Njia zilizotumika kumpatia Ubunge anajua hazikuwa sahihi na haki haikutendeka lakini Leo hii hajawahi popote kuukataa ubunge wake Wala japo kuukubali lakini kutumia kanisa kukemea pale ambapo hakukuwa na haki
Amekywepo kwenye utawala wa awamu iliyopita ambapo tulishuhudia na kusikia watu wakipoteza uhai na kutekwa na watu wasiojulikana, tulishudia risasi adharani lakini hakuna siku amewahi kutoka adharani kukemea uvunjivu wa sheria na katiba ya nchi
Alikuwepo BUNGENI juzi wakati tozo kandamizi zinapitishwa hakuna siku tulimsikia akipinga na kura alipiga ya ndiyo. Hata hao waoumini wake hajawahi kuwaonea huruma, mshahara wake alipi Kodi na hatumsikii akikemea.
Leo anaibuka anaanza kumjadili JPM kwamba wakati wake hakuna aliyeleta chanjo. Je wakati wa JPM wakati watu wanabambikiwa kesi yeye hakuwepo? Alitusemea? Wakati watu wanakufa kwa corona alisema? Wakati tunaficha data alisema? Leo ametoa wapi ujasiri wakutumia nyumba za ibada kutaka kujifanya yeye ni daktari?
Tunaporuhusu watu wa aina ya Gwajima waongoze jamii ndipo tunapozalisha mawazo mgando. Yeye anaamini JPM alikuwa Mungu na kwamba maarifa ya JPM lazima yaheshimiwe hata Kama yalikuwa hayafai, kwamba Leo badala atueleze Mungu anasemaje anatulazimisha tufuate nyayo za binadamu ambaye ana mapungufu mengi ya wazi. Hii dini gani yakuelekeza watu wamwabudu mtu?
Leo ndipo amekuwa na msimamo, mbona huo msimamo upo kwa mambo ya mwendazake haupo kwa wengine?
Huyu mtu apuuzwe, siyo kiingozi wa dini Bali ni Kiongozi wa walafi wa madaraka. Kwenye siasa anataka, kwenye dini anataka na kwenye ushirikina anataka. Yeye Nani wakuombea watu wafe kisa awakubaliani naye? Unasiamama madhabauni unabiri kuua watu unadhani waumini wako wanajitunza Nini? Kwamba wanaokwenda kinyume na mtizamo wako na JPM wafe? Nani kakwambia ninyi ni miungu? Kwamba wewe utokufa?
Nadhani huyu mtu kwa kuwa tu Ni mwana ccm anayo haki yakutumia kanisa anavyojisikia yeye Tena kwa mambo ya hovyo kinyume kabisa na imani yake. Ila ipo siku ataadhibiwa