issenye
JF-Expert Member
- Feb 2, 2011
- 3,795
- 5,255
dhehebu lake halina hicho cheo cha Askofu Mkuu bali wana mtu wanayemuita Mkuu wa Kanisa. Kingine ni kuwa kila dayosisi ina katiba yake.Huyu Mtumishi angekuwa Askofu Mkuu ingependeza
dhehebu lake halina hicho cheo cha Askofu Mkuu bali wana mtu wanayemuita Mkuu wa Kanisa. Kingine ni kuwa kila dayosisi ina katiba yake.Huyu Mtumishi angekuwa Askofu Mkuu ingependeza
Kwa mamlaka mliyonipa wanaJF,namtunuku Mhashamu Baba Askofu Bagonza (PhD), kuwa Askofu wa Taifa.Huyu Mtumishi angekuwa Askofu Mkuu ingependeza
Mbona vihoja badala ya hoja.....! Katiba ya Dayosisi inasemaje kuhusu muda wa Uaskofu!Bagonza ni mnafikini tu!
Nendeni kwenye dayosisi yake mkaone jinsi kalivyo ka dikteta!....
Wewe unamjua Bagonza kupitia mitandao ya kijamii! Waulize walioko kwenye dayosisi yake uone.Mbona vihoja badala ya hoja.....! Katiba ya Dayosisi inasemaje kuhusu muda wa Uaskofu!
Elezea Udikteta wake
Jibu hoja zake kuhusu ...Madaraka hayaondoi udhaifu!
mimi nipi Nyaishozi mkuu natembea kwa mguu tu kwenda kwa Askofu mwenye uelewa kuliko wote!Wewe unamjua Bagonza kupitia mitandao ya kijamii! Waulize walioko kwenye dayosisi yake uone.
Jibu lilitakiwa iwe ni nukuu ya kutoka kwenye katiba ya kanisa lake ili tuujue huo udikteta unaomtuhumuWewe unamjua Bagonza kupitia mitandao ya kijamii! Waulize walioko kwenye dayosisi yake uone.
Haa!kumbe kuwa askofu unajiita mwenyewe. Tumuogope Mungu.Huyu wakuchunga naye atulize mshono, yaaani baada ya Tanzania kukataaa kufungisha ndoa za ushoga kanisanii, aligeuka kuwa adui. Hata afanyeje tz hatuko tayari kwa hilo, kama anataka ahamie huko wapokubaliana
Na misaada hapati kabisaaa.
Ni kadikteta sana hako! Kwanza kana dharau sijui ndio hurka ya watu wa huko.mimi nipi Nyaishozi mkuu natembea kwa mguu tu kwenda kwa Askofu mwenye uelewa kuliko wote!
Naamini hata wewe Askofu unajua kuwa asiyefanya makossa, asiye na udhaifu wowote ni Mungu, Baba Yetu wa Mbinguni; aliyejitambulisha kwa Musa kuwa Yeye ni NIKO AMBAYE NIKO (Kutoka 3:14) na pia akajitambulisha tena kwa Musa kuwa MIMI NI YEHOVA (Kutoka 6:2). Huyo ndiye hakosei wala hana udhaifu. Wengine sisi wote pamoja na wewe Askofu hilo ndio KUNDI LETU.Ujumbe wa baba Askofu Dr.Benson Bagonza (PhD), mkuu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe.
____________________
Mwaka 2015 hatukuchagua malaika kuwa serikali. Tulichagua watu wenye ubinadamu. Watu hao na udhaifu wao wakaunda serikali. Serikali iliyoundwa na binadamu dhaifu, haiwezi kuwa takatifu kama malaika.
Kwa hiyo serikali ni dhaifu, kwa sababu imeundwa na watu dhaifu, na ilichaguliwa na watu dhaifu. Udhaifu maana yake ni "si kamilifu", "si takatifu" na ina uwezekano wa kufanya makosa.
Madaraka hayaondoi udhaifu. Madaraka si chanjo ya kuzuia kufanya makosa.
Kwa hiyo, nafasi au madaraka hayakingi uchoyo, ubabe, ulafi, uwongo, fitna, ukatili, upendeleo, ukabila, udini, ujinga, maradhi, na hila. Kisingizio cha "kufanya siasa" si kinga ya kuzuia madhara ya udhaifu huo.
Hali kadhalika, kutambua udhaifu si tiketi ya kuendelea kufanya makosa.
Kukubali kuwa unaweza kufanya makosa, ni ibada inayokubalika mbele za Mungu kwa sababu ni ukiri (admission) kuwa wewe si Mungu bali mwanadamu.
Kukiri udhaifu ni kupata nguvu, si kupoteza nguvu. Kunyenyekea ni kuhifadhi nguvu si kuogopa. Hapa ndipo tunakutana na tofauti kati ya ukatili na ujasiri, uungwana na unyonge.
Kama ningechagua, ningemheshimu anayenipa chakula kuliko anayeninyima chakula ili nimjue ana madaraka juu yangu.
Haki huanzia pale tunapokubaliana kuwa sisi ni binadamu wenye udhaifu katika kufikiri, kunena, kutenda. Waliopewa mengi, wadaiwa mengi. Yatosha siku kwa uovu wake.
Hasira ya Mwanadamu haitendi haki ya Mungu. Kisasi ni kwa Bwana wa visasi vyote, anayependa rehema kuliko sadaka!
Baba Askofu Bagonza