PostGE2025 Je, mpaka sasa Serikali imewajibika kwa kilichotokea Oktoba 29, 2025?

PostGE2025 Je, mpaka sasa Serikali imewajibika kwa kilichotokea Oktoba 29, 2025?

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Upi Mtazamo wako ?

  • Tuipe Muda Tume

    Votes: 0 0.0%
  • Hakuna kitakacho tokea

    Votes: 4 50.0%
  • We live our life watajua wenyewe

    Votes: 0 0.0%
  • Who are you ?

    Votes: 4 50.0%

  • Total voters
    8

Ntemi_Ntale

Member
Joined
Aug 23, 2026
Posts
20
Reaction score
16
Tarehe 14 Novemba 2025, Rais Samia alitangaza kuundwa kwa Tume ya Uchunguzi kuhusu mauaji yaliyotokea wakati na baada ya uchaguzi. Tume hiyo iliyoongozwa na Jaji Mkuu mstaafu Mohamed Chande Othman ilibaini kuwa watu 518 walipoteza maisha, wengi wao kwa majeraha ya risasi. Mwenyekiti wa Tume hio (Jaji Mkuu mstaafu Mohamed Chande Othman) alisisitiza kuwa uwajibikaji unapaswa kufuatwa kwa haki na kwa mujibu wa sheria.

Ripoti ya tume haikutaja mtu wala taasisi yoyote kuwa na jukumu la mauaji hayo. Badala yake, iliwalaumu waandamanaji, hasa vijana, na ikasema madai ya miili kurundikwa mochwari au kuzikwa kwenye makaburi ya halaiki hayakuwa ya kweli. Vyama vya upinzani viliikataa ripoti hiyo na kuiita njia ya kuficha ukweli, vikidai uchunguzi wa kimataifa. Human Rights Watch nayo ilisema mamlaka bado hazijafanya uchunguzi kamili kuhusu nafasi ya vyombo vya usalama katika vurugu hizo. CHADEMA iliiomba UN na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kuchunguza mauaji hayo.

-------------------------------------------
Kwa ufupi ni Kwamba :
Serikali imechukua hatua rasmi (Tume, Ripoti, )
Mjadala uliobaki ni kama hatua hizo zimefikia uwajibikaji halisi, kwa kuwa hadi sasa hakuna aliyetajwa kuwajibika kwa vifo hivyo vilivyotokana na vurugu za oktoba 29,2025.


source :The chanzo & The Citizen

WhatsApp Image 2026-10-29 at 06.52.50-remove-the-social-media-ui-overlay-for-a-clean-pri (1).jpg
 
Hio picha ya huyo mama anaekimbia kisha wahuni wakampiga risasi ya kichwa bila huruma hapo unajua unatonesha kidonda unajua
 
kiukweli ile trh 29 sisi kama wa tzee tulikuwa tyr sanaa
 
Lengo ilikuwa kiwatuliza, mmetulia sasa tuendelee kupigika
 
Back
Top Bottom