Mfikirie Vero. Mumewe aliuawa kwa kupigwa risasi, Oktoba 29 mwaka jana. Lakini kwenye Cheti cha Kifo, ikaandikwa sababu ya kifo ilikuwa "uti wa mgongo".Mnadhani Vero anawezaje kuipenda Serikali baada ya hapo?
Watoto wake, wakikua na kusoma hicho cheti, wakijua Baba yao alikufa kwa kupigwa...
Humphrey Isangya, baba mzazi wa Allen Humphrey (16), anadai mwanawe alipigwa risasi majira ya saa kumi jioni ya Oktoba 29, 2025, jijini Arusha. Anasema kuwa katika jitihada za kumtafuta mwanawe baada ya tukio hilo, alifanikiwa kupata kiatu chake pekee, huku mwili wake ukiwa haujulikani ulipo...
https://www.instagram.com/p/DfK43SzjUOo/
Mfadhili ajitokeza kumsaidia mtoto Angel aliyepigwa risasi Oktoba 29 Manzese: Kugharamia matibabu Muhimbili, makazi na elimu.
Mama wa Angel awashukuru Watanzania, mfadhili na Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa msaada wa hali na mali.
Pia soma ~ Mtoto wa...
Mchambuzi wa masuala ya siasa na kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Profesa Azaveli Lwaitama, amezitaja tume zilizoundwa kuchunguza matukio ya Oktoba 29, 2025, kuwa ni “mambo ya ujanja ujanja”, akidai kuwa zina lengo la kupunguza hasira za wananchi na kurejesha matumaini kwa...
Habari Wakuu
Mitandao huwa inatusaidia sana kuwaumbua watu wenye magamba mawili, Jana Oktoba 30, 2026, Sheikh Mwaipopo alidhihaki sana Misa iliyofanywa na Kanisa Katoliki kuwaombea Waliouawa wakati na baada ya Uchaguzi Oktoba 29, 2025, akaenda mbali kusema dhambi ya kuuwa wakati mwingine siyo...
Akiongoza Misa takatifu katika Kanisa Kuu la Jimbo Katoliki Bagamoyo kwa ajili ya kuwaombea waliouawa, waliopotea, waliojeruhiwa, na walioathirika katika uchaguzi uliofanyika Oktoba 29, 2026.Askofu Stephano Lameck Musomba (O.S.A), ameeleza kusikitishwa na namna Baraza la Maaskofu Katoliki...
Sheikh Mwaipopo amesema kuwa, “Kwa hiyo, hizi ibada zinazofanywa za ujanja ujanja, mngewaombea watu wengine. Kuna MV Bukoba iliyozama, mngewaombea waliokufa kwenye ajali hiyo, ingekuwa bora zaidi.”
"tufike sehemu ya Tanzania tuelezane ukweli. Kwa hiyo hizi ibada zinazofanywa za ujanja ujanja...
Mwaka mmoja baada ya Oktoba 29, Tanzania imepiga hatua gani kutoka katika kutambua yaliyotokea hadi kuweka wazi ukweli, kuwawajibisha wahusika na kutoa haki kwa walioathirika?
Ni takribani mwaka mmoja tangu Tanzania ikumbwe na doa kubwa katika historia yake kufuatia uchaguzi mkuu wa Oktoba 29...
Watanzania poleni kwa kumbukizi ya mauaji ya maelfu ya ndugu jamaa na marafiki kufuatia ghasia za uchaguzi mkuu wa mwaka jana maarufu kama mauaji ya oktoba 29.
Kwa kweli watanzania wameshindwa kusahau na kumove on. Ni mwaka sasa Serikali hii ya CCM ikijitahidi kumaliza mkwamo huu lakini naona...
Wakuu,
Mnaikumbuka hii amri? ‘Kazi Maalum’ ambayo ilifanywa na Jeshi la Polisi na ‘vyombo vingine’ ilikuwa ipi?
