Askofu Gwajima kada wa chama aliyeamua kujihatarisha kuokoa nchi yake

Askofu Gwajima kada wa chama aliyeamua kujihatarisha kuokoa nchi yake

mzeekazi_

New Member
Joined
Apr 21, 2025
Posts
3
Reaction score
7
GWAJIMA KADA WA CHAMA ALIYEAMUA KUJIHATARISHA KUOKOA NCHI YAKE

Askofu Gwajima siku ya jana alitoa ushauri kwa mamlaka za kiserikali kutokana na sakata la utekaji lililozidi sana nchini kwa sasa. Katika hotuba yake ya lisaa limoja, Askofu Gwajima amenukuliwa akisema utekaji sio utamaduni wetu kama watanzania huku akionesha athari zake pia kwenye diplomasia ya uchumi na biashara katika nchi yetu.

Maneno ya Askofu Gwajima ni maneno mazito yaliyobeba moyo wazi wa mtu anayeipenda nchi yake na sio tu kuipenda, kuwa tayari kujihatarisha kwa ajili ya watanzania. Haya ni maneno ambayo wengi wanayajua lakini huyasema na wake zao chumbani kwa kuhofia madhara yake.

Mtu wa kuyaongea maneno yaliyonyooka kwa kiwango hiki na anaishi nchini na anategemea kuendelea kuwepo na kufanya shughuli zake, ni ujasiri, upendo na ni kiwango cha juu cha kuonesha upendo na uthamani wa maisha ya watu.

Kada huyu wa Chama cha Mapinduzi amekuwa kimya kwa muda mrefu huku wengi tukiwa tunajiuliza kulikoni kwa mtu mpenda haki kunyamaza kwa kipindi kama hiki. Kada huyu ambaye ni mbunge wa Kawe, MNEC na kiongozi wa dhehebu ameweka haya yote rehani kwa ajili ya kuliokoa taifa ambalo linaonekana kuelekeza pua yake kwenye poromoko refu.

Tuseme wazi, Askofu Gwajima tuna deni kubwa ambalo kama wapenda haki umetuwekea na tunapaswa kulilipa. Jambo la kwanza tupuuze hizi kauli ambazo wengi kwasababu ya kulinda nyadhifa zao watajaribu kuzileta huku wakibeza hoja nzito iliyowekwa mezani.

Askofu Gwajima amekanusha CCM kuhusika na utekaji huku akisema hategemei mwana CCM kutoka na kumshambulia. Sisi pia tunasubiri atakayemshambulia huyu shujaa aliyejihatarisha kupaza sauti ili nasi tumdai ndugu zetu ambao tulitamani hata tusikie kauli zao za mwisho wakituaga kwamba hatutaonana tena.

Swala na wakuu wa vyombo kutokuwa huru kufanya kazi yake ni hoja ambayo inahitaji akili za kutosha kuielewa. Pamoja na hayo wakuu wa vyombo wameelewa na wameona dalili za moshi mweupe katika utendaji wa kazi pasipo kukanyaga taaluma zao.

Tuzidi kumwombea Mheshimiwa Gwajima aendelee na moyo wake huo huku nikinukuu maneno yake kuwa "Atakayenijibu au kujaribu kunirukia nitarudi tena na zamu hii nitakuja kwa namna nzito zaidi". Hii inatia moyo sana kwa mtu aliye ndani ya chama kuwa na kauli iliyonyooka namna hii.

Mwisho niseme, Firauni aliposikia ushauri wa Yusufu kuhusu njaa itakayoipata nchi ya Misri na dunia yote akasema TUPATE WAPI MTU KAMA HUYU? Mtu akinijibu, nitarudi kufafanua na zamu hii nitaandikia sio wino.

Mtakatifu Yuda Thadei
Utuombee
 
Gwajima akiamua kukinukisha, hakuna wa kumshinda. Na kama kuna mtu haamini hiki nilicho kisema, basi amuulize BASHITE.
 
At least kwenye hili tunajiona hatupo peke yetu tunapata watu wakututia moyo
 
Gwajima akiamua kukinukisha, hakuna wa kumshinda. Na kama kuna mtu haamini hiki nilicho kisema, basi amuulize BASHITE.
Usimchongee, omba maneno yake ya busara na ya wazi na mazito, mkuu ayatilie maanani, na aagize vitendo hivyo visiendelee, aidha mwenyewe avikemee angalau tuone vinamshtuka vitendo vinavyo wakuta wanadamu, akiwa na wajibu wa kuwalinda!
 
Back
Top Bottom