DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Dkt. Josephat Gwajima, amesema ataendelea kushiriki ibada kanisani hapo kila Jumapili bila woga wowote, akisisitiza kuwa hawezi kuepuka kusimama hadharani kwa sababu ya vitisho au hofu.
Akizungumza katika ibada ya mwaka mpya iliyofanyika usiku wa kuamkia Januari 1, 2026, Gwajima amesema alipokea jumbe nyingi kutoka kwa watu mbalimbali wakiwemo wanaojiita manabii, mitume na maaskofu wakimtahadharisha kutojitokeza hadharani, lakini aliamua kupuuza ushauri huo.
Amesema ujasiri haumaanishi kukosa hofu, bali ni kuelewa kusudi la mtu duniani, akiongeza kuwa yeye anajua kilichomleta duniani na hawezi kuyumbishwa katika kusimama kwake kwenye imani.
Gwajima amekumbusha msimamo wake wakati wa janga la UVIKO-19 (Corona), akieleza kuwa wakati wengine walikuwa na hofu, kanisa lake liliendelea na ibada na hata kujenga jengo la ghorofa kadhaa, jambo alilolitaja kama ushuhuda wa imani isiyotetereka.
Askofu Gwajima amesisitiza kuwa yuko tayari kufuatwa kokote atakakokwenda kwani hana hofu juu ya usalama wake, akionesha imani kuwa yuko salama.
Soma pia PreGE2025 - Askofu Gwajima: Utekaji si utamaduni wetu na halitakiwi kuchekewa!