PostGE2025 Mwaka mmoja baada ya doa la Oktoba 29: Je,Taifa linaelekea kwenye suluhu?

PostGE2025 Mwaka mmoja baada ya doa la Oktoba 29: Je,Taifa linaelekea kwenye suluhu?

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Anonymous

Senior Member
Joined
Apr 6, 2006
Posts
131
Reaction score
379
Mwaka mmoja baada ya Oktoba 29, Tanzania imepiga hatua gani kutoka katika kutambua yaliyotokea hadi kuweka wazi ukweli, kuwawajibisha wahusika na kutoa haki kwa walioathirika?

Ni takribani mwaka mmoja tangu Tanzania ikumbwe na doa kubwa katika historia yake kufuatia uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025. Katika kipindi hicho, iliripotiwa kutokea kwa mauaji, majeruhi pamoja na uharibifu wa miundombinu na mali mbalimbali.

Matukio hayo yaliweka Tanzania katika sura mpya, kwa kuwa historia ya Tanzania Bara haikuwa na kumbukumbu za matukio ya aina hiyo yenye athari kubwa kwa Taifa na jamii kwa ujumla, isipokuwa kumbukumbu za matukio ya uchaguzi Zanzibar yaliyowahi kuacha athari zinazoshabiana.

Baada ya matukio hayo, wadau mbalimbali walisisitiza umuhimu wa uwajibikaji ili hatua stahiki zichukuliwe na kuzuia matukio ya aina hiyo yasijirudie. Jumuiya za kimataifa, viongozi wa dini, jumuiya za kikanda, wadau wa kidiplomasia na mashirika ya haki za binadamu ndani na nje ya nchi walitoa wito wa kutaka kuwepo kwa uwajibikaji.

Katika hatua za awali, zaidi ya watu 500 waliripotiwa kukamwa kwa tuhuma za kuhusika na matukio mbalimbali, yakiwemo ya uharibifu wa mali. Baadhi yao walifunguliwa kesi mbalimbali, ikiwemo ya uhaini. Hata hivyo, baadaye wengi waliachiwa baada ya upande wa mashtaka wa Serikali kueleza kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi hizo. Ambapo pia kulikuwepo na sauti kwenye jamii na wadau kutoa wito wa watuhumiwa hao kuachiwa huru.

Safari ya Uwajibikaji Ilianza na Tume

Rais Samia Suluhu Hassan alitangaza kuundwa kwa Tume ya Rais ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 nchini Tanzania. Tume hiyo iliongozwa na Jaji Mkuu mstaafu Mohamed Chande Othman.

Tume hiyo iliundwa tarehe 18 Novemba 2025, kufuatia ghasia zilizotokea wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa tarehe 29 Oktoba 2025. Ripoti yake iliwasilishwa tarehe 23 Aprili 2026, ikibainisha kuwepo kwa vifo 518 vilivyothibitishwa, wakiwemo wanawake na watoto.

Tume ilieleza pia kuwa uchambuzi wa taarifa za uchunguzi wa maiti 219 ulibaini kuwa vifo 197 vilihusishwa na matumizi ya risasi. Hata hivyo, idadi ya vifo 518 haikutajwa kuwa ya mwisho, kwa kuwa huenda kulikuwa na vifo vingine ambavyo havikufika katika kumbukumbu za hospitali au za Tume. Aidha, Tume iliripoti kuwa zaidi ya watu 400 walikuwa wamepotea.

Tume ilieleza pia kuwa kulikuwa na vifo visivyo vya kawaida na kupendekeza uchunguzi zaidi wa matukio yenye viashiria vya jinai, pamoja na kuchukuliwa kwa hatua za kuwawajibisha wahusika.

Hata hivyo, tangu kuundwa kwake, Tume hiyo ilikumbana na ukosoaji kutoka kwa baadhi ya wadau walioitilia shaka, wakidai kuwa muundo wake ungeweza kuifanya ionekane kama chombo chenye mwelekeo wa kisiasa badala ya kuwa utaratibu wa kuhakikisha uwajibikaji wa kweli. Hata baada ya ripoti kuwasilishwa, baadhi ya wadau waliendelea kutoa ukosoaji wao hadharani na kupitia majukwaa ya mitandao ya kijamii.

