nditolo
JF-Expert Member
- Jul 2, 2011
- 3,731
- 4,271
Kuna wengine hamuwezi kuelewa hata kwa picture.Jina Askofu/ Padri/ Shekhe na majina mengine yanayowakilisha mjumbe wa Mungu, ni majina makubwa Sana, yanaheshima ya kipekee, Ni majina yanayopatikana Kwa sifa ya kubeba mamlaka nyingine, ili kulinda hadhi ya jina Hilo na kuondoa ukakasi na kuwapa watu Uhuru wa kuchambua mada mfu zinazoletwa na viongozi wa Dini, ni Bora wajisajiri hapa Kwa majina Yao halisi au majina feki, hii itawapa nafasi hata wafuasi wao kuchambua hoja zao
Maana kunahoja zingine zinaletwa hapa na viongozi wetu wa dini ni dhaifu na zinamaudhui ya kisiasa Wakati mamlaka walizozivaa hazina ushirika na siasa, Wala kuonesha upendeleo Kwa Baadhi ya makundi
Kwani, ikiwa Dunia itashindwa kuunganisha watu,moja Kwa moja inakuwa hata wao wanahusika kuibomoa jamii Kwa sababu ya kule kuegemea upande
Wakati umefika wa kila mtu asitumie cheo chake kuleta hofu ya watu kujadiri kile mtu anawasilisha hapa, Wajisajiri Kwa majina Yao, kama ni Jambo la kushauri watumie hivyo vyeo vyao, na nafasi ya kushauri hawa watu, wanaruhusiwa kuingia popote pale kupeleka Ushauri wao,
Vinginevyo vinavyofanyika hapa ni siasa Tu hakuna lingine,
Mtu ukizungumzia vita, mkuu wa nchi anaweza kutangaza vita hata akiwa kijijini kwetu kule Kimokela kule, na vita vtapiganwa
Raisi, mahali popote aweza kwenda na akafanya kituo na mipango yote ikaanza kufanyika Kutokea hapo alipo,
Je kwani akiwa Tu Dar-es-salaam ndio mipango mizuri ya kivita itafanikiwa!!
Baba Askofu, Kwanza ni lazima kutofautisha vita vya Kagera vita ambavyo unapigana na kitu kinachoooneka,
Baba Askofu, nilidhani Kwa upande wenu kama watumishi wa Mungu,na Kwa vile vita hivi ni vya Kiroho, basi nyinyi ndio muwe maamiri Jeshi wa vita hivi, maana Biblia ninayoisoma Mimi, inaniambia, vita vya kiroho hupiganwa katika ulimwengu huo huo wa Kiroho, inakuwaje ninyi ndio mnaanza kulalamikia huu ulimwengu usioona chochote?
Baba askofu anamanisha kuwa, hatukuchukua tahadhari yoyote. Lkn pia baada ya ugonjwa kuingia hatujajipanga kuushinda.
Leo hii wagonjwa wamejoficha ndani, majirani wanaogopa kutoa taarifa lakini wengine vifo vinawakuta bila kujulikana anaumwa Nini.
Mlipuko ni vita, ndio maana tunafanya mazoezi magumu wakati wa amani ili vita itakapotokea kupunguza vifo na majeruhi.
Hongera baba askofu
Sent using Jamii Forums mobile app