Askofu Gamanywa: Nilimuombea hayati Magufuli nina uhakika amepokelewa mbinguni kwa Baba

Askofu Gamanywa: Nilimuombea hayati Magufuli nina uhakika amepokelewa mbinguni kwa Baba

Huyu Gamanywa alikuwa mara kwa mara anaalikwa TBC kipindi kile cha kampeni za uchaguzi, ni mbaya sana mtumishi kuwachagulia waumini wako mgombea. Bora uweke wazi sifa za mgombea mzuri, yeyote atakayeangukia hizo sifa atafaa, lakini sio kama alivyokuwa anafanya Gamanywa
 
Kati ya wapumbavu ninaotaka waondolewe TBC ni huyu Rioba, kaigeuza TBC kuwa chombo cha kumsifu na kumuabudu jiwe 24/7
Hapo ndiko kunakomwaribia nakumbuka Rioba alikuwa ni mchambuzi mzuri sana lakini mwisho amekuja kuishia mahali ambapo sio pa ndoto yake kwani miaka mitano sio sehemu ya ndoto yake.
 
Hivi huyu askofu anaelewa maandiko? Mtu anaenda mbinguni kwa kuombewa kweli? Yeye ni nani hadi amuondolee mtu dhambi zake na kuingia mbinguni. Ni huyu Gamanywa ninaye mfahamu kweli, ameanguka wapi huyu mtumishi?
Nakumbuka Gamanywa alikuwa anafundisha somo la Roho Mtakatifu sijui akujekuingia ktk mtego wa wanasiasa ambao sio mzuri kwake.
Nakumbuka ktk vipindi vyake pale TBC alikuwa anaingea mambo mengi yenye maswali kwa mtu anayejua Imani na Siasa ndo maana yule Shehe aliyekuwaga naye kwenye kipindi alikuwa makini sana kwani alikuwa anaongea kwa kubalansi na kutumia zaidi Imani kuliko kibinadamu.
Ila Mungu amsaidie Askofu uwezo wa Roho Mtakatifu urudi ili ajue alikokosea na toba imweke huru
 
Huyu Gamanywa alikuwa mara kwa mara anaalikwa TBC kipindi kile cha kampeni za uchaguzi, ni mbaya sana mtumishi kuwachagulia waumini wako mgombea. Bora uweke wazi sifa za mgombea mzuri, yeyote atakayeangukia hizo sifa atafaa, lakini sio kama alivyokuwa anafanya Gamanywa
Ndo maana yule Shehe hakutakaga kuingia ktk huo akaona kwani alijua maneno yake yanaweza kumpunguzia heshima ndo maana hawezi kuzungumziwa vibaya
 
Askofu Gamanywa amesema watu wasitegemee mama Samia kufanana na hayati Magufuli kwa sababu Mungu amemuumba kila mtu na kipawa chake.
Rais Samia atatimiza majukumu yake vizuri sana kulingana na kipaji alichobarikiwa na Mungu, amesema.

Askofu Gamanywa amesema wao walimuombea hayati Magufuli hivyo ana uhakika amepokelewa mbinguni kwa Baba.

Source Shallom tv
Duh Huyu Gwajima anastahili kifungo cha daima, anajijua Yeye na Uaskofu wake uko matatani mbele ya Muumba, kwa madhambi aliyoyatenda na anayoyatenda akilitumia jina la Bwana. Anajijua akimuombea mtu yoyote basi huyo Marehemu anakwenda matesoni, sasa huyu Gwajima ana Maana gani??????
 
Gamanywa siyo Gwajima!
 
Maaskofu wa kipentekoste wameanza kupotea taratibu
 
Back
Top Bottom