Swali la uwajibikaji limeendelea kuwa hoja kuu, likijitokeza kwa namna tofauti kila matukio hayo yanapogusiwa katika hotuba za viongozi na mijadala ya kisiasa na kijamii.
Tume Nyingine ya Uchunguzi wa Kijinai.

Baada ya hatua ya kwanza ya uchunguzi, Rais Samia Suluhu Hassan aliunda Tume nyingine ya uchunguzi wa kijinai kwa lengo la kubaini wahusika wa matukio yaliyotokea.

Tume hiyo inachunguza kwa mtazamo wa kijinai ili kubaini watu waliopanga, kufadhili na kuratibu ghasia hizo, pamoja na mazingira na kiwango cha nguvu iliyotumika.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa kuhusu Tume hiyo, inaendelea kukusanya ushahidi na taarifa mbalimbali kabla ya kuwasilisha ripoti kwa Rais kuhusu masuala iliyokabidhiwa kuyachunguza, kwa mujibu wa hadidu zake za rejea.

Hata hivyo, Tume hiyo nayo imekumbana na ukosoaji kutoka kwa baadhi ya wadau, jambo linaloendeleza mjadala kuhusu uaminifu wa mchakato wa uchunguzi na namna ambavyo hatimaye uwajibikaji utatekelezwa.

Maswali na Hoja Zinazoibuliwa na Jamii

Kumekuwa na mtazamo miongoni mwa baadhi ya wadau kwamba tume hizo hazibebi dhamira halisi ya uwajibikaji, bali ni mkakati wa kuchelewesha hatua stahiki na kuifanya jamii isahau doa lililoachwa na matukio hayo. Hata hivyo, mamlaka zimeendelea kusisitiza kuwa uwajibikaji ni mchakato unaotekelezwa kwa hatua.

Lakini hoja ya uwajibikaji imeendelea kuibua wasiwasi kuhusu iwapo wahusika halisi watachukuliwa hatua za kweli au kama mzigo wa kuwajibika utaelekezwa kwa watu wengine.

Kupitia mijadala kwenye mitandao ya kijamii, baadhi ya wadau, wakiwemo baadhi ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), na wanaharakati wameendelea kusisitiza umuhimu wa kuundwa kwa tume huru ambazo, kwa mtazamo wao, zitakuwa na uwezo wa kufanya kazi kimuundo bila kuingiliwa.

Kwa msingi huo, swali linalobaki ni iwapo michakato inayoendelea itafikia hatua ya kubaini ukweli, kuwawajibisha wahusika na kutoa majibu yanayokubalika kwa jamii.

Maridhiano, Tume Huru na Katiba Mpya

Hoja ya maridhiano ilikuwa miongoni mwa ajenda zilizosisitizwa na upinzani kabla ya uchaguzi, wakitaka hatua za maridhiano zichukuliwe kabla ya uchaguzi mkuu hata hivyo hilo halikufanikiwa. Kwa upande wa Chama cha Mapinduzi (CCM), kupitia ahadi zake za siku 100 baada ya Rais Samia kuingia madarakani, kilieleza kuwa ajenda hiyo ingetekelezwa kuanza maridhiano na mchakato wa Katiba mpya.

Hata hivyo, hadi sasa ajenda hiyo haijatekelezwa kwa kiwango kilichotarajiwa na baadhi ya wadau. Kwa upande wa Serikali na CCM, hoja imekuwa kwamba mazingira ya kisiasa yaliyojitokeza yalifanya utekelezaji wa ajenda hiyo kuwa mgumu na kuathiri namna ambavyo maridhiano yangeweza kufikiwa kwa uhalisia uliokusudiwa.

Hata hivyo, katika kipindi cha mwaka mmoja, bado hakuna mabadiliko makubwa yanayoonekana ambayo yameweka mwelekeo wa moja kwa moja kuhusu utekelezaji wa mahitaji hayo.

