Askofu Gwajima anamuonea Waziri Gwajima kijinga

Uwazir ni ajira, Kujiuzulu hapa kwetu ni ngumu kuliko ngamia kupita kwenye tundu la sindano. Lakini pia Ukijiuzulu kwa kumpinga mtawala kutaambatana na consequences. Unaweza kupotea au kung'olewa kucha.
 
Gwajike atalijua jiji!! Asubiri kutumbuliwa!! Hakuna namna nyingine!! Amefedhenesha serikali!! Hakuna njia nyingine ya kurejesha heshima ya serikali!! Kwa kadri anavyobaki ndivyo kadri serikali inavyochafuliwa!
 
Uwazir ni ajira, Kujiuzulu hapa kwetu ni ngumu kuliko ngamia kupita kwenye tundu la sindano. Lakini pia Ukijiuzulu kwa kumpinga mtawala kutaambatana na consequences. Unaweza kupotea au kung'olewa kucha.
Dr mwale na Dr ndugulile mbona hawajangolewa kucha? 2025 tunafukuza kichaa na kutupa makopo yake
 
Pochi ndio shetani mkubwa
Inaonekana mzee anauza utu wake kwa ajili ya hela
Kuna watu hawana aibu wala Soni likija suala la hela
Watu mnaongea ongea tu, imagine umezaa mtoto wako umemlea na kumkuza kisha mwanamke anaolewa kwenye familia yako anatoa amri kwamba naamrisha majeshi yote yamkamate mtoto wako, yampe kashi kashi...

Nyie hamjui kuzaa labda.
Hapo hata mm ningekuwa mzazi ningewaka.

Na baba wa watu alisema wazi kuwa yule mama analeta mtafaruku sana kwenye familia yake

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Hao ni watu wakubwa isitoshe wana impact kubwa katika jamii
Ni busara kukaa kimya na kuyamaliza wenyewe
Hapo inaonekana hakuna anaemzidi mwenzie kifikra
Mtu mwenye hekima hawezi kufanya hivyo kama hizi sarakasi wanazofanya hawa jamaa

Kwa kuwa hakuna wa kuwaambia ukweli basi tuwaache waparuane
 
Gwajike atalijua jiji!! Asubiri kutumbuliwa!! Hakuna namna nyingine!! Amefedhenesha serikali!! Hakuna njia nyingine ya kurejesha heshima ya serikali!! Kwa kadri anavyobaki ndivyo kadri serikali inavyochafuliwa!
Waziri hana hatia, anatakiwa kulindwa kwa nguvu zote maana chanjo ni matokeo ya mapendekezo ya tume ya Rais ya wanasayansi wetu. Hata kama Gwajike alikuwa anaamini nyungu ni dawa lakini tume ya Rais ya wanasayansi imekuja kupindua meza. Waziri Gwajima ni Nani hata aigomee tume ya Rais ya wanasayansi?

Kuchanja ni hiari, ni kosa kubwa Askofu Gwajima kuwalazimisha kwa nguvu watanzania wanaosali kanisani kwake wafuate hiari yake yeye ya kukataa chanjo. Hii ni hatari sana kwa taifa na serikali tawala, maana haijulikani kesho atawakataza nini tena. Iko siku sheikh nae atawakataza waumini wake msikitini wasilipe Kodi kwakuwa tayari wameshalipa zaka kutoka kwenye vipato vyao halali.

Kila mtu atue hiari yake bila kulazimisha kwa kutumia hila za dini
 
Askofu haonei wala hadhalilishi mtu.
Dorothy ni mteule wa Rais, ni serikali, kumdhalilisha Rais na serikali yake kwa kanuni ileile ya kama A=B na B=C basi A=C pia. Hivyo kuna kila sababu ya kuamini kuwa Askofu hamlengi Dorothy bali Rais na serikali yake. Dorothy anatekeleza maagizo ya Rais yaliyotokana na wanasayansi kuhusu chanjo na covid-19.
 
