Askofu Dkt. Bagonza amshukia Lugola kwa kumfananisha Magufuli na Yesu. Asema hii laana lazima itafune mtu na Taifa

Mungu ametuumba kwa sura na mfano wake hivyo binadamu anamwakilisha mungu na ukimpenda binadamu umempenda MUNGU

Hivyo ufananisho yesu ni Mungu kwa mantiki ya kiteolojia isipokuwa ukiongeza maneno mengine yenye mrengo wa kushusha heshima yaMungu
Nae mwanadamu aliyevimbiwa Kodi za wananchi kupewa sifa ya Mungu ni kufuru
 
Rais alishawahi kusema siku akifika mbinguni atakua kiongozi wa malaika, sasa unajuaje kama hafurahii hizi sifa na utukufu anazopewa na wafuasi wake?!
 
Kweli kiongozi mkubwa wa kidini askofu. Kuna Mambo ya wanasiasa wanajitafutia laana wenyewe. Kwanza Magufuli hajamtuma huyo kenge. Kaamua mwenyewe kukufuru hakutumwa anatafuta Jimbo tuu.


Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa Jimbo halitafutwi hivyo! Kange kakosea Sana!! Ni vizuri Rais Magufuli akakataa hadharani kufananishwa na Yesu!!
Sifa alizo nazo rais Magufuli zinamtosha na ni nyingi Sana!! Naunga mkono kuongezewa awamu mbili zaidi Kama special case!! Lakini sifa ya kufananishwa na Yesu hapana!! Namwomba Kange afute kauli yake, ni uchawi huo!!
 
Shida ya Mzee wangu Bagonza amejaa chuki, Chuki Imemjaa hata kwenye vitu vidogovidogo tu.
1.Kwa Magufuli kwa sawa na Yesu ni sahihi?
2.Mungu kumuomba samahani Magufuli ni sahihi?
*Nadhani kuna fyuzi haziko sawa vichwani.
 
Nakuunga mkono mbinguni kwetu kange afute kauli au Magufuli akemee hili Jambo. Yesu ni Mungu.
 
Hii ndiyo kazi ya kiongozi wa dini.
Kama wewe umezoea kulamba makalio, huwezi fahamu kazi ya kiongozi wa kiroho
 
lugola anafata nyayo za mwigulu .labda anaweza akapata tena uwaziri
 
Tulia dawa ikuingie hata kama chungu
 
kwamba Utatu mtakatifu ni ulisukwa na wajanja? kwahiyo unamaanisha wanao amini hivyo nao ni wajanja? pili umesema magufuli anaikomboa tanzania kutoka muikono ya mafisadi ? ebu toa ufafanuzi maana mkuu wa nchi tulipo Pata uhuru alikuwa nyerere.akamkabidhi Mwinyi,naye akamkabidhi Mkapa, naye akamkabidhi Kikwete.Jee kumbe hao wali kuwa mafisadi?
 
Kati ya awamu zote, hii ya tano ndio imeweza kupambana na mafisadi kikamilifu. Ndio maana nimesema "kajitoa mhanga " Kulinganishwa na nabii Isa sioni la ajabu.
 
Hii ndiyo kazi ya kiongozi wa dini.
Kama wewe umezoea kulamba makalio, huwezi fahamu kazi ya kiongozi wa kiroho

Hao wamezoea kupokea pesa zitokanazo na rushwa na ufisadi kisha wanatoa na baraka kwa mafisadi huku wakijuwa hao mafisadi wanaumiza wanyonge bila kuwakemea.
Sasa hapo utasema wana haki ya kukemea viongozi wa serikari?
 
Nimesikiliza mchango wa Mhe. Kangi Lugola kwenye Bajeti Kuu ya Serikali 2020/21 inasikitisha na imekosa focus.

Mhe. Kangi Lugola hakupashwa awe Bungeni huyu Fisadi mkubwa na mla rushwa aliyebobea. Neno la Mungu linasema: AMELAANIWA AMTUMAINIYE MWANADAMU! Sifa zote alizoimba na mapambio yote kwa Rais Magufuli kiasi cha kumfananisha na Bwana Yesu Kristo hakika ni kufuru kwa Mwenyezi Mungu na Kangi Lugola atavuna hichi alichopanda maana Mungu hadhihakiwi!

Msamaha wa Rais Magufuli kwa MAFISADI WA CCM ndani ya Jeshi la Magereza chini ya Andengenye na Kangi Lugola ndiko kumepelekea Lugola kumwona Magufuli Kama Mungu wake.!

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…