#COVID19 Askofu Gwajima ni bora uwe mpole tu uendelee na mambo yako lakini ukitaka kushindana na shemeji yako utaumbuka

#COVID19 Askofu Gwajima ni bora uwe mpole tu uendelee na mambo yako lakini ukitaka kushindana na shemeji yako utaumbuka

James Martin

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2016
Posts
1,206
Reaction score
1,509
Habari wana Jamìi Forum popote mlipo.

Nilitaka tu kumpa ushauri wa bure Askofu Gwajima kwasababu naona huko anakoelekea atakuja kujuta.

Nilianza kuona viashiria tangu wiki za nyuma baada ya watu mbalimbali kuanza kumuongelea Askofu kuhusu chanjo ya Uviko. Sasa nasikia waziri wa afya, Dk Dorothy Gwajima ameshaviandikia vyombo vya ulinzi na usalama vimuhoji Askofu Gwajima.

Huyu mama ni wale wanawake ngangari na Askofu Gwajima akiendelea kushindana naye ataingia cha kike.

Habari wana Jamìi Forum popote mlipo.

Nilitaka tu kumpa ushauri wa bure Askofu Gwajima kwasababu naona huko anakoelekea atakuja kujuta.
Alimshindwa Bashite na ungangari wake sasa huyu shemeji anamuweza?,IGP aliliona hili kwenye angle nyingine akaamua kulimaliza hili jambo kikubwa,sasa mpambeni bwana shemeji uone yatayotokea
View attachment 1899624
 
Safi sana Dorothy munyooshe huyo mpenda blah blah anayehadaa watu wa akili ndogo, hafu mzinifu utetezi wake eti mkono wa baunsa. Mheshimiwa Waziri mnyooshe huyo fyatu gwajiboy na atoe vidhibitisho vya kutaalamu
 
Mh Rais wakati anajaza nafasi ya Waziri wa Ulinzi afanye mini reshufle ya Baraza lake la Mawaziri. Hata kuwa hamisha baadhi wizara itasaidia kitu flani.
 
Habari wana Jamìi Forum popote mlipo.
Hatujambo, lakini niwahi kukujibu kuwa, hakuna majuto kwa Rev. Gwajima...!!
Nilitaka tu kumpa ushauri wa bure Askofu Gwajima kwasababu naona huko anakoelekea atakuja kujuta.

Hakuna majuto kwa Mch. Gwajima. Nakupa uhakika mmoja, nao ni huu, kuwa, kama waziri na naibu wake wataendelea kuwepo ktk nafasi zao hadi mwezi November, ni PM nikupe zawadi...
Nilianza kuona viashiria tangu wiki za nyuma baada ya watu mbalimbali kuanza kumuongelea Askofu kuhusu chanjo ya Uviko. Sasa nasikia waziri wa afya, Dk Dorothy Gwajima ameshaviandikia vyombo vya ulinzi na usalama vimuhoji Askofu Gwajima.

Kwani kuhojiwa ndiyo kuhukumiwa? Sikia ndugu, wataishia kumhoji tu lakini mwisho wa siku Waziri wenu huyu atapoteza uwaziri wake kabla ya mwaka huu kwisha...!!!
Huyu mama ni wale wanawake ngangari na Askofu Gwajima akiendelea kushindana naye ataingia cha kike.

View attachment 1899611
Eti nini? Mama ngangari?

Ugangari usio na akili ni ujinga na hauna maana...!

Wewe labda umesahau. Ngoja nikukumbushe;

Unalikumbuka sakata la Kadinali Polycap Pengo, waislamu na mahakama ya Kadhi dhidi ya Rev. Bishop Gwajima miaka 6 au 7 iliyopita...?

Walioitaka mahakama walimwona mchungaji huyu ni kikwazo kufikia malengo yao kama tu ilivyo leo wataka chanjo za UV-19 wanavyoona huyu bwana ndiyo tatizo na kikwazo chao ktk dhamira zao ovu...

Wakati huo, sheria haikuwa na nguvu kwake. Badala yake walidhamiria kum - eliminate kwa njia ya kifo cha sumu Rev. Gwajima na walifanikiwa kum - paralyze na kumfanya atembelee wheel chair for just some days...

Mwisho wa siku nani alishinda vita hiyo?

Ni Rev. Gwajima na tuliokuwa nyuma yake tukimuunga mkono maana;

å Sumu haikufua dafu kuuondoa uhai wake...

å Mungu alimwinua toka kwenye wheel chair na kusimama ktk afya yake tena na moto uleule hadi leo...

å Mahakama ya kadhi haikuanzishwa Tanzania kwa kutanbuliwa na katiba ya JMT..!!

Nakushangaa sana kusema leo eti Rev. Gwajima anaweza kuwa ktk vita na huyu mama mpuuzi asiyejielewa na mwenye ufahamu mdogo kabisa wa mambo...

Nakuhakikishia atapigwa mpaka atajisalimisha mwenyewe kwa Yesu Kristo...!!
 
Hiyo vita ipo kwenye level ya mawifi, gwajingo anaendelea na mishe zake.....
 
Baba Askofu Gwajima potezea tu,wakati mwingine mashindano hayatatui tatizo bali yanaongeza tatizo.
 
Habari wana Jamìi Forum popote mlipo.

Nilitaka tu kumpa ushauri wa bure Askofu Gwajima kwasababu naona huko anakoelekea atakuja kujuta.

Nilianza kuona viashiria tangu wiki za nyuma baada ya watu mbalimbali kuanza kumuongelea Askofu kuhusu chanjo ya Uviko. Sasa nasikia waziri wa afya, Dk Dorothy Gwajima ameshaviandikia vyombo vya ulinzi na usalama vimuhoji Askofu Gwajima.

Huyu mama ni wale wanawake ngangari na Askofu Gwajima akiendelea kushindana naye ataingia cha kike.

View attachment 1899611
Anayeumbuka ni shemeji mtu mwenye ndimi mbili
 
Mtu na shemeji yake kuna nini nyuma ya pazia??? au walishabanjuana au walinyimana? au kuna conflict zao binafsi. Haya mambo wangeweza kuyamaliza nyumbani.... lakini wanataka kuonyeshana msuli..... waacheni waendelee angalau tupate kucheka
 
Dorothy hamuwezi Rashid,atarukaruka tu lakini mwisho wa siku Chidboy ataibuka kidedea. Gwajima ana 'watu'.
 
Mpaka Sasa Gwaji fix 11
Dorothy 0 mechi ipo dakika 3 kipindi Cha kwanza subiri jumapili uone magoli kwenye nyavu utafikiri ni mpira wa rede 🔥🔥🔥🔥
 
Yangu macho lakini wabongo sijui tunasahau wapi hivi nyie Rashid mnamchkulia poa? Muda ukifika mtaona huyo shemeji chozi likimtoka
 
Huyu gwaji boy kuna namna huyu sio bure!!!!

Angekuwa mwepesi mwepesi tu tungeshampoteza kitambo!!!
 
Back
Top Bottom