Mimi nakupenda sana tangia kipindi cha covid 19. Misimamo yako naipenda sana ikiwa unasema ukweli. Siku unahubiri kanisani kuhusu utekaji nilikuwa nakufuatilisa vizuri. Tangia unaingika kanisani nilikufuatilitia vizuri.
Lakini mh Askofu niliingiwa na hofu kuu sana nikajiuliza hiki nini kimetokea. Kuhubiri juu ya utekaji siyo mbaya, lakini namna ulivyoanza mahubiri yako siyo heshima kwa Mungu na kwa taratibu za kanisa lenye kuwalisha kondoo neno la uzima. Unaanza kuhubiri kabla ya kusoma neno la MUNGU? Pale kanisani tunaenda kusikiliza neno la Mungu kwanza. Leo Mungu wetu ametuandalia nini watoto wake, kama chakula cha uzima?
Neno la Mungu ndiyo chakula cha uzima, mengine pale ulikuwa unapiga blablaa tu. Yale maneno yako ya siku ile hayawezi kuwapa watu uzima na kuwapeleka watu mbinguni. Kama ni kuhubiri kuhusu utekaji, ulitakiwa utafute kifungu kwenye Biblia KINACHOENDANA NA MAHALIFU KATIKA jamii, ukifananue vizuri, ndiposa uchomekee maneno kuhusu utekaji unaotokea nchini.
Kosa lingine ni kumtaji mkuu wa nchi japo indirectly kwamba anahusika na utekaji. Kwa kweli ulipotamka kwamba anayekupinga tujiulize anahusikaje kwenye utekaji, moyo uliniuma sana kwa sababu niliona sasa umekwea kwengine ambako kutoka huko itakuwa shida. Mh Rais kwenye chama alikujibu kiimani, wewe ukatafsiri amekupinga.
Lakini hata kama angekuwa amekupinga, wewe kama askofu uchungaye kondoo hukutakiwa kuwaonyesha waumini wako tena kanisani kwamba sasa inajulikana anayeagiza watu watekwe ni huyu, maana bado huna ushahidi. Na hata kama una ushahidi bado huna uwezo wa kupambana na taasisi ya uraisi. Na kwa nini wewe kama mchungaji wa kondoo uwe chanzo cha machafuko? Hatufanyagi hivyo mzee.
Unakumbuka lile neno YESU KRISTO alilowambia wanafunzi wake wakati anawatuma ulimwenguni? Au wewe siyo mwanafunzi wa YESU kwa sababu ni askofu?
Angalieni, mimi nawatuma kama kondoo kati ya mbwa-mwitu; basi iweni na busara kama nyoka, na kuwa watu wapole kama hua.
sasa wewe unakuwa mkali badala ya kuwa mpole .unategemea nini ?
unakumbuka kisa cha cha jogoo wa wili jasiri na mwoga?
nakushauri uombe msamaha kwa mkuu wa nchi na pia kwa MUNGU na kwa waumini.umesababisha kondoo kutawanyika sasa hawana mchungaji? umesababisha uitwe mtumishi wa shetani na siyo wa Mungu.Hii ni kosa lako kubwa.Nakuomba ukatubu
jifunze kwa YESU .yeye ni mpole na mnyenyekevu
wakati mwingini upole ni mhimu sana.ache wengine waongee wewe baki katika kuwaombea waongeaji wapate hekima na busara katika kuongea.

Mt 10:16
Angalieni, mimi nawatuma kama kondoo kati ya mbwa-mwitu; basi iweni na busara kama nyoka, na kuwa watu wapole kama hua.
sasa wewe unakuwa mkali badala ya kuwa mpole .unategemea nini ?
unakumbuka kisa cha cha jogoo wa wili jasiri na mwoga?
nakushauri uombe msamaha kwa mkuu wa nchi na pia kwa MUNGU na kwa waumini.umesababisha kondoo kutawanyika sasa hawana mchungaji? umesababisha uitwe mtumishi wa shetani na siyo wa Mungu.Hii ni kosa lako kubwa.Nakuomba ukatubu
jifunze kwa YESU .yeye ni mpole na mnyenyekevu
Mt 11:29
Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenuwakati mwingini upole ni mhimu sana.ache wengine waongee wewe baki katika kuwaombea waongeaji wapate hekima na busara katika kuongea.