Askofu Gwajima anatofautishaje mapato ya sadaka na matumizi ya kufanya siasa?

Askofu Gwajima anatofautishaje mapato ya sadaka na matumizi ya kufanya siasa?

Resilience

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2023
Posts
1,096
Reaction score
4,948
Nimeona Gwajima amekusanya vijana wa kumlinda na kushiriki naye kuzunguka jimbo la Kawe. Naamini hawa vijana wamepangisha nyumba, wanakula na pia wanayo matumizi mengine mengi.

Kwa mantiki hiyo hawa vijana wanalipwa na mlipaji maana yake ni Pastor Gwajima.

Lakini Gwajima chanzo chake cha mapato ni dini; na kwenye dini kipato ni sadaka, na sadaka kazi yake nikuendeleza kazi ya Mungu.

Lakini pia mifumo yetu inapingana kiimani kwa mtu anayetumia sadaka kuendesha mambo binafsi yasiyo ya kiroho ikiwemo kufadhili siasa.

Swali, Pastor Gwajima anawezaje kutuaminisha kwamba hatumii sadaka kufadhili shughuli zake za siasa?
 
Vilevile, anao mshahara na marupurupu ya ubunge. Hata hivyo, mwisho kabisa wa majadiliano, kanisa linabaki kuwa ni la kwake. Hivyo basi, mmliki wa kanisa na sadaka ni yuleyule mtu mmoja. Unataka nani awe na maamuzi ya matumizi?
 
Kwani wewe ktk kipato chako.

Umewezaje kutenga kwamba, pesa hii ni ada ya watoto, hii ni Kwa ajili ya CHAKULA, hii mavazi, hii ni rent, na hii ni SADAKA?

Gwajima ana mshahara, na marupurupu, matumizi ya kipato chake apanga mwenyewe!!

Pia usiye muumini waezaje hoji matumizi ikiwa wewe Si mmoja wa waumini?

Na kama ni muumini, kwann usihoji Kanisani, huoni kuwa kuhoji hayo jukwaa la siasa ni kuchanganya SADAKA na KODI ya kaisari?
 
Kama hujamsaidia Kutafuta usimpangie kutumia mkuu.Unadhani kupiga Hela ya sadaka ni rahisi?Kwanza lazima upate kondoo
 
Back
Top Bottom