Prof Lwaitama: Tume za kuchunguza Oktoba 29 ni janja janja tu

Prof Lwaitama: Tume za kuchunguza Oktoba 29 ni janja janja tu

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,922
Reaction score
3,252

​

Mchambuzi wa masuala ya siasa na kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Profesa Azaveli Lwaitama, amezitaja tume zilizoundwa kuchunguza matukio ya Oktoba 29, 2025, kuwa ni “mambo ya ujanja ujanja”, akidai kuwa zina lengo la kupunguza hasira za wananchi na kurejesha matumaini kwa makundi yanayodai mabadiliko.​


Akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Profesa Lwaitama amesema viongozi wa Serikali wanatumia njia mbalimbali kukabiliana na malalamiko ya wananchi, ikiwemo kuunda tume za uchunguzi, kutoa mikopo kwa vijana na kutoa fursa mbalimbali kwa viongozi wa vyama vya siasa.

Amesema hatua hizo zinaweza kuwa mikakati ya kuzuia vijana kulipuka kutokana na kupungua kwa matumaini kuhusu mustakabali wao.

“Yaani, hizi tume ni mambo ya ujanja ujanja tu. Hawa wanaofanya hizo tume wameshakwambia matumaini yakipungua, vijana watalipuka. Kwa hiyo wameweka mifumo ya kuwapa mikopo na kuwapa matumaini mengine,” amesema.

Ameongeza kuwa hata katika siasa kuna juhudi za kuwafanya viongozi wa vyama vya upinzani wajisikie kushirikishwa, akitolea mfano wa wagombea urais wa vyama mbalimbali kupewa magari wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopita.

Tume ya Chande iliundwaje?

Rais Samia Suluhu Hassan aliunda Tume ya Uchunguzi wa matukio ya uvunjifu wa amani yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, Novemba 18, 2025, akimteua Jaji Mkuu mstaafu Mohamed Chande Othman kuwa mwenyekiti.

Tume hiyo ilianza kazi rasmi Novemba 20, 2025, ikiwa na wajumbe saba wengine wenye uzoefu katika masuala ya sheria, diplomasia, usalama na utawala.

Ilipewa jukumu la kuchunguza chanzo na mazingira ya vurugu hizo, malengo ya waliohusika katika kupanga na kutekeleza matukio hayo, madhara yaliyojitokeza yakiwemo vifo, majeruhi na uharibifu wa mali, pamoja na hatua zilizochukuliwa kukabiliana na hali hiyo.

Baada ya uchunguzi wa siku 153, tume hiyo iliwasilisha ripoti yake kwa Rais Samia Aprili 23, 2026, ikieleza kuwa watu 518 walifariki dunia kutokana na matukio hayo, huku ikisema idadi hiyo huenda isiwe ya mwisho.

Tume hiyo pia ilieleza kuwa matukio hayo yalikuwa yamepangwa, kuratibiwa na kufadhiliwa, lakini haikuwataja watu binafsi waliohusika. Aidha, ilipendekeza uchunguzi zaidi kuhusu matumizi ya silaha na matukio mbalimbali yaliyohusisha vifo.

Tume ya Lila na uchunguzi wa wahusika

Baada ya ripoti ya Tume ya Chande, Rais Samia aliunda tume nyingine iliyoongozwa na Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani, Shaban Ally Lila, iliyozinduliwa Agosti 7, 2026.

Tume hiyo yenye wajumbe sita, wakiwemo majaji kutoka Tanzania, Uganda na Namibia, iliundwa kuchunguza kwa kina watu waliohusika na matukio ya vurugu na uvunjifu wa sheria wakati na baada ya uchaguzi huo.

Tofauti na tume ya awali iliyojikita zaidi katika kubaini chanzo, mazingira na madhara ya matukio hayo, Tume ya Lila imepewa jukumu la kubaini waliopanga, kufadhili, kuratibu na kutekeleza vurugu hizo pamoja na nafasi ya kila mmoja.

Pia inachunguza mazingira ya vifo visivyo vya kawaida, watu waliopotea, matumizi ya nguvu kupita kiasi na ukiukwaji wa taratibu katika kukabiliana na vurugu hizo.

Tume hiyo ilipewa siku 150 kukamilisha uchunguzi na kuwasilisha ripoti yake.

Akizungumzia tume hizo, Profesa Lwaitama amesema Tume ya Jaji Chande ilikwepa kulitaja CHADEMA katika maelezo yake kuhusu wahusika wa matukio hayo.

Amesema sasa macho yanaelekezwa kwenye Tume ya Jaji Lila, ambayo kwa mtazamo wake inaweza pia kugusa baadhi ya makundi yaliyopo ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Ametoa mfano wa aliyekuwa kada wa CCM, Humphrey Polepole, ambaye aliwahi kutoa kauli kuhusu kumwaga mafuta, akisema hatashangaa iwapo baadhi ya wanachama wa chama hicho waliokuwa na misimamo kama hiyo wataathiriwa na matokeo ya uchunguzi wa tume hiyo.

Azimio la Arusha na chanzo cha malalamiko

Akizungumzia chanzo cha matukio ya Oktoba 29, 2025, Profesa Lwaitama amesema yanapaswa kuangaliwa katika muktadha mpana wa mabadiliko ya mfumo wa kisiasa na kiuchumi nchini, akidai kuwa kuachana na misingi ya Azimio la Arusha na ujamaa kumechangia hali ya wananchi kujisikia kunyonywa na kupuuzwa.

“Ukitaka kujua kiini cha mwaka jana kilichotokea, ni matokeo ya kutelekeza Azimio la Arusha, matokeo ya kutelekeza mwelekeo wa ujamaa. Tumenyonywa kiasi cha kutosha, tumepuuzwa kiasi cha kutosha, sasa tunataka mapinduzi,” amesema.

Ameongeza kuwa hali hiyo imeongeza mgawanyiko wa kijamii na kiuchumi, akidai kuwa baadhi ya watu waliokuwa sehemu ya uongozi wa awali wamejipatia fursa za kiuchumi, ikiwemo kuanzisha kampuni zinazohusika na ujenzi wa barabara.

Profesa Lwaitama amesema viongozi wa nchi wanatumia mbinu mbalimbali kukabiliana na makundi yanayodai mabadiliko, akitaja wafuasi wa CHADEMA wanaosisitiza Katiba mpya na watu wengine wanaopaza sauti kuhusu mabadiliko ya kisiasa nchini.
 
Ni kweli kabisa ,hakuna Cha maan.

Wala hajakosea.


Uue alafu ujiundie tume
 
Utawala wa sasa hivi umejengwa kwenye misingi ya dhuluma na uovu. Uliunda tume bandia ya uchaguzi,l kusimamia uchaguzi bandia, imeunda tume mbili bandia za uchunguzi wa matukio ya Oct 29. Utawala ulikuwa na nafasi nzuri sana ya kujenga heshima na historia nzuri lakini ukabadilika na kuwa utawala haramu kuliko wowote uliowahi kuwepo katika historia ya Afrika nzima. Kwa sasa, kwa Afrika nzima, hakuna utawala katili uliokosa utu kuufikia huu wa kwetu!
 
Back
Top Bottom