Josephat Gwajima ni Askofu na mwanzilishi wa kanisa la 'Glory of Christ Tanzania Church' GCTC (Ufufuo na Uzima Ministries), kadhalika ni mwanasiasa ambaye mwaka 2020 alichaguliwa kuwa
mbunge wa jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM.
Askofu Gwajima mara kadhaa amekuwa akizungumza mbashara kupitia Mtandao wa
YouTube na kwamba anatoa ushauri wake kwa Taifa la Tanzania pamoja na viongozi wake hususani kuelekea uchaguzi mkuu 2025.
Madai
Ipo taarifa inayosambazwa mtandaoni ikidaiwa kutolewa na Askofu Gwajima kuwa amesema
"Leo Tarehe 27 Septemba, 2025, Saa 2:00 Usiku - Nitatoa Ushauri wangu kwa Watanzania Kushiriki uchaguzi wa 29 Oktoba, 2025 Kama Haki yao ya Msingi Kikatiba."
Je ni upi uhalisia wa taarifa hiyo?
Ufuatiliaji wa Kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu umejiridhisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli ni ya kutengenezwa na wapotoshaji kwani haijachapishwa na
Askofu Gwajima kwenye ukurasa kurasa zake rasmi za mitandao ya kijamii.
Vilevile grafiki zilizotumika kusambaza taarifa hiyo si za kweli, ni za kughushi kwani vyombo hivyo (
Mwananchi,
Jambo TV) havikuchapisha taarifa hiyo, bali wapotoshaji walitumia utambulisho huo ili kusambaza taarifa potoshi.