Oktoba 29 NIDA kushughulikia watu ambao hawana Vitambulisho Kata ya Mhandu-Mwanza

Oktoba 29 NIDA kushughulikia watu ambao hawana Vitambulisho Kata ya Mhandu-Mwanza

OgaBoy

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2022
Posts
4,031
Reaction score
6,156
Habari za muda huu viongozi! kuanzia kesho jumatano tarehe 28/10/2026 watu wa NIDA watakuwa katika ofisi ya kata ya Mhandu iliyopo katika Wilaya ya Nyamagana, Mkoa wa Mwanza, watakuwa na kituo cha muda kwaajili ya kushughulikia watu ambao hawana vitambulisho vya nida.

Nakuomba uwatangazie wananchi wako ambao hawana vitambulisho vya nida wajaze fomu za NIDA na kuzigonga muhuri kisha waambatanishe na barua ya utambulisho kisha ambatanishe vitu na cheti cha kuzaliwa,ila kama hana cheti cha kuzaliwa aambatanishe moja kati ya vitu vifuatavyo;

1: Leseni ya udereva, 2: kadi ya mpiga kura, 3: cheti cha ubatizo, 4: cheti cha sekondari

5: Cheti cha darasa la saba

6: Cheti cha chuo kinachotambuliwa na serikali na kama ana namba za nida za wazazi wake ni vizuri akatoa kopi alafu akaambatanisha pale ila kama ana cheti cha kuzaliwa ni vizuri akakiambatanisha. kwa maelezo zaidi mwananchi afike ofisi za watendaji wa mitaa au kata ya mahina kupata ufafanuzi zaidi.

Naomba ujumbe huu tutume kwenye makundi mengine ya whatsapp au ya meseni za kawaida ili iwafikie wengi zaidi. zoezi hili litakuwa la wiki moja ila watu wakiwa wengi wataongeza muda.
 
Back
Top Bottom