#COVID19 Askofu Gwajima: Ni jambo baya sana kuwapa Chanjo ya Corona Wanajeshi, Polisi na watu wa Usalama

Umenena vyema mkuu
Huyu mtu ni mjinga kabisa tena he is fool maneno anayo sema unahisi kichwani kuna funza... lkn ukweli anajua kila kitu isipokuwa anatengeneza attention kwake ili aendele kuwa na wa waumini wengi. Unajua kama huja pata msiba wa ndugu au jamaa aliyefarika na CORONA unaweza kuleta masikhara sn kwenye jambo hili lkn kama umepata misiba huwezi kufanya masikhara hata kidogo.
 
Huyu Rashid anafilimbwa nini?
*Corona naifunga haitaingia Tanzania- ikaingia
* Siwezi kugombea ubunge, Urais -kagombea ubunge.
*Naizimisha corona haitakaa Tanzania- Imeua watu na bado iko.
Sasa huyu mbona ni kigeugeu kuliko watu wote nchini?
 
Kwa hio Gwajima ana maanisha kwamba Rais Samia ni kigeugeu. Ila yeye hajioni alivyo kigeugeu na alivyo muongo (Waumini wanasubiri ile treni aliowaahidi kununua).


Hongera zake Gwajima kwa kumrushia mawe SSH.
Miaka ya sabini Rais Nyerere alipoanzisha Sera ya vijiji vya ujamaa, kuna mbunge mmoja machachali alitoka hadhalani na kumpinga Mwl. Nyerere kuwa hiyo Sera haifai.
Mwl. Nyerere alikasirishwa sana na kitendo hicho cha mbunge huyo wa jimbo la Karagwe Mhe.Kaneno ambae kwa sasa ni marehemu.

Alimfuta uanachama wa TANU na hivyo akupoteza ubunge Moja kwa moja na ukaitishwa uchaguzi na akachaguliwa mbunge mwingine.

Sasa yetu macho, ngoje tuone huu mnyukano wenye viashiria vya uasi na uchochezi kati ya Mama na mbunge wa chama chake.
Muda utaongea na historia itahukumu.
 
Tunaambiwa tukachanje ila waziri mkuu, rais au makamu hawachanji tukawaona...
Tunaambiwa inakuja chanjo fulani kisha tunamuona waziri wa zamani anachanja chanjo ya urusi...

Kwani mtu yeyote kuchanjwa wewe inakuhusu nini? Chanjo si hiari?

Inasemekana vigogo wote wakiwamo kina Jobo walishachanjwa. Unavyowaona hawana pressure. Ile ni nguvu ya chanjo wala si nguvu ya buku.

Kwamba kuwaona wakichanjwa?Labda kama una maana wachanjwe kwa mara nyingine tena?
 

Kwenye mada, kauli ya serikali (inayowajibika na mustakabala wa afya zetu) kuhusiana na protokali za kushughulika na Ugonjwa huu umeiona?

Serikali inayowajibika ni ile inayotimiza kajukuu yake kwa mujibu wa protokali mbalimbali za kimataifa. Kauli ya serikali anayoibeza gwajima inavyo vigezo vyote vyenye kuendana na protokali hizo.

Kauli ya serikali inatokana na mapendekezo ya tume ya wataalamu wabobezi iliyokuwa imeundwa na SSH.

Kauli ya gwajima haina mashiko isiyokuwa na tofauti na kauli za kibwetere zilizopelekea msiba mkubwa.

Kauli ya gwajima inaelekea kule kule ilikoishia kauli ya kibwetere.
 
Elimu yetu Tanzania haijatutendea haki. Bado tu wajinga kupita kiasi. Sasa ona JF ambao tunaona wanauelewa kidogo lakini wanaakili kama au chini ya Gwajima. Inakuwaje hadi mtu anamaliza hadi form four hajui basics za chanjo?
Na kitu kimoja nimegundua, wajinga huwa paranoid sana. Kazi sana kureason nao.

Chanjo wandugu zipo za aina nyingi sana. Kuna chanjo ya Typhoid. Chanjo ya Typhoid kila baada ya miaka mitatu inaisha nguvu. Inatakiwa kuchoma kila baada ya miaka mitatu.
 
Uzuri wa corona inaweza kupita naye yeye mwenyewe
 
Huyu ni askofu wa wajinga tuu!
 
Uzuri wa corona inaweza kupita naye yeye mwenyewe
Tena naomba kwa MMUNGU nayeye impate ili ajue kuna mambo ya mchezo yakutafutia umaarufu na Majanga yaliyo kuwa serious hayataki masikhara .
 
Huyu bwana ni hatari sana kwa nchi hii sijui kwanini hata ameruhusiwa kugombea ubunge!
 
Samia naye ndiye wale wale. Karibu wiki sasa hajasikika sijui naye COVID-19 imeshamsarandia? Alifanya kosa kubwa kuwaacha Mawaziri wote wa dhalimu mwendazake. Sasa dharau zao kwake nje nje. Akiona yamenshinda abwage manyanga. Kwani hii vuta nikuvute ya timu Kikwete na timu mwendazake siyo kabisa.
 
Ujumbe uwafikie wanalumumba wote na kule Mwanakwerekwe
 
Kwamba?

"...na sio group la waswahili ni hao hao wazungu mnao waamini na kuwaabudu."

Madhara ya porojo za mwendazake.

😂😂😂!

Hiiiiii bagosha!
Ujinga wa aina hii, no wonder hili bara lina zaidi ya miaka 50 ya uhuru lakini zaidi ya asilimia 70 ya watu wake ni masikini wa kutupwa..akili kama hizi hizi
 
Wewe kilaza hata chanjo ya pepopunda huwa inarudiwa rudiwa, ukichanjwa mara moja haimaanishi hutapata kabisa pepopunda.
 
Bora kibwetere hakuwa kiongozi serikalini
 
Acha zako fanya mambo yako. Kwani wewe ndiye uliyempa huo ubunge. Kama alipewa ubunge na mtu mwingine mwache afanye anavyotaka yeye.
 
GWAJIMA ANAPAMBANA VITA NGUMU SANA NA MABEBERU NA MAKAMPUNI YAO MAKUBWA YA DAWA ANATAKIWA AONGEZEWE ULINZI ILI AENDELEE KUSEMA UKWELI WATANZANIA AMKENI CHANJO NI HATARI KURIKO KORONA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…