beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,880
- 6,368
Mbunge wa Jimbo la Kawe, Askofu Josephat Gwajima ametaka kuwepo umakini wa kuchagua Chanjo dhidi ya Ugonjwa wa COVID-19. Amesema hayo akiwa Bungeni Dodoma leo wakati wa Mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Afya iliyowasilishwa na Waziri Dorothy Gwajima.
Amefafanua, "Mimi sipo kinyume na Chanjo za Corona wala chanjo yoyote. Mtu asininukuu napinga chanjo, hapana. Tanzania tulishachanjwa Chanjo ya Kifua Kikuu, Surua, Kifaduro na Polio''.
Amesema ni kweli Tanzania ikikataa Chanjo inaweza kuwekewa zuio la kwenda Ulaya. Ameeleza, "Tunakabiliwa na uchaguzi mbaya sana, tuchanjwe kitu tusichokijua sawa sawa au tusichanjwe tuzuiwe kwenda Ulaya".
Ameiomba Wizara ya Afya kuangalia suala la Chanjo kwa umakini, akisema waangalie madhara ya sasa, ya siku zijazo na ya Taifa. Ameongeza kuwa, tatizo lililopo ni kufikiri kila kinachotoka Ulaya kinafaa.
Amesema, "Before we venture into what kind of vaccine we should take, tunatakiwa tuwe na wataalamu wetu wa hapa".