Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wewe na huyo Gwajima wenu hamko serious, kuna tofauti baina ya kupata corona ukafa na kupata lakini ukarecover na kuendelea na maisha. Kumbukeni lengo ni kuokoa maisha.Nyie mnaochangia bila kutumia akili ila kwa chuki zenu acheni ujinga hii nchi siyo ya mtu mmoja gwajima alichokisema ni sawa serikali itoke ije ijibu hoja ili wananchi tuikubal gwajima na mimi tupo tunauliza iyo chanjo mbona ata ukichanjwa na bado utapata korona je ni chanjo ya kuzuia nini hii?
Na kama inasaidia mbona bado naweza kupata iyo korona ? Sasa kuna umuuhimu gani wa kutumia na kuweka nguvu kwenye kitu ambacho hakisaidii?
Mie nishapiga dozi zote mbili (pfizer), na alhamdulilahi natype kukujibu.Acha kufoka hovyo, badala yake ujikite katika KUELEZA KUHUSU USALAMA WA CHANJO
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Mie nishapiga dozi zote mbili (pfizer), na alhamdulilahi natype kukujibu.
SUA.Ni wazo baya sana kuwachanja chanjo ya Corona askari wa majeshi yetu kwa sababu hatujui usalama wa hizo chanjo.
Baba Gwajima amesema anapinga kwa 100% vyombo vya dola kuchanjwa kwa sababu tunaweza kupoteza taifa. Askofu Gwajima amesema haya Kanisani kwake leo.
Askofu Gwajima amewataka wafuasi wake na wapiga kura wa jimbo la Kawe wakatae kabisa kuchanja kwa sababu watapata hasara kubwa sana maishani.
" Naikataa kabisa chanjo ya Corona " amesisitiza baba askofu.
Chanzo: Mtandao wa You tube!
======
Dar es Salaam. Wanasiasa, wananchi na viongozi wa dini wamemshukia Mbunge wa Kawe(CCM) ambaye pia ni Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima juu ya kauli yake kuwa daktari atakaye ‘shadadia’ suala la chanjo bila kufanya utafiti wa kina kujua madhara ya muda mrefu na mfupi atakufa.
Askofu Gwajima aliyasema hayo katika ibada ya Jumapili wakati akiwahubiria waumini wake huku akionyesha mashaka kuwa chanjo za Uingereza na Tanzania zinaweza kuwa hazina content sawa.
Kauli ya Askofu Gwajima imekuja ikiwa ni siku moja tangu Serikali ipokee msaada wa dozi 1,058,400 za chanjo ya corona zilizotolewa na nchi ya Marekani kupitia mpango wa Covax facility.
“Mmefanya uchambuzi wa kina kujua chemical content ya hiyo chanjo ni nini, mimi namtaka daktari atakayeshadadia nitakula naye meza moja utakufa daktari, utakufa utaona.”
Kufuatia maneno yake watu mbalimbali wametoa maoni yao kupitia kipande chake cha video kinachosambaa mitandaoni huku wengi wao wakionekana kukemea kauli hiyo.
Mbunge wa Bumbuli, Januari Makamba kupitia ukurasa wake wa Twitter aliandika “Kauli ya Askofu Gwajima kuhusu chanjo na dhamira ya Serikali kuleta chanjo nchini haikubaliki. Ni hatari kupotosha watu wanaotuamini kuhusu mambo ambayo hatuna utaalam nayo,”
“Mjadala kuhusu usalama wa chanjo ni sahihi lakini kiapo kwamba Serikali imeileta kuwadhuru watu si sahihi.” aliandika
Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT na Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Tanzania (CCT), Dk Fredrick Shoo amehimiza wananchi kuendelea kujikinga na wimbi la tatu la corona na kusisitiza kuendelea na maombi ya kufunga na kutubu, ili kujinusuru na janga hilo.
“Nawaonya viongozi wa dini kuacha kuhusisha suala la chanjo ya Covid 19 na mpango wa shetani kwani huko ni kumjaribu Mungu,” alisema.
