Askofu Gwajima akili kubwa sana, awauza polisi

Askofu Gwajima akili kubwa sana, awauza polisi

Bila kupoteza muda huyu jamaa mjanja sana.

Inasemakana ile video aliyorekodi kua yuko kanisani na nje kuna polisi ilikua danganya toto kuwapoteza maboya polisi.

Bila kufikiria mara mbili polisi wakaenda kujazana pale wakaambulia manyoya mtu kawaacha kwenye mataa. Gwajima pamoja na makando yake jamaa ana akili sana kuwalinganisha na viongozi wengi kwenye serikali jamaa alijifanya kasahau hadi tarehe ili ionekane yuko kwenye hatari😁 kumbe wapi.

Namtakia kila la kheri huko aliko kwa kufumbua fumbo la utekaji M/Mungu ambariki sanaa.
of course lazima alijua anatafutwa, hakai kizembe.
 
Huyo tapeli kichwa mbupu alikuwa anatesti zari, sasa yamemkuta.....
Ameona ubunge hapati tena, akaamua kujizima data....
 
Tume amrishwa tuheshimu mamlaka iliyopo madarakani.
Kutii kuna limit,

Mamlaka ikikwambia usiabidu ni ruksa kuiasi kama waliyofanya Daniel, Meshach and Abednego! Petro nk nk

Usome bible kwa ufahamu.
 
Pole na KAZI za mchana kutwa.

Pale ufufuo na uzima Kuna maombi ya kushindana.

Nakwambia ivi linawakuta Jambo pale KUNA MAJASUSI YA MBINGUNI NA NI MAJASUSI KWELI KWELI.

UTASIKIA SHABABAAAABAA LAKATIKASINO MOSIMOLIMOOO LAKATAKATAAA MASHIKATARASO SHARINAKAMBIZIZIIII KASEMONARISO

Hizo ni lugha za malaika na moto unawawakia wotee ni Jambo la mudaa
Nimecheka kama mazuri hivi, ila kweli wenda hili kanisa lipo na majasusi ya Mbinguni, mnakumbuka Mwanamapinduzi akiwa ameambatana na lissu walipozuhiliwa kwenda Ngorongoro pamoja na timbwili lote ,watu kukamatwa , mwanamapinduzi alichomoka kama mshale, badae akatoa clip akiwa polini ,alifikaje nyumbani kwake haijulikani
 
Kwa hela aliyonayo gwajima anaweza kuirudisha bikra ya mke wako, akawarudisha watoto wako tumboni Kwa mkeo akamuoa upya akampa mimba akawazaa watoto upya
Ameshindwa kutimiza ahadi alizowaahidi wananchi wa jimbo lake la Kawe hayo mengine atayaweza?!
Si angefufua angalau msukule mmoja kama alivyodanganya kuwa hata uwezo wa kumfufua kanumba anao?!
Huyu kaisha na ndio hatanyanyuka tena ila atakapofanya kile alichofanya ndugai labda kidogo watu wanaweza kumfikiria?!
 
Hivi huyo aliefungia kanisa hakuna mtu wa kuweza kuwateka watoto wake? Japo nae aonje utamu kidogo?
Kwanini kosa afanye yeye ( ikiwa kweli alichofanya ni kosa kisheria ) halafu kutekwa watekwe watoto wake?!
Kwanini mawazo yako yamekupeleka kwenye kuwateka watoto wake wasiokuwa na hatia badala ya kumteka muhusika aliyefungia kanisa hilo?!
Fikra zako ni kama fikra za kigaidi kama alshabaab na alqaida.!
Wao wanapokosana na serikali fulani badala ya kwenda kukabiliana na viongozi wa serikali walizokosana nazo kwa uoga wao wanakimbilia masokoni , mahospitalini na mashuleni kwenda kuwalipua kwa risasi na mabomu raia wasiokuwa na hatia!
Acheni mawazo ya kigaidi!.
 
Bila kufikiri mara mbili polisi wakajazana pale,akawaachia manyoya, Yeye Akala kuku!
Cha muhimu kanisa limefungiwa!
Yeye si alikuwa anasema serikali haiwezi kufungia kanisa lake na barua iliyopo mitandaoni ni ya uzushi toka kwa wahuni wanaoteka watu?!
Sasa na atie mguu pale kanisani kuendesha maombi aone vijana wa kamanda Jumanne Muliro watakavyombeba juujuu huku akitembelea vidole!
Mtu kakimbia na kuwaacha waumini wake kwenye matatizo halafu mnamsifia!.
Yesu alipofuatwa na wayahudi wanaotaka kumuua ( kwa mujibu wa biblia ) wanafunzi wake walikimbia na kumuacha Yesu akienda kusulubiwa peke yake!.
Yeye gwajima kawakimbia polisi na kuwaacha wafuasi wake wakisulubiwa peke yao!
Hiki alichofanya ni kitendo cha aibu sana wala sio jambo la kusifia.
Yeye angebaki pale na hao polisi wanaokuja kumkamta akawahubiria injili KWA JINA LA YESU hadi hao polisi waokoke na kutubu dhambi zao za kuteka watu kama anavyodai kuwa polisi ndio wanateka watu!
 
Nimecheka kama mazuri hivi, ila kweli wenda hili kanisa lipo na majasusi ya Mbinguni, mnakumbuka Mwanamapinduzi akiwa ameambatana na lissu walipozuhiliwa kwenda Ngorongoro pamoja na timbwili lote ,watu kukamatwa , mwanamapinduzi alichomoka kama mshale, badae akatoa clip akiwa polini ,alifikaje nyumbani kwake haijulikani
Ni kweli mkuu ni Jambo la muda TU.
 
Back
Top Bottom