Ikumbukwe kuwa Tume ya Jaji Chande, kupitia ripoti yake, ilishauri umuhimu wa kupatikana kwa Katiba mpya ifikapo mwaka 2028 ili iweze kutumika katika chaguzi zijazo, zikiwemo za mwaka 2029 na 2030.

Katika kipindi hiki, ushauri huo bado haujatekelezwa. Badala yake, kumekuwa na mitazamo na mijadala kuhusu umuhimu, muda na namna ya kushughulikia suala la Katiba mpya, ambalo pia limewekwa katika Ilani ya CCM ya mwaka 2025–2030.

Hali hiyo inaacha swali kuhusu lini madai hayo yataanza kuzaa matokeo yanayoonekana na iwapo yatakuwa sehemu ya hatua za kujenga upya imani ya wananchi katika mifumo ya kisiasa na kiutawala.

Madai ya Utekaji na Kupotea kwa Watu

Miongoni mwa hoja zilizozua hofu na kutajwa katika mijadala kuhusu sababu zilizochangia ghasia ni madai ya kutekwa na kupotea kwa baadhi ya watu, bila hatua stahiki kuchukuliwa kwa wakati ili kubaini walipo na mazingira ya kutoweka kwao.

Licha ya mamlaka kuwa na mitazamo tofauti kuhusu madai hayo, hofu na maswali yameendelea kujitokeza kutokana na kuripotiwa kwa matukio ya aina hiyo. Baadhi ya taarifa zimehusisha watu kudaiwa kupotea au kutekwa, huku wengine wakidaiwa kunyamazishwa au kuchukuliwa hatua kwa sababu ya kutetea haki.

Hali hiyo imeongeza maswali kuhusu ukweli wa matukio hayo: Watu wanaoripotiwa kupotea wanachukuliwa na nani? Kwa sababu zipi? Na wanapelekwa wapi?

Hadi sasa, kwa mujibu wa hali ya taarifa zinazojulikana bado hajulikani alipo mwanasiasa Humphrey Polepole, aliyekuwa kada wa Chama cha Mapinduzi na ambaye alidaiwa kutekwa, bado hajafahamika. Huo ni mfano mmoja wa watu wanaodaiwa kutekwa.

Baadhi ya wadau wanasema kuwa mazingigira hayo yameiweka jamii kuendelea kuishi katika kivuli cha hofu kutokana na kutotokomezwa kwa matukio hayo yanayodaiwa kutokea. Hali hii inaibua hoja upya upya juu ya umuhimu wa uwajibikaji, uchunguzi wa kuaminika na upatikanaji wa ukweli unaoweza kusaidia kupata suluhu ya kudumu.

Wapo wanoamini kuwa jamii inayotaka kujenga upya imani katika taasisi zake, majibu kuhusu watu wanaodaiwa kutekwa au kupotea ni muhimu. Bila majibu yanayoeleweka, hofu na mashaka vinaweza kuendelea hata pale ambapo mamlaka zinapotangaza hatua nyingine za kiutawala au kiuchunguzi.

Uwajibikaji wa Kisiasa

Licha ya Serikali kueleza kuwa hatua mbalimbali zimekuwa zikichukuliwa kama sehemu ya mchakato wa uwajibikaji, katika kipindi cha mwaka mmoja bado hakuna taarifa iliyo wazi kuhusu uwajibikaji wa moja kwa moja wa watu binafsi au taasisi unaotokana na matukio ya Oktoba 29 na ambao haujasubiri matokeo ya michakato ya tume.

Katika mijadala ya mitandao ya kijamii na majukwaa mengine, baadhi ya watu wamependekeza kuwepo kwa uwajibikaji wa kisiasa au binafsi kabla ya kungojea Tume.

Mapendekezo hayo yamehusisha baadhi ya viongozi kujiweka pembeni kutokana na matukio yaliyotokea wakati wakiwa katika nafasi ambazo, kwa maoni ya wanaotoa hoja hizo, ziliwapa uwezo wa kuchukua hatua za kuzuia madhara hayo. Wengine wamependekeza mamlaka husika kuwatoa baadhi ya viongozi katika nafasi zao.

