku ni kutekwa, kama kiongozi huyo akikubali, siyo amegeuka na kuwa mjinga.

Mateka atajinasua vipi kutoka katika hali yake ya umateka?
Hili ndilo linalopaswa kujadiliwa kwa kina, hasa wakati huu tunapoelekezwa tuendelee kuukubali umateka wetu kwa kuwarudisha CCM kuendelea na utekaji wao.

tukishindwa kujinasua safari hii kwa amani, italazimu tuukate huu mnyororo wa umateka wetu kwa kumwaga damu ya waTanzania. Huko ndiko inakotupeleka CCM.
Mpaka kufikia hatua ya kutekwa huku ulikokuandika, HAPO UNAKUWA USHAKUWA MJINGA TAYARI
 
Back
Top Bottom