Nashangaa sana kuona wale wanaoitwa waumini wa Gwajima wakijiinua inua kutoka vitini huku wanaitika Haleluya pale mchungaji wao bwana Gwajima anapowapigisha stori za kijinga na kuwapotezea muda wao.
Gwajima anaongea mambo ya uongo, yasiyo na ushahidi na mbaya zaidi anayapeleka madhabahuni na anahubiria watu. Siwezi kumtofautisha mtu huyu na muhuni wa kijiweni!
Kuongea mambo ya uongo eti umetumiwa video za watu waliochoreka namba 666 kwenye mabega yao baada ya kuchanjwa huko Marekani na unayo huku ukiwa huionyeshi naachaje kikufananisha na muhuni tuu wa kijiweni? Huyu eti ni mbunge! Mbunge?
Kusema watu wanaochanjwa ni free Mason sijui nini, hivi umewahi kuuliza kilichowaua viongozi ambao unawaita mashujaa eti waliishinda Corona? Au unakaa tu kuwadanganya watu wako upuuzi.
Hivi hao wazungu kwani wameanza kuchanja waafrika na wao wakajitenga na chanjo? Si wameanza wao kujichanja ili waondokane na vifo holela? Sisi waafrika si tumeletewa baadaye kabisa? Emb acha uhuni na usiwapotoshe watu wako kwa ujinga wako bwana Gwajima!
G Sam, kama ulikuwa hujui, naomba nikufahamishe jambo hili, kuwa,
Mimi na wewe ktk kujadili siasa za nchi yetu ya Tanzania tunakubaliana na kusomeka kwenye ukurasa mmoja (same page) katika mambo mengi...
Ila kwa hili UMETUTUKANA na KUTUDHARAU kwa kiwango cha juu sana washirika na waumini wote wa kanisa la Ufufuo na Uzima chini ya uongozi wa Mchungaji na Askofu Dr. Josephat Gwajima...
Umetuita "wajinga" kwa kudhani kuwa kiongozi wetu anatupigisha story za kijinga kijinga kanisani huku tukijiinua kwenye viti vyetu na kusema "hallelujah" kama mapoyoyo...
Nakuhakikishia kuwa, sisi siyo wajinga. Sisi siyo wapumbavu. Sisi tuna ufahamu na akili zetu timamu. Tunajua tutokako na tuendako. Tunaweka kila neno la kiongozi wetu au muhubiri wetu katika kipimo ambacho ni NENO LA MUNGU. Tunapima lolote lisemwalo kama linapatana na Neno la Mungu, basi tunaliamini na kulitenda sawia. Niyo maana tuko hivi tulivyo leo. Tunafanya kama waluvyofanya Waberoya...!!
Hebu nikuulize swali hili. Hivi ukinisoma na kunitazama mimi hapa nilipo, unaniona katika sura ya ujinga na upumbàvu siyo...?
Kama jibu lako ni NDIYO, basi pole sana becausr...you are totally wrong...!!
G Sam, kwa hili ni bora ungenyamaza na ukaenda zako kuchanjwa salama kwa hiari yako wewe na watoto wako na ndugu zako kwa sababu JAMBO USILOLIJUA KUTUHUSU SISI, BASI HILO NI NI SAWA NA USIKU WA GIZA KWAKO...!!
Ndiyo. Kwani ni wazi kuwa hujui lolote juu ya Biblia [Neno la Mungu]. Na ni wazi kuwa, unaamini sayansi zaidi [maarifa ya kibinadamu] kuliko Neno lake linaloizaa hiyo Sayansi. Sina shida na hili...
Lakini, unapata wapi ujasiri kututukana sisi tusioamini ktk akili, mawazo na maarifa ya kibinadamu yenye mwisho na mipaka ya ukomo..?
Anyway. Mimi nakusamehe bure kabisa kwa sababu hata katika kizazi cha Yesu Kristo miaka zaidi ya 2000 iliyopita, wasio na ufahamu wa kiroho, wasio na imani kama wewe walikuwepo na walimwita Yesu Kristo mwongo, ana mapepo na hajui sayansi na anapotosha watu kwa ujinga wake...
Mwisho wa siku wakidhani kuwa wanaondoa kikwazo na kumaliza matatizo yao, walimshitaki na kumhukumu adhabu ya kifo msalabani si kwa yale aliyokuwa anatenda na kuyasema bali kwa kumtengenezea kesi ya makosa ya kubumba, ya uongo tu ili mradi kuridhisha nafsi na tamaa zao za kimwili...!
Mwisho ulikuwaje?
Kifo hakikuweza kumshinda. Alikishinda kifo na leo YU HAI na waliomhukumu waliaibika wenyewe na kukosa mahali pa kuficha nyuso zao kwa aibu ya uongo wao...
Asante..