#COVID19 Askofu Gwajima: Ni jambo baya sana kuwapa Chanjo ya Corona Wanajeshi, Polisi na watu wa Usalama

Wewe ni mpuuzi huna ujualo umeandika maelfu ya waliopata chanjo wanakufa lakini huna ushahidi wowote ule wa kuthibitisha ulichoandika kuhusu vifo hivyo. Nimekuonyesha ushahidi wa kwamba 99% ya wanaokufa ná Covid kwa sasa ni wale ambao hawajapata chanjo maana yake waliopata ná chanjo ná wanakufa ni 1% lakini bado unaleta UBISHI WAKO wa KIPUMBAVU usio na kichwa wala miguu. Wazushi kama wewe ni watu hatari sana ná hasara kubwa kwa Taifa.
Ukija humu kuandika uzushi wako bila kuwa ná chembe ya ushahidi ujue uongo wako hautavumiliwa. Kadanganye kwingine siyo humu.
 
Ndio umekaririshwa hivyo!? Kwa taarifa yako, wapo waliochanjwa wengi tu wamekufa kwa corona!
Hiyo siyo chanjo, ni majaribio ya human genetic engineering 😭!
 
Inasikitisha kiwango cha upotoshaji kuhusu Covid na chanjo yake, mleta mada fahamu kwamba mRNA sio concept mpya, ni maelekezo tu ya kuifundisha cell namna ya kutengeneza viral protein ambayo mwili utaitambua kama adui na kuweka kinga(immunity) Hata chanjo ambazo sio mRNA based, wanatumia kirusi halisi kinaingia kwenye cell kinazalisha mRNA then cycle inaendelea kma kawaida. Hapa ni kwamba wame-weza kusythesize mRNA bila kutumia kirusi chochote, hii ni medical breakthrough sio manyaunyau ya waafrika.

Mi sio daktari wala mtaalamu wa medicine but nimeamua kujielelimisha kwa kina tu out of interest nikaelewa ABCs zote, wenzetu wanatumia maarifa na utafiti usiku na mchana watatoa suluhisho la matatizo, waafrica kazi kulalamika tu, inasikitisha.
 
Hahahaaaa.... !
 
Haya tueleze Bwana Molecular Biologist hiyo mRNA inaingia vipi kwenye cytoplasm na kuungana na DNA.
Au ndiyo akina amfifiro????
 
Mkuu, pana wengine hukurupuka tu kupinga hoja bila tafakari. Toka mwanzo umesema HUPINGI hanjo ila si hizi za MRNA! Jamaa kakomaa tu na chanjo chanjo huyu hana tofauti na wanaotupigia kelele za CORONA kana kwamba kirusi hiki kimeanza 2019. Kirusi cha korona kipo duniani hapa miaka nendarudi ila sasa tunapigana na hiki cha CoVid19.
 
Wewe kwani unavaa mask kama urembo au unavaa ili kijikinga na ugonjwa? Kama hivyo ndivyo ipi maana ya kuchanjwa ficha ujinga wako basi ndugu yetu
 
Mburula hawawezi kuamini, kama watu walioambukizwa korona wakapona bado wanaweza kuambukizwa tena na kuugua ndani ya kipindi kifupi, hiyo chanjo itasaidia nini zaidi ya kujidunga sumu.....
 
ukimpeleka mahakamani askofu Gwagima anaweza kukushinda kiurahisi sana

1.Tangia chanjo zimetolewa nchini ,hakuna hata siku moja watu au wazazi walosaini consent form .sasa hii ya corona unaambiwa usaini consent form.na kama ile niliyoiona ikizunguka matandaoni ni ya kweli hata mimi siko tiari kuchoma sindano hiyo .Ati ......madhara yatakayoijiyokeza baada ya chanjo serikali isihussike ?? how and why?.Hili nitatizo kubwa kwa wasomi amabao wanajua research .serikali na CCM wawe makini kumjibu askofu Gwajima vinginevyo waweza kujikuta matatani.


