#COVID19 Askofu Gwajima: Ni jambo baya sana kuwapa Chanjo ya Corona Wanajeshi, Polisi na watu wa Usalama

Huwa wanajeshi wanatumika wachache tu Kwa ajili ya majaribio na sio wote.

Sasa mamlaka waangalie namna wanafanya,

Isiwe wote ila Wachache tu Kwa ajili ya kuangalia uelekeo wakee.
Panya wa majarubio si wapo wengi tu
 
Ina maana Gwajima haamini kamati ya wataalamu iliyoundwa na Mhe. Raisi Samia Suluhu Hassan ya kushauri ya nini kifanyike kuhusu COVID-19 na chanjo? Huu kwangu ni utovu wa nidhamu na kudharau wataalamu wetu. Ni imani yangu wataalamu wetu wamepitia na kuthibitisha ubora/uimara wa chanjo itakayotumia kuchanja wananchi wetu including vyombo vya usalama.
Watalamu walisema siyo lazima
 
Habari!

Hili jambo nililisikia 2020 toka kwa waumini 2 wa Gwajima.

Mimi niko karibu na waumini kadhaa wa Askofu Gwajima ambapo kati yao 2 ninafanya nao kazi ofisi moja, idara moja. Na hao wote ni wachungaji wa kikundi (Ministry pastors) wa kanisa la Ufufuo na Uzima.

Aliamini huenda angerithi mikoba ya Magufuli 2025 lakini Magufuli ametangulia mbele za haki.

Je, atasubiri mpaka 2030 pindi atakapomaliza Rais Samia Suluhu?
Hapana.

Hataweza kusubiri 2030 bali atajaribu karata yake ya bahati 2025.

Msitegemee 100% kuwa Gwajima atamuunga mkono Rais Samia Suluhu kwa sasa.

Gwajima mtu mwenye akili nyingi anaweza kuipiga ngome ya mama na ikapigika. Ngoja tusubiri.

Hii ni tetesi hivyo naomba msiufute huu uzi, hauna dhamira ya uchochezi.
SUKUMA GANG wameanza MASHAMBULIZI
ya URAIS MAPEMA
Tulimwambia Mama Wabunge na Mawaziri sio Wake ni wa MAGUFULI Dharua ya SPIKA kuhusu Tozo Na Gwajima kuhusu Chanjo wamezionyesha Mapema
 
je wewe kama mTanzania mpenda nchi yako unaionaje kauli ya askofu Gwajima kuhusu corona je ameongea kama mzalendo au anatumika

msikilize hapa chini
 
Nimeona video inayomuonesha Mchungaji Gwajima (Mbunge wa Kawe) akiwahimiza waumini katika kanisa lake kutokuchoma chanjo ya UVIKO.

Kwa namna nyingine amewatishia Wataalamu watakaohusika kuhamasisha matumizi ya chanjo hiyo kuwa wakifanya hivyo watakufa. Anadai anataka Wataalamu hao wajiridhishe na contents za chanjo hiyo kama ni salama kwa matumizi yetu.

Mheshimiwa Rais tumeshuhudia jitihada zako katika kupambana na janga hili la Corona, ni katika awamu yako tumeona pia Waziri wa afya akihamasisha wananchi kuzingatia ushauri wa wataalamu kujikinga na UVIKO.

Rais ulienda mbali na kuunda kamati maalumu ya Wataalamu ili wakushauri namna bora ya kukabiliana na ugonjwa huo, ripoti na mapendekezo ya Wataalamu ndiyo chanzo cha uagizaji wa chanjo baada ya kuthibitika zina faida kubwa katika kupambana na UVIKO 19.

Pamoja na kuwa mmeelekeza kuwa chanjo hiyo ni hiari lakini bado wanatokea watu kama Gwajima anawarubuni Watanzania bila kufikiria madhara makubwa yanayoweza kuwakumba.

Nimesikia kuwa Jumanne tarehe 28 July utakuwa unazindua matumizi ya chanjo hizo.

Ninashauri iundwe kamati ndogo ya uhamasishaji wa chanjo ya UVIKO itakayoundwa na Wataalamu, Viongozi wa dini na Wanasiasa.

Mojawapo ya watu watakaoshiriki katika kamati hiyo awe Mchungaji Gwajima.

Wanakamati hao wapewe elimu na waelewe vizuri maana halisi ya chanjo inayotolewa, matumizi yake na madhara yake. Kamati hiyo uitangaze siku hiyo ya Jumanne.

Nawasilisha.
 
Na wewe uwe kwenye kamati hiyo
 
Naamini Mh Mbowe ameonewa katika tuhuma zinazomkabili, lakini nikikumbuka kauli yake ya "chanjo ni lazima kwa wote" , naomba akae wiki tatu mahabusu Huku anapigwa miti Kisha aachiwe
 
Back
Top Bottom