Biggs
JF-Expert Member
- May 3, 2014
- 2,068
- 2,314
Hakuhitaji kuyasema haya kama ni kweli amesema hivyo maana si ilishatangazwa ya kuwa Chanjo ni Hiyari !!Askofu Gwajima amesema vikao vya kamati za bunge vinaanza kesho na yeye atakuwepo Dodoma lakini hatachanja chanjo ya Corona
Gwajima amesema ubunge ni kazi ya heshima na anawashukuru sana wana Kawe kwa kumchagua kuwa mbunge wao lakini kuchanja hapana hata kama itamlazimu kupoteza ubunge wake
"Nitarudi hapa nyumbani kuwatumikia' askofu Gwajima amewaambia waumini wa kanisa lake.
Nawatakia Dominica yenye baraka!