Askofu Gwajima anamuonea Waziri Gwajima kijinga

Askofu Gwajima anamuonea Waziri Gwajima kijinga

Waumini wa makanisa haya wote ni wale wenye shida hii na Ile. Wako tayari kusikiliza mipasho kanisani. Amri Inasema usisengenye!!!!! Na kusengenya ni kumsema vibaya mtu ambaye hayuko miongoni mwenu kwa wakati huo
Anaesengenywa hasemwi hadharani au hujui maana ya kusengenya?

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Nna uwezo wakuwalisha familia yenu wote Hadi bwanaako!


Uzoefu unaonesha wenye uwezo huo huwa si wepesi wa kuandika kama ulichoandika wewe kwa hiyo inaleta shaka kuamini maandishi yako!

Hata hivyo hata kama ni kweli huo uwezo unao ndio utakakie wenzio wafanyiwe mabaya?

Hiyo ni roho ya aina gani?

Halafu wewe utafaidika na nini hasa?
 
Kwa kweli kati ya wote. Babamkwe/Baba mzazi amekosea sana. Na hii inaonekana kwenye family hiyo Gwajima (askofu) ni untouchable.

Pochi ndio shetani mkubwa
Inaonekana mzee anauza utu wake kwa ajili ya hela
Kuna watu hawana aibu wala Soni likija suala la hela
 
Gwajiboy ana bit za kale eti choma chanjo afu tukuone baada ya miaka mitano utakuwaje??? wtf

Nashangaa anajiita Askofu halafu ana haki ya kuishi hiyo miaka mitano
Haya maisha ni fumbo tunasubiri
 
Taperi gwajima afukuzwe kwenye chama na ubunge, na ashtakiwe kwa kesi ya uhaini
Hata akifukuzwa chama atabaki na ubunge na hapa ndipo lile andiko katika Mithali 26:27 linalosema Achimbaye shimo atatumbukia mwenyewe; Naye abingirishaye jiwe litamrudia.

CCM na Ndungai walichimba shimo wakidhani wanaikomoa CHADEMA kwa kuwakumbatia wabunge waliofukuzwa kutoka chama cha CHADEMA sasa inawarudia. Gwajima hafukuziki ubunge wanaweza kumfukuza chama ila si ubunge.


Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Pochi ndio shetani mkubwa
Inaonekana mzee anauza utu wake kwa ajili ya hela
Kuna watu hawana aibu wala Soni likija suala la hela
Yule Mama amewazaa akina Gwajima (wajukuu zake) hapo. Leo badala ya kuileta family pamoja ameleta mpasuko na ukabila .

Mpaka unaanza kusema sijui aliachika somewhere !! Sijui arudie jina la kabila lake ?!
 
Waumini wa makanisa haya wote ni wale wenye shida hii na Ile. Wako tayari kusikiliza mipasho kanisani. Amri Inasema usisengenye!!!!! Na kusengenya ni kumsema vibaya mtu ambaye hayuko miongoni mwenu kwa wakati huo
Amri ya wapi hii unakoti?

wewe hapo unaona ni usengenyaji au ni ukweli unaozungumzwa?
 
Gwajima jike aliacha kujibu hoja za Gwajima a.k.a Gwaji Boy akaanza kumshambulia. Sasa shuzi limepata mjambaji
Hilo ndilo kosa waziri Gwajima alifanya. Yeye angejikita kwenye kujibu hoja za chanjo bila kumshambulia askofu Gwajima binafsi. Alichofanya waziri ni character assasination badala kujibu hoja.
Kwa hilo hata simuungi mkono waziri hata kidogo.
 
Hao wapewe Bunduki wachapane,..tumechoshwa na ushirikina wao.
Askofu Gwajima kumuingiza baba yake mzee Gwajima kwenye upuuuzi wa hili ni kuonyesha uoga kwakuwa Waziri Dorothy na mumewe hawana ugomvi sasa baba mkwe anaingiaje kwenye ugomvi wa askofu na Waziri?
 
Hii dawa mpya imejulikana leo baada ya jiwe kutoweka, acha kutuletea uzwazwa.....
Waziri Dorothy ni Daktari wa binadamu, ule upuuzi wa kutumia pilipili kichaa na kujifukisha kutibu covid-19 alishikwa mateka TU JPM lakini hakukubaliana nao, hasa baada ya mtangulizi wake Dr. Faustine Ndugulile kutumbuliwa baada ya kusema kujifukiza sio tiba na ni hatari kwa maisha.

Dorothy alilazimika kuimba wimbo asioutaka wa malimao kwa mtutu wa bunduki, na sio yeye TU bali hata makamu wa Rais (mama Samia) nae alinaswa na ulimbo huohuo ndani ya awamu ya 5. Walikubali TU yaishe na ifike kesho.
 
Uswahili mwingi
Hao wanachambana kama wote wanawake yaani mpaka baba mkwe
Hawa watu wana bahati wanaishi kwenye society inayoendekeza mambo haya na ndio way of life
Wasukuma bana ni sheeeda. Haya yote tunayaona kwakuwa kuna musukuma aliyewahi kuukwaa urais kibahatibahati. Mbona kwenye awamu za 1, 2, 3 na 4 hatujawahi kuona nginjanginja hizi.
 
