#COVID19 Askofu Gwajima: Ni jambo baya sana kuwapa Chanjo ya Corona Wanajeshi, Polisi na watu wa Usalama

#COVID19 Askofu Gwajima: Ni jambo baya sana kuwapa Chanjo ya Corona Wanajeshi, Polisi na watu wa Usalama

Sio Gwajima tu na walokole uchwara wengine na makanisa yao ya ajabuajabu .
 
Wewe kilaza hata chanjo ya pepopunda huwa inarudiwa rudiwa, ukichanjwa mara moja haimaanishi hutapata kabisa pepopunda.
Mimi Na wewe nani Kilaza
Chanjo ya pepopunda Kama ulicho mara mbili au zaidi ni wewe nahisi utakuwa wewe ni uzao wa shetan aliyevaa sura ya binadamu.
Dawa zenu zipo kuzimu ambao unatikiwa uende kila wakati kila mara kuongezewa nguvu.

kizazi cha Nyoka aliyepata nafasi kuvaa sura ya binadamu
 
Huyu alishindwa kujibu swali wakati wa kampeni kuhusu sukari haya mambo ya chanjo ataweza kuyatolea ufafanuzi?

I think he is an overrated lunatic
 
Ngoja nikuoneshe jinsi ulivyo naive......

nime quote baadhi ya maneno yako kama ifuatavyo...........uliandika hivi "Serikali ndio inayofanya kazi ya kujua kipi ni salama kwa wananchi wake, kama serikali na vyombo husika vikisema kitu ni salama, serikali za nchi nyingine zikasema ni salama, taasisi nyingine za kimataifa zikasema ni salama then who are you kupinga bila evidence ?"

Sasa naomba ukachukue kasha la kuhifadhia sigara yoyote iliyotengenezwa hapa Tanzania,utaona kuna maandishi makubwa yanasema "UVUTAJI WA SIGARA NI HATARI KWA AFYA YAKO",halafu pembeni ya kasha hilo kuna nembo ya TBS imepigwa hapo juu ya kasha,

Je,unaweza kunieleza kwanini TBS wamekubali kuthibitisha matumizi ya kitu ambacho hata aliyekitengeneza anakubali kwamba ni hatari kwa matumizi?

Nimekupa evidence kama ulivyotaka,maana najua utauliza evidence,sasa kafanye kama nilivyokwambia ili wewe mwenyewe ujionee hiyo evidence,ukishafanya hivyo rudi tena hapa niite nikupe elimu labda naweza kukuokoa na ujinga ambao unaweza kukusababishia madhara makubwa kwako au kwa uwapendao sasa au baadaye.
Unaelewa maana na dhumuni ya chapa ya TBS katika sigara ? Ni kuonyesha imekidhi kiwango cha ubora wa kuitwa sigara unaokubalika kimataifa huo ubora unaanzia inapohifadhiwa, inapoandaliwa mpaka kumfikia mtumiaji na kutokana na mvutano uliopo kimataifa matangazo yote ya sigara na hata makasha ya sigara yanahitaji kuwa na onyo ili kujaribu kupunguza ongezeko la watumiaji wa sigara bila kuingilia uhuru wa wale ambao watataka kuitumia pamoja na kujua athari yake, hiyo ni kwa mujibu wa Sheria ya Matumizi ya bidhaa za Tumbaku Tanzania. Hata matangazo ya sigara yanatakiwa kulenga kuwafikia watumiaji waliopo na sio kushawishi watumiaji wapya, ambapo mpaka leo hii ni tatizo kwa maana bado kuna watumiaji wapya wanashawishiwa, hata mahali pa kuweka hayo matangazo pametajwa na sheria hiyo hiyo.

Bado ni serikali hiyo hiyo inadhumuni la kushawishi watu kuacha matumizi ya sigara na ndio imefanya hatua kubwa kujulisha watu kuwa uvutaji sigara ni hatari.

Nachotaka unipe evidence kwamba chanjo X ya corona inamadhara Y kuliko faida Z ...na hiyo evidence uonyeshe takwimu za taifiti uliyofanya ama takwimu za wanasayansi wengine...vinginevyo ni kelele tu utakuwa unapiga !
 
Wewe nani kakwambia hiari watumishi wa afya usipochanjwa unawez,akupoteza ajira watuminshi wengi wanaweza kuacha kazi kwa sababu ya chanjo

Hawapo watumishi wa afya wanaopinga uwepo wa Corona na tahadhari zake zikiwamo matumizi ya chanjo. Kwa utangulizi huo, hayupo mtumishi wa afya asiyetaka chanjo

Kama wapo basi watakuwa mbona walisha pumzika kwa amani muda mrefu? Hospitali tena? Alikotimua ubio SSH?

IMG_20210720_114420_251.jpg


Mkuu hospitali ndiko kuliko na karakana pendwa za yule mwana wa Wuhan.

Yaani ndiyo yaliko mazingira yako ya kazi halafu usikilize porojo za gwajima?

Labda kama unataka kuimbiwa .. "parapanda italia" kabla ya habari yenyewe.

😂😂😂😂!

Hiiii bagosha!
 
Ho
Hoja iko wapi? Umekosa hoja unakimbilia kwenye uanachama wangu humu JF! Hiyo tarehe isikusumbue wengine tumo humu tangu enzi za akina Kichwa Mbovu na akina Magazine! Sijui wewe ulikuwa wapi mida hiyo. Humu JF unaweza kuingia na kutoka kadri upendavyo kwa Avatar yoyote tu. Sasa lete hoja kama unavyo on the subject in question!
 