2.Tutofautishe consent form ya kufanyiwa operesheni na ile niliyoiona mitandaoni kama kweli ilitolewa na serikali.inaleta mashaka.mashaka yamesababishwa

3.wanaopinga chanjo hii siyo Tanzania peke yake.Hata America wapo ndo maana mpaka sasa waliyochanjwa kule USA ni milioni 161 tu .sasa unaweza kuona acceptance bado ni ndogo sana

4.the vaccine is only 65% effective .sasa kwenye reseach sijajuja kama hii ni statistically significant.

5.we have passed through phase one and two without vaccine .yes people died.but what about this phase 3.People who are against this vaccine have passed through phase one and two .so to me they may have right to go against this RNA vaccine

6.tumeruhusu uhuru wa kuongea .sasa tuyaogelee .the consequences ndiyo hizooo
 
GWAJIMA ANAWASIWASI NA CHANJO YA CORONA TUU! LABDA NI KWA UJINGA WAKE AU KAAMUA KUIPINGA SERIKALI KWA UJEURI TUU.

Kwa Mkono wa, Robert Heriel.

Nimeiona Clip inayomuonyesha Ndugu Gwajima akitoa maoni yake Kanisani kwake kuhusu Masuala ya Chanjo ya Corona.

Katika Hotuba yake hiyo, Gwajima alitoa maudhui yaliyolenga kuwashawishi waumini na wasikilizaji wake kuwa wasikubali Chanjo ya Corona mpaka pale Madaktari wa kitanzania watakapo fanya uchunguzi wa contents akimaanisha Gradients au Chemical composition zilizopo kwenye Chanjo hiyo.

Kauli za Gwajima mbali na kushawishi waumini wake na waliokuwa wakimsikiliza, pia zililenga kutishia na kuwaogopesha baadhi ya watendaji katika sekta ya Afya, Kwa kuwataja Madaktari watakaohusika kuipitisha chanjo hiyo.
Gwajima alitoa kauli ambazo Mimi niliziona za kipuuzi na kitoto, kwani Kwa. Uelewa wake alidhani mungu anayemuamini yeye basi ni mungu wa watu wengine.

Gwajima kupitia kauli yake ya kutisha Madaktari namlimgamisha na Wale masheikhe waliomtishia Afande Sele wakidhani mungu wao ananguvu ya kufanya atakavyo Kwa watu wote Kama afanyavyo kwao. Jambo ambalo ni uongo.

Nikiachana na mambo ya Imani ili nisiguse makundi ya waaminio. Naomba nirejee kwenye hoja.

Gwajima anaongea Kama mtu asiyemtaalamu, anayebebwa na upepo wa propaganda za kitoto na watu wasioenda shule.
Na Kama kaenda shule basi elimu yake itakuwa na Shaka kubwa Sana, sio ajabu Mbunge Msukuma akiwakejeli wasomi ikiwa ndio akili zao zipo Kama hivi.

Gwajima lazima aelewe kuwa ishu ya Corona ipo kitabibu zaidi kuliko porojo zake au Siasa ambazo ni kuongea tuu.

Kuwaambia Madaktari ati wachunguze contents zilizopo ndani ya Chanjo ya Corona ni kujaribu Kueleza kuwa Madaktari WA nchi hii hawajui wajibu na kazi Yao.

Gwajima anataka kuwaambia Waumini na wasikilizaji wake kuwa, Madaktari wa Tanzania huwaga hawafanyagi uchunguzi katika madawa yanayotoka nje.

Gwajima anafikiri kuwa Madaktari WA Tanzania wanaongozwa na Teolojia inayomuongoza yeye ambayo ni Tawi la Falsafa ambayo Wachungaji huitumia kuwafundisha watu habari za Mungu, Jambo ambalo sio kweli. Madaktari huongozwa na Sayansi zaidi kuliko masuala dhahania.