Mbona TUME zinazoundwa hazionekani kutaka hata kuanzia hapa? Kwanini target au mlengwa wa Tume zinazoundwa awe mwananchi na sio waliokuwa na ‘Kazi Maalum’?
Akizungumza katika kipindi cha Kivulini Talk, Mkuu wa Programu wa JamiiAfrica, Ziada Seukindo, amesema kuwa mwaka mmoja baada ya matukio ya Oktoba 29, bado kuna deni la ukweli na uwajibikaji.
"Unajua ni kama bado tunasubiri ukiangalia hata comments, social media ah ukiangalia event yoyote...
Kinara wa Ligi Kuu Simba Sc, leo yupo Ugenini dhidi ya Fountain Gate kwenye uwanja wa Tanzanite Kwaraa akiendela kusaka alama kwa ajili ya kujisimika zaidi Kilele.
Naini kuibuka na alama 3 leo?
Tarehe 14 Novemba 2025, Rais Samia alitangaza kuundwa kwa Tume ya Uchunguzi kuhusu mauaji yaliyotokea wakati na baada ya uchaguzi. Tume hiyo iliyoongozwa na Jaji Mkuu mstaafu Mohamed Chande Othman ilibaini kuwa watu 518 walipoteza maisha, wengi wao kwa majeraha ya risasi. Mwenyekiti wa Tume hio...
Hii ni misa ya leo tarehe 29, Oktoba 2026 iliyoongozwa na Padre Charles Kitima kwaajili ya kuwaombea marehemu na waathirika wa matukio ya uchaguzi wa mwaka 2025 Oktoba 29.
Na sisi tulioko majumbani na makazini tuendelee kuwaombea ndugu zetu waliopoteza maisha, lakini na familia zilizopoteza...
Almachius Vincent Rweyongeza, Askofu wa Jimbo Katoliki la Kayanga, Kagera
Na kutukana vikali kwamba maskofu wanavuruga amani ya nchi kwa kufukua makaburi. Basi ukaanza kujiuliza hapa wito ni matamuko hilo? Ni kufukua makaburi? Ukimia unayoga wa wananchi ni amani hiyo? Sasa naomba niwasomee...
Kwangu leo ni siku yenye maumivu mengi sana na siku ya huzuni nzito.
Nahisi kama vile nina PTSD. Sijui Kiswahili chake ni nini. Mnaojua saidieni.
Oktoba 29 imenifanya niwe mtu katili dhidi ya wale wote waliohusika na kuwaua Watanzania na wale ambao wanawaunga mkono hao wauaji.
Sikuwahi kuwaza...
Tunapokaribia kufanya Misa na ibada za kuwaombea wafu na wahanga wote wa matukio ya October 29, 2025, tunakwenda kuzijua Dini na Madhehebu ya Mungu pia tunakwenda kuzijua Dini na Madhehebu ya Shetani.
Dini na Madhehebu ya Mungu watafanya Misa na ibada za kuwaombea wahanga wa matukio ya October...
Habari za muda huu viongozi! kuanzia kesho jumatano tarehe 28/10/2026 watu wa NIDA watakuwa katika ofisi ya kata ya Mhandu iliyopo katika Wilaya ya Nyamagana, Mkoa wa Mwanza, watakuwa na kituo cha muda kwaajili ya kushughulikia watu ambao hawana vitambulisho vya nida.
Nakuomba uwatangazie...
Wakuu,
Ni mwaka mmoja toka yalipotokea maandamano, ambapo wengi miongoni mwetu walipoteza maisha.
Wengine ni ndugu zetu, jamaa zetu, marafiki zetu na hata majirani. Wengine tulinusurika lakini tumebaki na majeraha ya kudumu mioyoni mwetu, wengine walinusurika lakini wamepata ulemavu wa kudumu...
Akizungumza leo Oktoba 27, 2026, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika, ametangaza maazimio ya Kamati Kuu ya chama hicho ya kufanya kumbukumbu na maombolezo ya siku saba kwa ajili ya wahanga wa matukio ya Oktoba 29.
Mnyika amesema kufuatia kikao cha Kamati kuu...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.