Askofu Bagonza: Wabunge wamekubaliana na Serikali kuwanyonya wananchi

Askofu Bagonza: Wabunge wamekubaliana na Serikali kuwanyonya wananchi

Mama akumbuke kuwa baadhi ya Mawaziri wake wanautaka Urais. Watamfitinisha na Wananchi ali apoteze Popularity...
 
Kwa bunge hili la sasa hakuna kitu,ni heri kipindi hiki,twende bila hilo Bunge hadi uchaguzi mkuu ujao kwa kuwa wabunge hawafanyi kazi za kibunge,pili kuna wawakilishi Covid 19 wasiowakilisha Chadema aka wabunge wa Ndugai. Tatu tukivunja bunge butu tutakuwa tumebana matumizi kisawa sawa mshahara wa mbunge kwa mwezi12,000,000 x wabunge 400,ukiongeza na mamlaka ya speaker na pesa za vikao tutaokoa pesa nyingi.
 
Huyu ni askofu asieelewa nn anakifanya ila anatumia haki yqke kikatiba kutoa maoni yake lkn uenda yeye Ni msomi kuliko Mimi lkn muumba bado hajamfahamisha maana navyotambua mihimili ya nchi iko mitato yaan mahakama bunge na serikal Sasa huyu serkali ndo kila kitu na rahis wa awamu ya tano alituambia ukwel hakuficha kwamba yeye ndo mkuu wa dola wengine mumsikilize yeye lkn Kama haitoshi nimuongezee askofu kwamba Dola Ni ukabaji,uporaji,ujasusi na dhuluma dhidi ya raia wake Sasa ukihubir haki au ukiitaka haki serkalini Ni kupikia jiko la kuni kwenye mafuriko ebu ajikite kwenye kuwaelekeza watu wasiwashangalie viongoz wa serkali pale wanapokuja na uongo isipokuwa wakimbilie kanisani wamuache mwana siasa abwabwaje mwenyewe
Haya maneno hayakupaswa kwenda kwa Bagonza, huyu Askofu alianza siku nyingi kuwatetea wananchi, wapo Maaskofu waliopaswa kuambiwa haya usemayo
 
"Tozo za miamala ya simu zimeunganisha mihimili bunge na serikali dhidi ya wananchi na walaji. Katiba inatenganisha mihimili hii miwili. Tozo zimeiunganisha. Ni kinyume cha katiba. Wabunge wamekubaliana na serikali kuwanyonya wananchi. Nani mtetezi wa wananchi?"

Askofu Bagonza

2847454_Screenshot_20210717-205013.png
 
Wananchi Tanzania miaka yote hawana mtetezi, na hata wananchi wakiamua kukimbilia kwenye mhimili wa tatu (mahakama) nako watashindwa kwasababu hizo tozo tayari zipo kisheria, hapa wananchi ni sawa na tumefungwa pingu mikononi na miguuni.

fact
 
Serikali inatukamua mpaka damu, viongozi wanakula na kusaza.
Si mnawaona wakipita na ma-V8 kwenda kuzindua vyoo vya shule?
Au nasema uongo jamaa zangu?
 
Tunahimizwa tuchangie kodi lakini ubadhirifu ukifanyika hauwekwi hadharani na wala hakuna anaewajibija. Matokeo ya tume ya wizi wa BoT yamefanyiwa kazi gani?
Vipi kuhusu repoti ya waziri mkuu juu ya faulo za wizara ya fedha....watumishi kujilipa mamilioni bila taratibu rasmi!?
 
Vipi kuhusu repoti ya waziri mkuu juu ya faulo za wizara ya fedha....watumishi kujilipa mamilioni bila taratibu rasmi!?
Ni mengi na yakiwekwa hadharani utagundua wengi wa hawa tunaowapigia makofi walitakiwa kuwa Segerea.
 
Wananchi Tanzania miaka yote hawana mtetezi, na hata wananchi wakiamua kukimbilia kwenye mhimili wa tatu (mahakama) nako watashindwa kwasababu hizo tozo tayari zipo kisheria, hapa wananchi ni sawa na tumefungwa pingu mikononi na miguuni.
Aisee, lakini wao ndio wanaiweka seriksli madarakani. Kuwatawala watanzania ni rahisi sana, ukiwaonea watalalamika badala ya kukuzuia.
 
Back
Top Bottom