Hata hivyo, hadi sasa hakuna taarifa rasmi iliyotajwa katika suala hilo kuhusu mtu kujiuzulu au kutenguliwa moja kwa moja kutokana na matukio ya Oktoba 29.

Hapo ndipo hoja ya uwajibikaji wa kisiasa inapoibua maswali: Je, uwajibikaji unapaswa kusubiri kukamilika kwa uchunguzi na kutolewa kwa ripoti, au kuna hatua za kisiasa na kiutawala zinazoweza kuchukuliwa mapema ili kuonesha dhamira ya dhati ya kurejesha imani ya wananchi?

Maelewano Baina ya Upinzani na Watawala

Kwa kipindi cha takribani mwaka mmoja, kumekuwa na msuguano wa kisiasa baina ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na mamlaka mbalimbali za kiutawala.

CHADEMA imeripoti kuwa baadhi ya wanachama wake wamefunguliwa kesi zinazohusisha makosa mazito, yakiwemo ugaidi na uhaini, huku pia ikitoa taarifa kuhusu wanachama wake kukamatwa na polisi na kuwekwa kizuizini kwa muda mrefu, katika mazingira ambayo chama hicho kimekuwa kikiyataja kuwa yanatia shaka kuhusu uzingatiaji wa taratibu za kisheria.
Wakati hali hiyo ikiendelea, mwenyekiti wa chama hicho Tundu Lissu ameendelea kuwa gerezani akikabiliwa na kesi ya uhaini.

Mlolongo wa matukio hayo umeifanya baadhi ya jamii na wadau wa kisiasa kuhoji iwapo hatua zinazochukuliwa zinasaidia kupata suluhu au zinaendeleza msuguano katika mazingira ambayo yanahitaji mazungumzo, maridhiano na juhudi za kuunganisha Taifa.

Kwa mtazamo huo, suala la uwajibikaji haliwezi kutenganishwa na mazingira mapana ya kisiasa. Kwa kuwa matukio ya Oktoba 29 yalikuwa na athari kwa jamii na siasa za nchi, hatua za kuyashughulikia zinatarajiwa pia kuchangia kupunguza migawanyiko, kujenga imani na kuimarisha misingi ya utawala wa sheria.

Mwaka Mmoja Baadaye: Maswali Bado Yapo

Haya ni baadhi tu ya masuala yanayoendelea kuibua maswali mwaka mmoja baada ya matukio ya Oktoba 29, 2025, yaliyoacha doa kubwa katika historia ya Tanzania.

Hadi sasa, sehemu ya jamii imeendelea kuonesha kiu ya kutaka ukweli wa kilichotokea ujulikane, wahusika wawajibishwe na haki itendeke kwa walioathirika.

Pamoja na hatua za uchunguzi zilizoelezwa na Serikali, bado kuna maswali kuhusu matokeo yatakayopatikana, namna yatakavyotekelezwa na iwapo yatatosheleza matarajio ya wananchi.

Kwa upande wake, Serikali imeendelea kusisitiza umuhimu wa amani na utulivu, ikieleza kuwa inachukua hatua stahiki kwa wakati ili kulinda amani na usalama wa Taifa.
 
Wale mujaheedina wa kikatoliki walitolewa chambo ili kutumika kisiasa hawana utofauti na wale wa shakahola
 
Huwezi kuua maelfu ya wananchi halafu wewe huyo huyo muuaji eti ndo uunde tume za kuchunguza yaliyotokea.

Akili za kipumbavu kabisa hizo.

Halafu hizo tume wala hazichunguzi mauaji yaliyofanywa.

Zinachunguza mambo tofauti kabisa.

Samia and her cabal of killers should go fucq themselves.
 
Huwezi kuua maelfu ya wananchi halafu wewe huyo huyo muuaji eti ndo uunde tume za kuchunguza yaliyotokea.

Akili za kipumbavu kabisa hizo.

Halafu hizo tume wala hazichunguzi mauaji yaliyofanywa.

Zinachunguza mambo tofauti kabisa.

Samia and her cabal of killers should go fucq themselves.
Sijasikia tume ikisema inachunguza aliyetoa amri ya shoot to kill Wala waliohusika na kushuti
 
Back
Top Bottom