#COVID19 Askofu Gwajima: Ni jambo baya sana kuwapa Chanjo ya Corona Wanajeshi, Polisi na watu wa Usalama

Vaccine shilling threads will be on a high note this coming month
 
Nakubalii nakubalii. chanjo sidungwi, najua tutafika wakati tusiochanjwa hatutaruhusiwa kununua kitu chechote lakini nimejiandaa. Nitakula nyasi za shambani kwangu
 
Kila nikiifikiria serikali ya CCM chini ya magufuli jinsi ilivyolichukulia swala la corona, na serikali ya ccm chini ya Samia inavyolichukulia swala la corona, na hapo hizo Serikali zimepishana chini miezi 6, napata wasiwasi Sana na mtu aitwaye mwanasisa!
 
Shari peleka kwenu chanjo ni hiari wacha watu watumie hiari yao
Watanzania mlio wengi (isipokuwa Mimi na wenzangu wachache) bila shuruti hamtii na kufanya mambo yenye faida kwenu.
 
Watanzania mlio wengi (isipokuwa Mimi na wenzangu wachache) bila shuruti hamtii na kufanya mambo yenye faida kwenu.
Tanzania pamoja na kukandamizwa na viongozi wengi walio na UBINAFSI (dhambi kuu ya nchi hii) bado Mungu anatuhesabu kama wanadamu wenye kiwango kikubwa cha Imani(high spiritual sensitivity) ndio maana tumebarikiwa sana.

Sasa hivi wenye upendo mkubwa na nchi hii wako wanaanda namna ya kugeuza idadi kubwa ya watu tuliobarikiwa na mwenyezi Mungu kuwa rasilimali. Mara tukifanikiwa Jambo hilo Africa na dunia itatambua ukuu wetu.

Mungu huwalinda na kuwabariki wenye maarifa Mithali imeandika hivyo tuongezee bidii kuyatafuta maarifa ya kweli.

#ONYO: Usimdhihaki Gwajima kama huwezi kujibu maswali yake. Amefanyika kuwa sauti ya wengi.
 
Hakuna ubinafsi zaidi ya huo anaoufanya Gwajima, anawarubuni waumini wake ambao huenda walio wengi ni wajinga.

Tanzania ni nchi sawa na nchi zingine, Wala hakuna kundi la watu waliodhamiria kutumia dawa/chanjo kufanya maangamizi kwetu.

Chanzo cha haya yote ni Paranoic leader aliyewahi kusema Mabeberu wanataka kutuua kwa kutumia chanjo wakati tuna vitu vingi vya Wazungu tunavyotumia bila hata kujua teknolojia yake ikoje.
 
#TujitokezeKuchanjwaChanjoYaUviko
#NchiKwanza
#KaziIendelee
 
Mbona nyie makada mmeshupaza shingo kuipakiki Corona na hayo machanjo yenu
 
Nenda kachanjwe buda ww
 
Acha UPOTOSHAJI wewe unataka kumpinga mtu anayekusanya takwimu za wanaolazwa ná kufa kwa COVID-19!? Watu kama wewe ni hatari sana ni hasara kubwa Kwa Taifa. Ulichoandika ni UONGO MTUPU!!!
Mimi nayewaambia watu kuhusu ukweli wa chanjo wasichanjwe wasichokijua Vs wewe unayewahamasisha watu wachanjwe wasichokijua yaani watu milioni 60 wageuzwe majaribio ya wazungu ni nani hatari kwa usalama wa taifa?
 
Unaonaje ukitoa takwimu za chanjo zenye ahueni zisizofuata kanuni ya MRNA ili tuanze kuzifuatilia kabla hatujalazimishwa kukinga mabega
Kuna chanjo kama

Novavax ya Marekani


Sinopham ya China



Spurnk V ya urusi

Hizi zote sio mrna
 
Kwahiyo wewe unatuletea stori zako zinazopromotiwa na watengenezaji chanjo na big pharma? Kwani unalipwa shilingi ngapi eti[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]waambie hao wenzako kwamba hatuchanjwi mrna ng'oo
 
[emoji13][emoji13][emoji13][emoji13][emoji13][emoji13]kumbe!!!!!!!!!!
 
Wewe ndo mpumbavu,mjinga tena brainwashed na hao bwana zako mimi unaniforce nimsikilize dr fauci ambaye an share kwenye hayo makampuni?wewe utakua mgonjwa sio bure
 
Haya tueleze Bwana Molecular Biologist hiyo mRNA inaingia vipi kwenye cytoplasm na kuungana na DNA.
Au ndiyo akina amfifiro????
Akina amfifiro?wewe ni mpumbavu wa mwisho kwahiyo unadhani hizi ni propaganda kama hizo zenu nyie mawakala wa bilgate?
 
Gwajima ni mtu mjinga sana.
 
