Askofu Gwajima na Jerry Silaa waitwa kwenye Kamati ya Bunge kujieleza kwa kusema uongo na kushusha hadhi ya Bunge

Askofu Gwajima na Jerry Silaa waitwa kwenye Kamati ya Bunge kujieleza kwa kusema uongo na kushusha hadhi ya Bunge

msovero

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2019
Posts
863
Reaction score
1,534
Spika wa Bunge amewaita Mbunge Josephat Gwajima na Jerry Slaa mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya bunge

Wanatakiwa kujibu tuhuma mbalimbali ikiwemo kusema uongo na kushusha hadhi na heshima ya bunge

Gwajima ametakiwa afike Dodoma Agosti 23 saa saba mchana, Slaa ametakiwa afike Agosti 24 Saa saba mchana

cloudstv-20210821-0001.jpg


Mbunge wa Kawe (CCM), Josephat Gwajima pamoja na Mbunge wa Ukonga (CCM) Jelly Silaa wameitwa mbele ya Kamati ya Maadili na Madaraka ya Bunge ili kujibu tuhuma mbalimbali ikiwemo kusema uongo na kushusha hadhi na heshima ya Bunge.

Taarifa iliyotolewa leo Jumamosi Agosti 21, 2021 na Kitengo cha Mawasiliano Ofisi ya Bunge, imeeleza wabunge hao wameitwa mbele ya Kamati hiyo kwa agizo la Spika wa Bunge Job Ndugai.

“Wanatakiwa kufika mbele ya Kamati hiyo kwa mujibu wa kanuni ya 4 (1) (a) na (b) ya nyongeza ya nane ya Kanuni za Kudumu za Bunge, toleo la Juni 2020 ambayo inaipa mamlaka Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuchunguza mambo yanayohusu maadili ya wabunge yanayopelekwa na Spika” imesema taarifa hiyo.

Hata hivyo taarifa imeeleza kuwa, Mbunge Gwajima anatakiwa kufika kwenye Kamati hiyo siku ya Jumatatu Agosti 23, 2021 saa saba mchana na Mbunge Silaa anatakiwa kufika Jumanne Agosti 24 saa saba kamili mchana.

“Yeyote kati ya waliotajwa hatafika mbele ya Kamati kwa siku na muda uliotajwa hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake kwa mujibu wa kifungu cha 17 na 34 (1) (a) cha sheria ya Kinga, Haki na Madaraka ya Bunge, Sura ya 296, Toleo la mwaka 2020” imesema taarifa hiyo
 
Mh Spika kaamua anunue huu mtanange? Hakujifunza kitu kwenye bandari na ndege ATCL. Viongozi wetu wanaona taabu ya nini kusema kauli rahisi tu kama hii 'Mimi nimechanjwa chanjo ni hiari yako mwananchi'
 
jasusi la mbinguni limeanza kutikiswa soon litatikisika na kukongoroka kabisa
 
Kusema ukweli ni kushusha haadhi ya Bunge?

Kuwa na mtazamo tofauti na spika ni kuvunja haadhi ya Bunge?

JPM aliwahi itwa na Bunge kuonywa juu ya kauli zake kuwa chanjo hazifai? maana na yeye alikuwa sehemu ya Bunge.
 
Kusema ukweli ni kushusha haadhi ya Bunge?

Kuwa na mtazamo tofauti na sipika ni kuvunja haadhi ya Bunge?

JPM aliwahi itwa na Bunge kuonywa juu ya kauli zake kuwa chanjo hazifai?maana na yeye alikuwa sehemu ya Bunge.
Ndugai hakuwahi kwenda kinyume na JPM, ulitaka aitwe bungeni kufanya nini? kwanza Ndugai hana mamlaka hayo.
 
Kwa hadhi ipi sasa bunge lenyewe lilishajishushia hadhi kitambo kilichopo ni kikao tu cha wana CCM ndio maana linapitisha tozo za ajabu
 
Atleast Ndugai kwa nafasi yake anatenda, huyo mwenyekiti wa chama chao ndio hajielewi kabisa.mws
Mwambieni tu awafukuze Ubunge ndo ndo atajua kilichokunja mkia wa mbwa.
Yeye mwenyewe Kongwa alibebwa na JPM,leo kaanza mdomo ili tu kulinda kibarua chake.
 
Back
Top Bottom