POTOSHI Askofu Gwajima amesema yupo tayari kushiriki Uchaguzi

POTOSHI Askofu Gwajima amesema yupo tayari kushiriki Uchaguzi

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
JAMBO2.jpg
JAMBO1.jpg
MWANANCHI.jpg
MWANAHA.jpg
 
Tunachokijua
Josephat Gwajima ni Askofu na mwanzilishi wa kanisa la 'Glory of Christ Tanzania Church' GCTC (Ufufuo na Uzima Ministries), kadhalika ni mwanasiasa ambaye mwaka 2020 alichaguliwa kuwa mbunge wa jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM.

Mnamo tarehe 26 Oktoba, 2025 Askofu Gwajima alizungumza mbashara kupitia Mtandao wa YouTube ambapo awali alibanisha kuwa ni kauli yake kwa taifa la Tanzania na viongozi wake.

Madai

Kumekuwepo na taarifa inayosambazwa mtandaoni ikitumia utambulisho wa grafiki za vyombo mbalimbali vya habari kuwa Askofu Gwajima amesema yupo tayari kushiriki uchaguzi.


Je, ni upi uhalisia?

Ufuatiliaji wa kimtandao kupitia marejeo ya video umebaini kuwa taarifa hiyo si ya kweli kwani Askofu Gwajima hakutoa kauli hiyo alipozungumza kupitia mtandao wa Youtube.

Aidha grafiki zilizotumika kusambaza taarifa hiyo ni za kughushi kwani halijachapishwa na vyombo hivyo (Mwananchi, Mwanahalisi, Jambo TV) kupitia kurasa rasmi za mitandao ya kijamii.

Aidha katika mazungumzo yake askofu Gwajima kwa sehemu kubwa alisisitiza na alikemea matukio ya utekaji akisema haungi mkono uwepo wa matukio hayo na kwamba ni lazima kuwe na hatua za dharula kutatua tuhuma zinazoletwa kuhusu utekaji.​
Back
Top Bottom