Askofu Frederick Shoo: Viongozi wa dini wanapaswa kutoegemea upande mmoja wa siasa kwa kuwa watu wa vyama vyote ni waumini wao

Askofu Shoo mara kwa mara amejinadi kama mtu anayehusudu demokrasia na kuwa ni kiongozi mzuri.

Lakini katika kanisa la KKKT analoongoza anaibua migogoro mingi kwa udhaifu wake na udikteta wake wa kutokuwa tayari kuwasikiliza watu ambao wanatofautiana mitazamo.

Hivyo inajidhihirisha kwamba hana sifa za kukosoa serikali kama anashindwa kuongoza kanisa.
 
Kweli hujui ulisemalo, Wala Askofu Shoo humjui, wala KKKT huijui, huyu ni Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini Ila alichaguliwa kuwa kiongozi wa Dayosisi zipatazo 23 zene maaskkfu km yeye.
Ukimsikia kwenye siasa ni kwamba muumini wake wa Dayosisi anamzungumzia na tena ni Kanisani
Huko Konde matatizo NI yao na mikopo yao yeye kaenda kama Mkuu wa wenzake
Hebu fuatilia siasa zake na Askofu km Malasusa au Mwamasika ndio utajua km yupi ni dikteta
 
Mbona umekurupuka!!??
Baseless accussations!!
Hueleweki.
Ukidadisi utakuta huyu ni mhanga wa Dayosisi inaitwa Konde!
Mpigania haki za Yule aliyeambiwa Kura za wajumbe zimesema aondoke, yeye kasema haondoki!
Anaenda mahakamani, kung'oka hadi winchi!

Sijui dikteta ni yupi katika hawa!
 
Ujinga mtupu umeandika
 

Achakukurupuka kama Panyabuku waliovamiwa na Moto.

Baba Askofu Dr Shoo anahusika Vipi na migogoro ya Dayosisi nyingine !.
 
Kwa nini asingemuita Askofu Bagonza na Askofu Mwamakula,ili waongee faragha kwanza. View attachment 2169224View attachment 2169225
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…