Askofu Dkt. Bagonza amshukia Lugola kwa kumfananisha Magufuli na Yesu. Asema hii laana lazima itafune mtu na Taifa

Mimi binafsi naona wazi Lugola anakera sana sana kuanzia kwa wananchi wa kawaida naamini vile vile anamkera sana Mh Rais wetu, lugha za Lugola ni za hovyo, hafai kuwa kiongozi, ni bahati mbaya tu alipewa uwaziri, naamini pia Oct 2020, CCM sitegemei impe nafasi ya kupita kugombea tena, Lugola ana maneno ya kufuru sana, mengi na anamkera sana Mh. Rais naamini hivyo, Lugola hapimi maneno yake vema kabla ya kuongea, na ana uwezo mdogo sana wa kufikiri
 
We unaongea kwa hisia. Wenzio tunaongea kwa kuona. Yaani unatumia hearsays.

Jibu Hoja usirahisishe mambo ,unaposema jambo flani ina maana unataka kufilisha ujumbe flani uio ukusudia.

Lugola amemfananisha Mh Rais na Yesu ,je ni sahihi ?
 
Mh rais anapenda kutukuzwa ndio maana akina Lugola, Kessy na wengineo wasaka vyeo wanajua ukimsifu bwana mkubwa anakuteua.
Na wenyewe wanapiga mule mule sema huyu Kange amepitiliza
 
Mwanzo ulikuwa una tetea kitu gani na sasa unasema nini ..!!
Haya kangi kashasema ni kama yesu je kuna cha kubadilisha kwenye kauli yake? au ndio kupotezeana muda kujadili jambo ambalo limeshasemwa na hakuna wa kulibadili, Mimi ninachojua ni kwamba, MAGUFULI SIO YESU KIRISTO, bali ni mwanadamu kama alivyokuwa Yesu kiristo akiwa hapa duniani.
 
Na spika akakaa kimya bila kukemea na kuamuru hiyo kauli ifutwe. Ina endelea kubaki kwenye kumbukumbu za bunge kwamba kuna mpuuzi mmoja alimuita Magufuli ni sawa na Kristo na maneno ya huyo mpuuzi yana ishi kwenye kumbukumbu za bunge la ajabu la Tanzania lililo ongozwa na Ndugai... Hii ni aibu
 
Hivi hamjui kwamba Yesu ni mwana wa Adamu na ni mwanadamu kama wanadamu wengine?? Yesu Kiristo "Mwana wa Adamu" ni kwamba Yesu alikuwa kweli binadamu. Mungu alimwita nabii Ezekia "mwana wa Adamu " mara 93. Mungu kwa njia nyingine alikua anamwita Ezekia binadamu. Mwana wa Adamu ni binadamu. Yesu alikuwa Mungu kamili (Yohana 1:1), lakini pia alikuwa binadamu (Yohana 1:14). Sasa neno "KAMA" Linapelekea mfanano wa moja kwa moja wa Magufuli kuwa YESU KIRISTO hapo ndipo sjui.
 

Upotoshwaji na Ujinga hauwezi kuachwa bila ya kukemewa Sababu utaharibu Taifa ,imagine ingekuwa amemfanisha na wa upande ule unafikiri ni nini kinge tokea !?.

Katika maneno ya Busara ya Baba Askofu ametoa mifano iliyo sababisha kutokea Mauaji na uharibifu wa Mali pia na kuchochea Chuki kwa baadhi ya Wajinga kufanya kama alivyo fanya Lugola,nimeahindwa kujua ni unasoma tu kama isha au tatizo ni uelewa wako.
 
KOMA kumfananisha YESU na midude mingine
 
Shida ya Mzee wangu Bagonza amejaa chuki, Chuki Imemjaa hata kwenye vitu vidogovidogo tu.
Mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni, hiyo ni kufuru ya wazi we unadai ana chuki? We kwako ni sawa Magu ni kama Yesu? Huko kusifia ndiko kunasababisha mnashindwa kumkemea pindi akoseapo huyo mpenda sifa kipofu wewe
 
Halafu bagonza sio mwema kiasi cha kuwanyooshea wengine vidole.
 
Mbona mifano aliyoiainishi pale mwanzo iko wazi? lakini Yesu alofananishwa na Magu sio hao binadamu wanaoitwa yesu vile vile ukumbuke kauli ya mkuu wa mkoa wa tabora siku za nyuma kuhusu Mungu amshukuru Magu japo aliitolea ufafanuzi. Anaepinga na askofu ndo ana chuki
 
Mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni, hiyo ni kufuru ya wazi we unadai ana chuki? We kwako ni sawa Magu ni kama Yesu? Huko kusifia ndiko kunasababisha mnashindwa kumkemea pindi akoseapo huyo mpenda sifa kipofu wewe
Mkuu tukubaliane kwamba Magu sio Yesu, ila kangi amesema RAIS MAGUFULI ni kama Yesu, kwa maana hyo ni kwamba, Magu(ulivyomtaja wewe) sio Yesu.
 
Halafu bagonza sio mwema kiasi cha kuwanyooshea wengine vidole.

Umeshindwa kutetea ulicho kuwa ukikisema mwanzo na kurukia Maisha binafsi ya Mtu ,jifunze kujadili Hoja na sio kumjadili mleta Hoja.

Lugola kumfananisha Mh Rais na Yesu ni sahihi !?
 
Hatochelewa kujibu soon. Keep cool.
 
Lugola kumfananisha Mh Rais na Yesu ni sahihi !?
Hakuna mahali Kangi amemfananisha Yesu Kristo mwana wa Adamu na Rais Magufuli, bali ametumia neno kama, neno ambalo halina mfanano wa moja kwa moja na kitu husika, Sasa wewe kwa akili yako unadhani YESU KRISTO MWANA WA ADAMU Anaweza kufananishwa na Mwandamu hapa duniani ingawa na Yeye YESU KRISTO alikuwa ni mwanadamu???? 😫👂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…