Ndugu Watanzania!
Rais Samia aliunda Time ya Jaji Lila kwa ajili ya kuchunguza au kubaini makundi makuu manne ya watu ambayo ni:
1. Watu waliopanga kile ambacho yeye alikiita kuwa ni matukio ya vurugu kabla, wakati na pia baada ya siku ya Uchaguzi wa 29 Oktoba 2025.
2. Watu walioratibu kile ambacho yeye alikiita ni matukio ya vurugu kabla, wakati na baada ya siku ya Uchaguzi wa 29 Oktoba 2025.
3. Watu waliofadhili kile ambacho yeye alikiita ni matukio ya vurugu kabla, wakati na baada ya siku ya Uchaguzi wa 29 Oktoba 2025.
Lakini kuna watu wengine ambao wapo katika makundi 4 ambao Tume ya Jaji Lila haijapewa kazi ya kuwachunguza na kuwabaini. Makundi hayo ni haya yafuatayo:
1. Watu waliopanga kupiga risasi na kuua watu ambao sisi tunawaita kuwa ni waandamanaji na ambao hawakuwa waandamanaji - wengine walifuatwa majumbani mwao, katika vibanda vya mpira, katika maduka na biashara zao, nk.
2. Watu walioratibu kupiga risasi na kuua watu ambao sisi tunawaita kuwa ni waandamanaji na ambao hawakuwa waandamanaji - wengine walifuatwa majumbani mwao, katika vibanda vya mpira, katika maduka na biashara zao, nk.
3. Watu waliofadhili kupiga risasi na kuua watu ambao sisi tunawaita kuwa ni waandamanaji na ambao hawakuwa waandamanaji - wengine walifuatwa majumbani mwao, katika vibanda vya mpira, katika maduka na biashara zao, nk.
4. Watu waliotekeleza kupiga risasi na kuwaua watu ambao sisi tunawaita kuwa hawakuwa ni waandamanaji - wapo waliofuatwa majumbani mwao, katika vibanda vya mpira, katika maduka na biashara zao, nk.
Kwa ujumla, kundi hili linahusisha watu walitoa amri ya kuua, watu waliotekeleza mauaji hayo, watu waliotoa fedha za kununua silaha na watu waliowalipa wauaji, nk.
Kwa katiba ya Tanzania kupanga maandamano; kuratibu maandamano, kufadhili maandamano na kufanya maandamano sio kosa la jinai wala sio kosa kabisa kisheria. Itabidi Serikali ya Rais Samia ithibitishe mahakamani kuwa waliouawa walipafanya vurugu, achilia mbali kuthibitisha kama zile zilikuwa ni vurugu na walichofanya (kuua watu wote wale ni kwa mujibu wa sheria.
Kwa muono wetu, Tume ya kuchunguza watu wote waliopanga, walioratibu, waliofadhili na waliotekeleza mauaji ndio Tume muhimu zaidi kuliko Tume ya kuchunguza watu waliopanga, walioratibu, waliofadhili na kutekeleza vitendo ambavyo Rais Samia anaviita ni vurugu lakini sisi tunaviita maandamano.
Watu waliowahi kushatakiwa the Hague ni wale waliotuhumiwa kupanga, kuratibu, kufadhili na kutekeleza mauaji; lakini sio waliotuhumiwa kupanga, kuratibu kufadhili na kutekeleza vitendo vya 'vurugu' (maandamano). Ni jambo la kushangaza kuwa kwa kiwango kikubwa cha mauaji kama yale, hakuna hata kamanda wa Jeshi la Polisi, Jeshi la Wananchi au Usalama wa Taifa anauechunguzwa kwa kutoa amri ya kuua mamia ya watu. Kwamba hakuna hata DC, RC au Waziri anauechunguzwa kwa kutoa amri ya kuua mamia ya watu kwa kiwango kile.
Lakini ni wazi kuwa jinai haiozi. Siku ambayo madaraka yatakuja kuondoka katika mikono ya watawala waliopo sasa, Watanzania watakuja kuunda Tume Huru ya kuchunguza watu wote waliopanga, walioratibu, waliofadhili pamoja na kutekeleza mauaji ya halaiki (massacres) ya 29 - 31 Oktoba 2025.
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Itunge, Dar es Salaam; 31 Oktoba 2026; Saa 2:10 usiku wa manane
Soma Pia: Tume ya Jaji Lila kuanza uchunguzi wa matukio ya Oktoba 29