Hapana. Sayansi ya ubora na usalama wa chanjo hizi vilijulikana wazi toka mwaka 2020 mwishoni. Kwa sababu tusizozijua ndipo Uongozi wa Tanzania ukapiga vita chanjo. Waziri Gwajima na wenzake walijua ubora na usalama wa chanjo wakati huo, lakini wakaendelea kuwadanganya watu kuwa ni mpango wa kuuwa Watanzania. Sasa wamegeuka nyuma kabisa na kuirudia sayansi. Ndiyo sababu ya watu wenye uelewa finyu, kama Mbunge Gwajima na watu wa kawaida mitaani, wanawakatalia, hawawaamini. Kama Waziri Gwajima, Naibu Waziri Mollel na yule profesa wa NIMR ndio wataendelea kuisemea chanjo haitakubalika kwa wengi. Hata wakiendelea na kazi zao, wasiisemee chanjo. Waje wengine wanaoelewa na kukubalika ndio waisemee.
 

Unazungumzia TFDA ipi?
Kwa sasa ipo TMDA, hakuna TFDA!
 
Yeye alipoagiza akamatwe na kuhojiwa na Majeshi yote yaani Takukuru,Polisi,usalama wa taifa,jeshi la wananchi.Hakuwa anamuonea raia?
 
Hivi huo mgogoro wa gwaji's family ungekuwa na TOZO,ingefikia hapa kweli..[emoji19][emoji19]..??
 
Hujamwelewa Mch. Gwajima hata kidogo...

Nakushauri usikilize tena maelezo yake kupitia mahubiri yake ya Jana tarehe 22/08/2021 J'pili....

Video yake ni ndefu kidogo (zaidi ya masaa 2 na dakika 30 lakini kama uñataka umpe fair judgement Mch. Gwajima, basi lazima umsikilize mwanzo hadi mwisho...

Lakini mpaka hapo ulipo, bila shaka hujamsikiliza Mch. Gwajima vyema. Inawezekana unachukua video clips fupi fupi zilizokatwa na kupostiwa ili ku - suit interests za anayeposti na wewe kutumia unusu nusu Wa taarifa za namna hiyo kutoa judgement...

Kama unafanya hivyo, basi hilo ni kosa kwa sababu utaishia kutoa hukumu isiyo haki...
 
He, tunahitaji msemaji anaekubalika ili utumie dawa ya mseto kutibu malaria yako? Waziri Gwajima sioni kosa lake hapa kwakuwa anatekeleza mamlaka za uteuzi. Engekuwa mimi ndio Rais nisingembadilisha
 
Anaesengenywa hasemwi hadharani au hujui maana ya kusengenya?

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
Pale ni kanisani sio hadharani, wanaingia kundi fulani TU. Anaesengenywa mara zote ni mtu ambae hayuko
Laana ya kupokonya ubunge Kawe
 
Mnashindwa kutofautisha Kati ya mkamwana na Waziri wa nchi. Hata akili ndogo kama hiyo hamna? Mwanao akiwa Rais huwezi kwenda kumuona utakavyo kwakuwa wewe ni baba. Askofu Gwajima hajui kama Dorothy ni zaidi ya Mke? Hajui kwamba Dorothy ni serikali? Hajui kama Dorothy anavyombo vya dola vinavyomtii kwa mujibu wa katiba?
 
Yeye alipoagiza akamatwe na kuhojiwa na Majeshi yote yaani Takukuru,Polisi,usalama wa taifa,jeshi la wananchi.Hakuwa anamuonea raia?
Ni maagizo ya Amirijeshi mkuu. Anaposema wamehongwa kukubali chanjo anamaanisha Rais wa nchi ndiye amehongwa na sio Waziri wa nchi. Rais ni Amirijeshi, anamiliki majeshi yote, hivyo anaweza kuyaamuru majeshi yote yashiriki kukabiliana na nguvu za Gwajima boy. Askofu peke yake hana uwezo wa kuitindia serikali kiasi hiki, lazima Kuna watu nyuma yake. Kunguru Hana kibyongo.
 
Ubunge hauwezi kusimamishwa
 
Ajabu ipi Kikwete aliwahi kutuhumiwa kuhongwa suti.
Waziri Hana mamlaka hayo ndo maana Siro akampa somo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…