Hapana. Sayansi ya ubora na usalama wa chanjo hizi vilijulikana wazi toka mwaka 2020 mwishoni. Kwa sababu tusizozijua ndipo Uongozi wa Tanzania ukapiga vita chanjo. Waziri Gwajima na wenzake walijua ubora na usalama wa chanjo wakati huo, lakini wakaendelea kuwadanganya watu kuwa ni mpango wa kuuwa Watanzania. Sasa wamegeuka nyuma kabisa na kuirudia sayansi. Ndiyo sababu ya watu wenye uelewa finyu, kama Mbunge Gwajima na watu wa kawaida mitaani, wanawakatalia, hawawaamini. Kama Waziri Gwajima, Naibu Waziri Mollel na yule profesa wa NIMR ndio wataendelea kuisemea chanjo haitakubalika kwa wengi. Hata wakiendelea na kazi zao, wasiisemee chanjo. Waje wengine wanaoelewa na kukubalika ndio waisemee.