Mwanamwana
Platinum Member
- Aug 1, 2011
- 9,604
- 22,722
Anaandika Baba Askofu Rev.Dr.Benson Bagonza (PhD), Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe.
____
Utesaji unalivunjia heshima taifa letu. Zipo taarifa za uhakika kuwa katika jitihada za vyombo vya ulinzi kutafuta ushahidi, vinatumia mateso na udhalilishaji (torture) ili kuwalazimisha watuhumiwa waseme ukweli. Baadhi ya mbinu wanazotumia ni:
Kwa picha za watuhumiwa zinazoonekana, inaonyesha madai haya yana ukweli. Kwa simulizi za waliokutwa na mambo hayo, pia kuna ukweli. Wakati hayo yanatokea, mahakama ziko kimya na viongozi wetu wako kimya. Vitendo hivi vinavunja katiba, sheria na haki za binadamu.
Serikali zetu zinatumia fedha nyingi kusomesha askari na watu wa usalama ili wajifunze kupata ushahidi bila kutesa wala kutweza utu wa binadamu yeyote. Lakini bado wanatumia nguvu kama watu wasio na mafunzo. Vitendo hivi vinafanya iwe vigumu kwa wana diplomasia wetu kulitetea taifa mbele ya jumuia ya kimataifa.
Matokeo yake, wana diplomasia wetu wanaonekana vichekesho, waongo na wababaishaji. Tume ya HAKI JINAI ilitoa ushahidi wa haya mambo na kushauri hatua za kufanya. Tuheshimu hiyo ripoti. Hatuwezi kuwa na mifumo miwili sambamba ya utoaji haki nchini.
Mateso kwa watuhumiwa ni kielekezo kibaya cha serikali yoyote. Tuone aibu kufira ili kupata ushahidi. Ushahidi haufichwi kwenye njia ya haja kubwa. Kichaka cha mbinu hii ni sheria ya usalama (iliyotungwa mwaka jana) ambayo inawapa kinga watesaji. Sheria hii inastawisha uvivu wa kufikiri kwa vyombo vyetu vya ulinzi na kuchochea matumizi ya nguvu yasiyofaa. Acheni kutesa watu ili kupata ushahidi. Hata Guantanamo wameacha.!

- kuwavua nguzo zote watuhumiwa
- Kuwalawiti au kuwafira
- kuwapiga picha (wakiwa utupu)
- kuwaunguza kwa pasi za umeme
- kuwapiga korodani (wanaume) na matiti (wanawake)
- kuwaninginiza kwenye kamba kichwa chini na miguu juu
- kuwalisha vinyesi na mikojo yao nk