Gwajima anajifanya anaakili mbele ya waumini na wasikilizaji wake na hawapi nafasi ya kufikiri kuliko upeo ili aonekane kaongea hoja yenye manufaa wakati Kwa akili ndogo ni kuwa ameongea pasipo kufikiri vizuri.

Kama Gwajima angetoa nafasi ya kuulizwa maswali huenda angejidharau pale pale na kujiona ameongea vitu visivyopaswa kuzungumzwa na mtu Kama yeye.
Mfano wa maswali;

1. Tangu nchi imepata Uhuru, ni lini Madaktari walitaja contents zilizopo kwenye madawa yatokayo nje au hata Chanjo ambazo tulichanjwa?

2. Kwa nini Gwajima Hana wasiwasi na Dawa zingine Kama vile ARVs, chanjo wapigwazo watoto wachanga, au wamama wajawazito, Kwa nini iwe Chanjo ya Korona na sio hizo?

3. Gwajima amegusia suala la biashara imejiingiza kwenye suala la Chanjo ya Corona, yupo sahihi. Ni Ugonjwa upo ambao sio biashara?
Na ni Huduma gani isiyobiashara Kwa sasa? Mbona hata kwenye dini biashara imejiingiza, yeye anaona Kwa wenzake haoni upande wake.

Gwajima alikuwa anaelezea Jambo ambalo Hana Uelewa nalo Kwa sababu yeye sio Daktari, hivyo kujifanya anaamrisha mambo asiyo na Uelewa nayo ni Kama kujivua nguo mbele za watu.

Gwajima sijui hajui au anafanya ukaidi, mambo mengi tunayoyatumia iwe Kwa kula au kutumia kawaida yanatoka nchi za nje, Kwa hao hao Wazungu. Hivyo Kama ni kutumaliza wangetumaliza hata kabla Gwajima mwenyewe hajazaliwa.

Gwajima anaweza akawa na hoja lakini uwasilishaji wake umekuwa wakijinga Kwa sababu maoni yake anajaribu kuyalazimisha na kutisha watu, huku akielezea mambo asiyo na utaalamu nayo.

Mahali ninapoungana na Gwajima;
Ninaungana na Gwajima ile siku alipompinga Mbowe kuhusu kauli yake kuwa Chanjo iwe Lazima,
Gwajima anajaribu kuifichua tabia ya Mbowe ya udikteta ya kulazimisha Chanjo ya Corona Kwa wote badala ya kutumia Demokrasia.

Hata hivyo Gwajima naye anajisahau, anataka kulazimisha watu wakatae Chanjo ya Corona badala ya kuruhusu demokrasia Kama Tamko la serikali lilivyoelekeza kuwa; Chanjo ya Corona ni Hiyari.
Anayetaka akapigwe, asiyetaka aache.

Gwajima usiwaze Kama mtu asiye na Uelewa wa mambo.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
MOROGORO
 
... hataki chanjo akae pembeni sio kuwatakia vifo walio tayari kuipata. Jinga sana yule askofu magumashi mbunge kilaza wa CCM.
 
Nashkuru katika uzi wako wote hujalinajisi jina 'Askofu' .
Nilidhani utam-refer kama 'Askofu Gwajima' ila hujafanya hivyo.

Napendekeza pia neno 'Mheshimiwa' liheshimiwe, tusilitumie hovyo hovyo kwa hawa wahuni wa ccm.

Hatuwezi kumuita 'Askofu' mtu asiyekuwa hata na chembe ya maadili achilia mbali ucha Mungu/utumishi
 
... "nileteeni Gwajima! Nireteeeeni Gwajiiima! Nireteeeeeeeeni Geajimaaaaaaa!". Connect dots! Tunaposema Katiba Mpya watu wachaguliwe kwa sifa badala ya ubabaishaji.
 

Ndio Mkuu, nimezingatia hayo. Nisije dhalilisha Kazi za watu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…