PostGE2025 Askofu Musomba: TEC imeshambuliwa sana kwa kuwaombea waliokufa siku ya uchaguzi

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Akiongoza Misa takatifu katika Kanisa Kuu la Jimbo Katoliki Bagamoyo kwa ajili ya kuwaombea waliouawa, waliopotea, waliojeruhiwa, na walioathirika katika uchaguzi uliofanyika Oktoba 29, 2026.Askofu Stephano Lameck Musomba (O.S.A), ameeleza kusikitishwa na namna Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) linavyoshambuliwa kwa sababu tu ya kusimamia wajibu wake wa kiroho wa kuwaombea waliotangulia na kuliombea taifa haki na amani.

"TEC imeshambuliwa sana, Kwa sababu tu tunataka kuwaombea waliokufa siku ya uchaguzi na baada ya uchaguzi, waliopotea, waliojeruhiwa, walioathirika, kuiombea nchi yetu haki na amani, tumeshambuliwa."-Amesema Askofu Musomba

wow, lugha nzuri hadi raha kumsikiliza akiongea, kiswahili kimenyooka hakina doa. siku zote ukitaka kujifunza Kiswahili sanifu njoo kanisani halafu kwa uzoefu wangu ubora wa kiswahili unaongezeka jinsi unavyopanda juu ukimsikiliza askofu akiongea unaona kabisa kweli huyu ni Askofu btw kiswahili chetu grammar yake imetokana na Biblia hivyo Kanisa ndilo lililotengeneza grammar hii tunayoitumia leo hii, hivyo tunaongea Kiswahili cha Biblia.

rip na poleni wafiwa wote ...
 
Waliochukia marehemu kuombewa ni samuya na machawa yake, wala sio wengi ila wanavipaza sauti vyenye sauti kubwa!.
 
Akiongoza Misa takatifu katika Kanisa Kuu la Jimbo Katoliki Bagamoyo kwa ajili ya kuwaombea waliouawa, waliopotea, waliojeruhiwa, na walioathirika katika uchaguzi uliofanyika Oktoba 29, 2026.Askofu Stephano Lameck Musomba (O.S.A), ameeleza kusikitishwa na namna Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) linavyoshambuliwa kwa sababu tu ya kusimamia wajibu wake wa kiroho wa kuwaombea waliotangulia na kuliombea taifa haki na amani.

"TEC imeshambuliwa sana, Kwa sababu tu tunataka kuwaombea waliokufa siku ya uchaguzi na baada ya uchaguzi, waliopotea, waliojeruhiwa, walioathirika, kuiombea nchi yetu haki na amani, tumeshambuliwa."-Amesema Askofu Musomba

Hiyo ndio inaitwa kuanzisha vita ya mawe ukiwa ndani ya nyumba ya vioo.
 
Back
Top Bottom