Ziko dawa, chanjo, na njia za matibabu ambazo zimeachwa kutumia wakati hapo mwanzo zilipitishwa na kuruhusiwa kutumiwa. Mfano, watu wameacha kutumia dawa kali kutibu minyoo, indocid, chloroquine na SP kutibu malaria, kuacha kutumia spirit kusafisha eneo la kuchoma sindano, kunyoa nywele za kinena wakati wa kwenda kwenye upasuaji, nk. Dawa, chanjo na njia za tiba zinabadilishwa na kuacha kutumiwa mara TU sayansi itakapogundua kuwa Ina madhara, haina faida au Kuna njia, dawa, chanjo mbadala nzuri zaidi ambayo inaleta matokeo bora kwenye jambo lile.

Sioni kosa la Waziri yuleyule, WHO ileile, TFDA ileile, TBS ileile, kukubali kuachana au kuongeza njia, dawa, au chanjo kwenye zile za awali. Huwezi kusema kwakuwa kuna penicillin kwa kutibu kaswende tusikubali aina nyingine za antibiotics kama erythromycin, azithromycin, ciproflaxin, etc.

Waziri Gwajima anakosa gani kutangaza dawa mpya na nzuri ya kutibu gonorhea, pumu, kisukari na covid-19 badala ya zile za zamani ? Kama kuna mtu anaemshangaa Waziri kwa hili basi mtu huyo ni ama mwehu au ana ajenda nyingine pana zaidi kuliko covid-19.

Tunapomtizama Askofu Gwajima msimtazame peke yake, watazameni pamoja na timu ya awamu ya tano iliyonyang'anywa usukani. Askofu na Polepole inawezekana wanatumika kama loud speaker TU kwenye mission fulani.
Lakini na wewe hujioni ni walewale? Hao wote kwa hadhi zao, wamekengeuka. Hawajadili UVIKO-19 tena bali wanashambuliana wao kwa wao. Sasa unapoongea hivi, ni kama hukusikia hata chembe namna waziri alimshambulia mchungaji ,asijue mchungaji ni zaidi yake kwa kuuchonga. Kwa kifupi, mimi simtazami mchungaji kama mwenye kujadili mada ya ya UVIKO-19 bali ninaona tu anatekeleza ule usemi, UKIMWAGA MBOGA, MIMI NINAMWAGA UGALI. Wamekutana.
 
Wasukuma bana ni sheeeda. Haya yote tunayaona kwakuwa kuna musukuma aliyewahi kuukwaa urais kibahatibahati. Mbona kwenye awamu za 1, 2, 3 na 4 hatujawahi kuona nginjanginja hizi.

Hilo ndio tatizo la wachunga ng’ombe akili za kuchunga tu
Majani yako wapi basi
Yaani hakuna wa kuwazaba makofi hao
 
Wakumfukuza Rashid ubunge ni kumwonea.
Rashid askofu ana hoja kuwa waziri hana uhalali wa kuhamasisha chanjo kwani awali alipinga na aliabudu mizizi. Kwanini hili tunalikwepa?
Askofu Gwajima ni heri angesoma alama za nyakati, wenye chanjo sio watu wa mchezomchezo. kule Facebook wameshaanza kumshughulikia,kwa kuufuta ujumbe wake kuhusu chanjo.

Ninamsihi aiondoe ngoma yake juani, maana ngoma inayovuma sana ndio ya kwanza kupasuka. Gwajima na wenzake wanaidhihaki serikali ya Rais Samia. Nina uhakika kuwa Askofu Gwajima anafahamu kuwa Waziri Gwajima anatekeleza maagizo ya Rais Samia kama vile alivyokuwa anatekeleza maagizo ya JPM kwenye awamu ya Tano. Gwajima na wenzake wanamchallange Rais, Dorothy ni kisingizio TU.
 
Waziri Dorothy ni Daktari wa binadamu, ule upuuzi wa kutumia pilipili kichaa na kujifukisha kutibu covid-19 alishikwa mateka TU JPM lakini hakukubaliana nao, hasa baada ya mtangulizi wake Dr. Faustine Ndugulile kutumbuliwa baada ya kusema kujifukiza sio tiba na ni hatari kwa maisha.

Dorothy alilazimika kuimba wimbo asioutaka wa malimao kwa mtutu wa bunduki, na sio yeye TU bali hata makamu wa Rais (mama Samia) nae alinaswa na ulimbo huohuo ndani ya awamu ya 5. Walikubali TU yaishe na ifike kesho.
Galileo aliuliwa kwa msimamo wake kuwa dunia ni duara, petro aliuwawa kikatili kwa kutetea yesu alikuwa mwana wa mungu huyu Dr aliyemeza glass ya juice ya pilipili mbuzi akitetea uwaziri hatumtaki.

Dr Mwale alifukuzwa kwa kusema ugonjwa wa zika upo, ndugulile alisema wazi kuwa malimao sio dawa ya virus na akafutwa kazi na akabeba briefcase yake akaenda nyumbani kwake,

Hivi kwa upuuzi ule wa kunywa matangawizi anajua watu wangapi wamekufa? Hivi hatukupata somo kwenye kikombe cha babu?
 
Wanawake ndivyo walivyo,wanapenda mipasho sana,si unaona wanavyojibizana huyu anatumia waandishi mwingine anatumia waumini ,katikati Kuna mchochezi Siro
 
Back
Top Bottom