Uchaguzi 2020 Askofu Emaus Mwamakula, wewe ni Mtumishi wa Mungu kweli kweli!

Uchaguzi 2020 Askofu Emaus Mwamakula, wewe ni Mtumishi wa Mungu kweli kweli!

Rasterman

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2015
Posts
33,894
Reaction score
44,117
Mtumishi wa Mungu Askofu, nakusalimu kwa Jina la Yesu Kristo.

Amani ya Bwana Iwe pamoja nawe.

Napenda kukuandikia barua fupi yenye maneno machache.

Napenda kukutambua rasmi kuwa wewe ni Mtumishi wa Mungu kweli kweli. Kazi yako ya upatanishi, haki na imani umeitendea haki, na Mungu akubariki sana.

Rasmi wewe ni Askofu na Mtu wa Haki, Imani na Mpatanishi. Nakulinganisha na Nabii Eliya wa Israel.

Ktk mchakato wote wa uchaguzi na kampeni umesimamia kuombea mikutano ya kampeni ya Lissu na kama Bwana aishivyo imefanikiwa kwa kiwango kikubwa. Hii ni matokea ya Sala zako kupokelewa kwa Mwenyezi Mungu na Insha Allah tutafanikiwa sana.

Nakupongeza sana umeniongezea kiwango cha imani kwa kujifunza kwa mtumishi kama wewe mwaminifu.

Kampeni zinakwenda vizuri na kwa kuwa wewe ni mtu wa haki na mwaminifu kwa Mungu. Mwenyezi Mungu Jehova ametenda maajabu mengi kupitia wewe.

Wewe ni Eliya wa Leo. Manabii wa Baal umewashinda kila mahali. Mbinu zao zote Bwana amewatia mikononi mwako.

Lisuu Oyeee!
 
Anakuwa ni mtumishi wa kweli pindi tu anaposimamia upande wa Chadema siyo?

Kwa tarifa yako, Mungu anao watumishi wake ambao pengine hata hawafahamiki kabisa na Watanzania wengi
 
Anakuwa ni mtumishi wa kweli pindi tu anaposimamia upande wa Chadema siyo?

Kwa tarifa yako, Mungu anao watumishi wake ambao pengine hata hawafahamiki kabisa na Watanzania wengi
Ulitaka awe upande wa mashetani harafu awe mtumishi wa Mungu?? Huyo automatically ni devil advocate
 
Back
Top Bottom