Solomon Franco @mamgunda1 kupitia ukurasa wake wa twitter aliandika “Huyu hana elimu ya utabibu lakini ndio anaongoza kupotosha watu,”
Aliyekuwa Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa aliiomba Serikali imchukulie hatua Askofu Gwajima kwa sababu atasababisha watanzania wengi wafe kwa mafundisho yanayopotosha
“Hana scientific evidence kwa vitu anavyozungumza, hajui mambo ya kitatibu na siyo mtabibu, ningemshauri na nimsihi aheshimu taaluma za watu, akawasikiliza wataaluma,”
“Pia kitendo cha kusema wanaopigia chapuo madawa haya wamepewa pesa anamaanisha anamtuhumu hata Rais ambaye pia ni mwenyekiti wa chama chake, hivyo ni vyema achukuliwe hatua,” alisema.
Chama Cha Mapinduzi(CCM) kimesema kinafutilia kwa makini mienendo ya baadhi viongozi wake ambao wamekuwa wakipotosha umma na kwenda kinyume na maelekezo ya Mwenyekiti wa CCM na Rais Samia Suluhu na maadili ya chama.
Taarifa iliyotolewa leo na CCM, Katibu wa Halmshauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka inawakikishia wanachama na Watanzania kuwa hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa dhidi ya wote ambao wanatumia nafasi iyo kusukuma ajenda zao binafsi, kwa mujibu wa Katiba, kanuni za maadili na uongozi za CCM
Chanzo: Mwananchi
View attachment 1869726
MrFrosty i salute your common sense,you are gentleman and a scholar!.Wewe na huyo Gwajima wenu hamko serious, kuna tofauti baina ya kupata corona ukafa na kupata lakini ukarecover na kuendelea na maisha. Kumbukeni lengo ni kuokoa maisha.
Takwimu zinasema mtu mwenye afya yake na kijana mbichi (no medical conditions kama diabeters etc) ni 1 / 10 anashindwa kurecover au anakuwa na dificulties katika kurecover.
Takwimu hii ndio ilionifanya nikubali kupiga vacine, sijawahi kupata corona wala sina complications zozote za kiafya. Lakini kama kila kwenye vijana 10 mmoja anashindwa kurecover, I simply wont take the chance!
Upande wa shilingi waliochoma vacine na kupata corona wakapoteza maisha, ni mdogo. Nashauri wengi wakatafakari kwa kutumia takwimu. Duniani ni watu wengi washachoma dozi zote mbili personally pia nishamaliza dozi zote 2. Takwimu hazidanganyi acheni ujuaji usio na kichwa wala miguu.
Na kaamua kutumia mbinu mbalimbali ili tusi-concentrate kuhusu filamu yake ila kiasi fulani kafanikiwa,mambo ya MUNGU na ngono wapi na wapi.Huyo jamaa alifaulu mno kuicheza ile filamu ya ngono kudadadeq! Alikata uno huku anatukania
Sijui kwa sasa ni nani anaweza kusimama na kukemea jambo na taifa likaheshimu. Nyerere aliweza japo kama angeweza kuwa na makosa.Pamoja na yote, tumepoteana zaidi tokea awamu ile. Tulipo ni kama tumemwagiwa petroli. Akitokea mvuta sigara na moto wake karibu inaweza kuwa hatari kubwa.
Walioko madarakani walikuwa na dhamana kubwa ya kuiondoa hali hii wala si kuipalilia.
Au nasema uongo ndugu zangu?
Sijui kwa sasa ni nani anaweza kusimama na kukemea jambo na taifa likaheshimu. Nyerere aliweza japo kama angeweza kuwa na makosa.
Kupoteana ni hatari sana. Dola ndilo linakemea sasa duh!
Askofu [emoji2]Na kaamua kutumia mbinu mbalimbali ili tusi-concentrate kuhusu filamu yake ila kiasi fulani kafanikiwa,mambo ya MUNGU na ngono wapi na wapi.