Ccm mnapenda sana watu wazinzi so mvumilieni gwajiboy mzinifu na mla kondoo
 
Kazi kubwa ya propaganda ni kuibadili akili timamu ya mtu ili aweze kuamini zaidi anachoambiwa na mtu mwingine kuliko kile anachokiona yeye mwenyewe.

Hivi ile ripoti ya kujua kwanini sample kutoka kwa mbuzi,papai nk zilitoa majibu positive baada kupimwa covid19 ilishatolewa eenh?Naombeni kujuzwa tafadhali...

Nadhani nitakua nimeeleweka hata kama aliyenielewa hatasema waziwazi.
Hiyo propaganda ilipigwa kipindi hicho ambapo huo uchunguzi ulikuwa mufilisi mashine iliyowekewa mfumo wa kuangalia kama kuna viashiria vya corona au la kwenye mwili wa binadamu italeta majibu yasiyo sahihi kama ukiipa mapapi, mbuzi na oili chafu...hilo jambo lilielezwa na wataalamu waliopigwa mawe na hiyo ripoti haiwezi kutolewa kwa sababu itamchafua Rais kwa hiyo ni funika kombwe mwanaharamu apite.

Jiulize tunaambiwa tuliishinda corona kwa sala na maombi tu halafu baadaye tukaanza kusikia vifo vya nimonia vilvyofuatana kwa haraka mpaka baadaye tukaanza kuambiwa sijui watu waliochanja wameleta corona ya ajabu ajabu, mara wakaanza kujitetea kwamba tuna muingiliano na watu wa mataifa mengine kwa hiyo tunaweza kupata corona, tulijaribu kupingana na uelekeo wa dunia kwa propaganda kuwa hatuna corona na mwisho wake ulikuaje ?
 
Mbunge wa Kawe mh Gwajima amesema hata ikilazimika abaki peke yake akiyatetea maisha ya watanzania atafanya hivyo na kamwe hatatetereka.

Kati ya mtume Simon Petro aliyemkana Yesu na Yuda Iskarioti aliyemsaliti Yesu, ni yupi mwenye dhambi iliyo kuu zaidi? - Kardinali Pengo

Mungu ni mwema wakati wote!
 
Anachokiongoza au Imani yake nadhani havituhusu..., Lakini matamshi yake kama yanavuka mipaka ya kiimani na kupotosha watu bila kuwa uhakika wa kutosha (kwa kutumia mgongo wa Dini) Nadhani hapo anavunja Sheria na Kukosa Ustaarabu...

Kama anaingilia mambo ya kitaalamu na kufanya kazi ya wataaluma kuwa ngumu hatendi haki sababu hao wataaluma pia wangeweza ku-question hizo porojo zake na kuzuia watu wasiende kumchangia sadaka (tena kwa kutoa mifano hai) lakini nadhani kwa busara wamemuachia yeye na watu wake uhuru wa kiimani ingawa hapa anaelekea kwenye kutaka uhuru wa kutapeli na kudanganya

Mambo ya Kisayansi mbona ni rahisi tu..., njoo na vivid evidence ambazo zipo backed na research na experiments sio ambazo zipo backed na conspiracies na clips kutoka Youtube
 
Gwajina na Bunge la chama kimoja ni kama hadithi ya anakonda jike anapom'bugia anakonda dume mara tu apatapo ujauzito. Anakonda kwa Anakonda na maisha yanaendelea.
 
Ndugu, mwenye dhamana ya maisha yako ni wewe mwenyewe si serikali.

Umechukua maana finyu sana mkuu ya nilichoandika.

Kikamilifu nilimaanisha "kutokeapo majanga kama ilivyo kwa hili gonjwa, vita, uasi, matetemeko, dhoruba, mafuriko, na vya namna hiyo, anayewajibika na maisha yetu ni serikali. Si Gwajima."

Naona ulihitaji niandike na darasa la 2 wawemo kama walengwa 😂😂😂😂!

Tafadhali jiridhishe kuwa nimeweza kukidhi vigezo vyote kutokana mwongozo wako mkuu.

Hiiiiii bagosha!
 
Nashangaa serikali inalea taasisi za hovyo kabisa kama kanisa la Gwajima, amekuwa akitoa kauli za kuhatarisha amani ya nchi lakini anaachwa tu kana kwamba nchi haina sheria.

Huyu alisikika akitoa kauli kwamba aunde kundi la wasukuma ndani ya serikali, na ahamasishe wasukuma wawe kabila la kuitawala nchi hii, je, kanisa lake lina malengo ya ukabila? Sheria ya usajili wa makanisa inaruhusu hilo? Msajili wa makanisa yuko wapi kuchukua hatua!

Juzi juzi tu alisikika akikashifu uislamu, amekashifu viongozi,anafanya siasa kanisani na serikali inamwangalia, siasa za kibaguzi, za kichawi, zinazohatarisha amani ya nchi!

Leo anamkashifu Rais wa nchi, anakashifu serikali nzima, watu wako kimya! Serikali ifute kanisa hili, ukidharau mwiba,mguu huota tende

Kikanisa hichi cha mtu mmoja chenye watu wasiofika 5000 kiharibu amani na ustawi wa watu milioni 60? Hivi usajili wake ukifutwa kuna hata vumbi yao itaonekana?

Tunahitaji serikali iingie kazini kupambana na huyu muhaini, haikubaliki, hii nchi ina serikali, huyu muhuni mmoja asituharibie nchi

Rwanda wanawadhibiti wahuni kama hawa kwa maslahi ya nchi,nchi kwanza
 
Back
Top Bottom