Well said mkuu.....akasome ripoti ya wizara ya afya ya 2013 kuhusu onyo juu ya mlipuko wa mafua yanayoitwa corona ilikua 2013 na huo uzi ulikuwepo humu ngoja niutafute
 
Kaka....ona hii


TAARIFA KWA UMMA. TAHADHARI YA UGONJWA WA NIMONIA INAYOTOKANA NA CORONA VIRUS

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, imepokea taarifa kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) mnamo tarehe 22 Mei 2013, kuhusu kuwepo kwa ugonjwa wa Nimonia unaosababishwa na kirusi cha Novel Coronavirus.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa,tangu ugonjwa huo utokee mwishoni wa mwaka 2012 hadi tarehe 23 Mei 2013 idadi ya wagonjwa wapatao 44 na vifo 22 viliripotiwa

Shirika la Afya Duniani limethibitisha ugonjwa huu kuwepo katika nchi za Mashariki ya Kati yaani Jordan, Qatar, Saudi Arabi na Falme za Kiarabu (UAE). Katika bara la Ulaya, ugonjwa huu umethibitishwa kutokea nchi za Ujerumani, Ufaransa, na Uingereza. Katika bara la Afrika, ugonjwa huu umetokea Tunisia.

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inapenda kutoa tahadhari ya Ugonjwa huu kwa wananchi wote, katika mikoa yote ya Tanzania na hasa wale wanaosafiri kuelekea maeneo tajwa yenye uthibitisho wa ugonjwa huu.

Ugonjwa huu unaenezwa na kirusi kiitwacho novel coronavirus (nCoV).

Dalili kuu za ugonjwa huu ni kushindwa kupumua kwa ghafla, homa kali, kukohoa, na kubanwa na mbavu na hatimaye kupata Nimonia.

Dalili nyingine ambazo zinaweza kutokea ni pamoja na kupata maumivu makali ya tumbo pamoja nakuharisha. Vile vile ugonjwa huu unaweza kupelekea figo kushindwa kufanya kazi na hata kusababisha kifo.

Kipindi cha kuonekana kwa dalili za ugonjwa huu ni kati ya siku 2 hadi 10 baada ya kupata maambukizi. Ugonjwa huu hauna tiba wala chanjo.

Ugonjwa huu unaweza kuambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.

Njia za maambukizo bado hazijajulikana ingawa uwezekano mkubwa wa maambukizo ni kwa kwa njia ya hewa (kukohoa/kupiga chafya) au kwa kugusa majimaji/makamasi kutoka kwa mgonjwa aliyethibitishwa kuwa na ugonjwa huo.

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, imechukua hatua zifuatazo katika kukabiliana na tishio la ugonjwa huu:

Kutoa taarifa ya tahadhari ya ugonjwa huu kupitia kwa Waganga Wakuu wote wa Mikoa na Wilaya kwa Tanzania bara.

Aidha, taarifa hii pia imejumuisha namna mgonjwa anavyoweza kutambuliwa (Ainisho la Ugonjwa),

Fact sheet ya ugonjwa, Mwongozo kwa watumishi wa afya wa namna ya kuchukua sampuli ikiwa ni pamoja na vipeperushi vinavyoelezea jinsi ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huu.

Kuimarisha ufuatiliaji wa ugonjwa huu kupitia kwa Wataalamu wa Afya katika Mikoa, Wilaya na maeneo ya mipakani. Aidha watalaamu hawa pia wanatoa elimu kwa wananchi kuhusu dalili za ugonjwa huu na jinsi ya kujikinga na maambukizi ili endapo ugonjwa huo utatokea uweze kutolewa taarifa mapema.

Wizara inasisitiza kuwa hakuna vikwazo vyovyote vilivyowekwa kwa ajili kwa wasafiri watakaokwenda au kurudi katika maeneo tajwa yaliyothibitishwa kuwa na ugonjwa huu. Vipeperushi vya ugonjwa huu vimetumwa katika maeneo ya mipakani ili iwapo msafiri anayeondoka au kurudi nchini akiwa na dalili tajwa atoe taarifa kwa watumishi wa afya wa mpakani ili hatua stahili ziweze kuchukuliwa.

Kutoa mafunzo kwa watumishi wa afya na mipakani wa namna ya kutambua na kujikinga dhidi ya maambukizo ya ugonjwa huu pamoja na uchukuaji wa sampuli iwapo mgonjwa atapatikana

Kupeleka vifaa kinga kwa ajili ya watumishi wa afya Wananchi wanashauriwa kutokuwa na hofu kwani mpaka sasa hakuna mgonjwa yeyote aliyeripotiwa nchini. Wizara inapenda kutoa tahadhari kwa wananchi juu ya umuhimu wa

KUNAWA MIKONO VIZURI KWA SABUNI NA MAJI MARA KWA MARA na pia KUZUIA MDOMO NA PUA KWA KITAMBAA AU KARATASI LAINI WAKATI WA KUKOHOA AU KUPIGA CHAFYA.

Pia wananchi wanashauriwa kutoa taarifa kwenye kituo cha kutolea huduma za afya kilicho karibu mara watakapoona mgonjwa yeyote atakayehisiwa kuwa na dalili za ugonjwa huu.

Imetolewa na;

Nsachris Mwamwaja
Kitengo cha Mawasiliano ya
Serikali
30/05/2013

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…