Askofu Gwajima: Nchi ni lazima iwe na maono ya kimaendeleo kwa miaka mingi. Tunafanya mambo kwa kukimbia kimbia tu

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Mbunge wa Jimbo la Kawe, Askofu Josephat Gwajima, amesema kwa sasa Tanzania haina maono ya muda mrefu kwa ajili ya Maendeleo ya Wananchi bali kuna Ilani za Vyama na mipango ya muda mfupi.

Amefafanua kuwepo kwa maono ya muda mrefu kutasaidia hata kumpima Rais anapoingia Madarakani kwa namna ambavyo anayatekeleza maono yaliyowekwa ila kwasasa tunaona tunasogea lakini ni kwa maono ya kila Serikali mpya inapoingia Madarakani.

Ameongeza "Sasa hivi hatuna Vision bali tuna mambo ya kukimbiza. Kila Mwaka tunatafuta Madawati, kwani hakuna tawimu za kuonesha Mwaka huu tunahitaji Madawati mangapi kutokana na idadi ya Wanafunzi?"

Amesema hayo wakati akichangia mapendekezo yake katika makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa mwaka wa fedha 2021/2022.
 
Naamini Gwajima amejikita zaidi kwenye dini, ya dunia yakampita. Asome Dira ya maendeleo 2o25 (Development Vision 2025) ambayo ndio msahafu unaotumika kutengeneza Ilani za Uchaguzi za CCM, Chama Tawala, ambacho ndicho kimemwingiza Bungeni. Ni Dira hiyo hiyo inayotumika kuweka mikakati ya maendeleo km MKUKUTA, Kilimo Kwanza, MUKURABITA, nk
 
Unadhani hajui yote hayo? Nadhani lengo lake ilikuwa kutetea legacy
 
Gwajima yupo sahihi, huko CCM mmezoea kukimbia kimbia huku mnaimba mapambio mapya ya kila bosi wenu, akiwageuza kushoto mnageuka, akija mwingine akiwageuza nyuma mnageuka, hata hamjielewi, na taifa linadumaa sababu nyie ndio mmeshika hatamu.
 
Maskini, kwahio haelewi chochote? Tanzania tuna maandiko mazuri sana na takwimu nzuri sana hadi 2016 kabla ya kuharibiwa na Mwendazake, tatizo analijua kuwa tulikua na mtu mmoja alikua analazimisha kufanya anachotaka
 
Mbunge wa Jimbo la Kawe, Askofu Josephat Gwajima, amesema kwa sasa Tanzania haina maono ya muda mrefu kwa ajili ya Maendeleo ya Wananchi bali kuna Ilani za Vyama na mipango ya muda mfupi...
Huwa siamini sana anachokisema maana mara nyingi is too subjective to make a good judgement.
 
Mbunge wa Jimbo la Kawe, Askofu Josephat Gwajima, amesema kwa sasa Tanzania haina maono ya muda mrefu kwa ajili ya Maendeleo ya Wananchi bali kuna Ilani za Vyama na mipango ya muda mfupi...
Ndio anajua leo kuwa nchi haina malengo ya muda mrefu?

hii kitu kimepigiwa sana kelele na wapinzani wakaitwa si wazalendo. Saa hizi wabunge ndio kama wanaamka usingizini
 
Nimemuelewa Gwajima.

Lakini hata Kanisa lake sijaona kama lina maono ya muda mrefu!
 
Naamini Gwajima amejikita zaidi kwenye dini, ya dunia yakampita. Asome Dira ya maendeleo 2o25 (Development Vision 2025) ambayo ndio msahafu unaotumika kutengeneza Ilani za Uchaguzi za CCM, Chama Tawala, ambacho ndicho kimemwingiza Bungeni. Ni Dira hiyo hiyo inayotumika kuweka mikakati ya maendeleo km MKUKUTA, Kilimo Kwanza, MUKURABITA, nk
Miaka 2025 ni karibu sana, Tunakiwa kama nchi sio chama iwe na vision ya miaka 50 -100, na iwe inajulikana na more than 50% ya wananchi hii inasaidia mpaka familia kupanga maisha ya vizazi vyao vinavyokuja
 
Akili zimeanza kuwarudi wafuasi wa Kayafa sasa!
2021041105401.jpg
 
Chukua chako mapema imerudi upya kila kitu ni dili sahivi, nawashauri yyte alipo tuchukue vyetu mapema hari si hari asilani
 
Askofu ndiyo unaibuka leo baada ya sisi kumaliza kuzika - mbona ?
 
Yeye anajua maono na mipango ni kujenfa mabarabara na kununua ndege
 
Maskini, kwahio haelewi chochote? Tanzania tuna maandiko mazuri sana na takwimu nzuri sana hadi 2016 kabla ya kuharibiwa na Mwendazake, tatizo analijua kuwa tulikua na mtu mmoja alikua analazimisha kufanya anachotaka
Huyo mwendazake alijigeuza kuwa mshauri mkuu mambo yote hata yale yasiyoonekana,hebu eti fikiria alikuwa anaandaa mpango wa kuwaruhusu viongozi wa ccm kukemea na kutoa mapepo siku za wikiend
 
Unadhani hajui yote hayo? Nadhani lengo lake ilikuwa kutetea legacy

Gwajima yuko sahihi kuhusu dhana ya kukosekana kwa dira ya taifa. Kuwepo kwa document hiyo haimaanishi inafuatwa. Dira huenda na bujeti, ufuatiliaji wa utekelezaji na taarifa. Kilimo Kwanza iliishia wapi? Je kilimo kilitutoa? Big Results Now, iko wapi sasa?? Uchumi wa viwanda je, hata kusikia tu ikisemwa Bungeni haisikiki tena!! Tunaanzisha vitu au kwa kuwa ni vikubwa sana, au hatuna uwezo navyo, au ni propaganda za kura - hatufikii kuona mwisho mwema!!

Yawezekana nia ya yeye kuyasema hayo sasa ndio ina walakini. Natamani badala ya kuonekana anazungumzia tatizo, angepeleka mswada ili tuanze kuangalia upya jambo hili. Kutaja matatizo bila kuyshughulikia imekuwa ni tabia ya wanasiasa wengi!!
 
CCM wana matatizo makubwa... wanavyoongea utafikiri kuna chama kingine kimewahi kutawala nchi hii.
 
Huyo mwendazake alijigeuza kuwa mshauri mkuu mambo yote hata yale yasiyoonekana,hebu eti fikiria alikuwa anaandaa mpango wa kuwaruhusu viongozi wa ccm kukemea na kutoa mapepo siku za wikiend
Hii Kali
 
Back
Top Bottom