Hio ndio tafsiri ya "USHINDI WA KISHINDO (Kupita Bila Kupingwa)" Baba Askofu. Acha watanzania mpaka akili ziwasogee. Serikali yote CCM, Bunge lote CCM, Serikali za mitaa zote CCM, Mahakama zote CCM. Wananchi walitegemea nini??? Kumwita Tundu Lissu msaliti??? Acha sasa waone ni kina nani wasaliti kama sio CCM!!!!
Huko Kahama wamachinga wamechezea virungu kutoka kwa Mkurugenzi na Polisi. Mwanza watu wamekamatwa na Polisi. Mtaani kila sehemu ni vigenge vya kujadili hizi kodi mpya (Wakulima Kupandishiwa Kodi + Kodi Ya Mbolea + Kodi Ya Mafuta + Kodi Ya Mitandao Ya Simu + Kodi Ya Wavuvi).
Ama kweli CCM wana fitina mpaka kwa Mwenyekiti wao, wamejua kumchonganisha na raia, na wameamua sasa asimalize miaka 5 yake kama walivomfanyia Rais Mzee Mwinyi.
Safari hii swala la katiba hakizimiki hata kwa magari ya zima moto. Mtaani pata chimbika dadeki.